Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hali ya Kikanda, uchoraji mipaka ya ardhi!

Kuweka matayarisho katika kambi ya Ain al-Hilweh kwa ajili ya vita na operesheni za usalama
(Imetafsiriwa)

Majed Faraj, mkuu wa Huduma Kuu ya Ujasusi katika Mamlaka ya Palestina, aliwasili mnamo 24/7/2023 na kukutana na uongozi wa ngazi ya juu nchini Lebanon. Iliripotiwa kwamba aliomba mkutano na Ziyad Nahaleh, Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad ya Kiislamu, ambaye alikataa mkutano huo na kuishia kwa mazungumzo ya simu. Baadaye, Faraj aliondoka kwenda Uturuki mnamo 25/7/2023, ambapo alikutana na Mahmoud Abbas ambaye, alikutana na Ismail Haniyeh jioni ya 25/7/2023. Kufuatia hili, Faraj aliruka kwenda Misri kushiriki katika mkutano wa makatibu wakuu wa vikundi vya Palestina jijini Cairo mnamo 30/7/2023.

Kwa hivyo, ni harakati gani hii ya usalama isiyo ya kawaida na yenye tashwishi?! Hasa kwa kuwa ziara hii ya Mkuu wa Ujasusi *ilihitimishwa* kabla ya hali kulipuka katika kambi ya Ain al-Hilweh mnamo 29/7/2023 bila onyo la kabla! Walakini, sehemu kutoka kwa harakati ya Fatah ilifyatua risasi katika shambulizi kwa kisingizio cha kulipiza kisasi, na kumuua kijana na kuwajeruhi wengine, pamoja na wasichana wawili. Tukio hili likawa cheche ambayo ilichochea tukio la kiusalama ambalo ushiriki wa upande mwingine haujulikani! Na ndani ya masaa machache tu, kwa njia ya kushangaza na katika shambulizi lililotekelezwa vizuri mnamo 30/7/2023, kamanda wa usalama wa kitaifa wa Palestina, Abu Ashraf al-Armoushi, pamoja na wenzake wanne, waliuawa katika eneo lao la udhibiti!

Kinachoweza kusemwa sasa ni kama ifuatavyo:

- Kuna mambo muhimu yanayojiri nchini Lebanon, ambayo ni suala la uwekaji mipaka ya ardhi, ambalo liko chini ya udhamini wa Marekani, lililokubaliwa na mamlaka za Lebanon, na kukubaliwa na vyama vya Lebanon, haswa chama kinachoungwa mkono na Iran nchini Lebanon. Hivyo basi, inahitajika kwa ajili ya hali iliyoko nchini kudhibitiwa kwa ushiriki wa Marekani.

- Uamuzi huo ulifanywa ili kujumuisha chembe zilizotawanyika za harakati za Fatah ndani ya kambi na kuregesha udhibiti kwa Mamlaka ya Dayton, ambayo inashikilia uratibu “mtakatifu” wa usalama, juu ya kambi. Hii inafanywa na watu ambao wanaahidi utiifu kamili kwa mamlaka hii, ambayo imeegemea wazi kwa Marekani.

- Hapo awali, ilionekana kuwa vita vilikuwa vya upande mmoja, vilivyochochewa na chama kimoja. Walakini, ili kupata kisingizio cha kufikia malengo yake ya kisiasa na usalama, kikundi kinachojulikana kama al-Shabab al-Muslim kilisukuma kwenye mzozo, ingawa hawakuhusika katika matukio ya hivi karibuni au yaliyotangulia.

- Vikundi vyengine vya Palestina vimeanza kufanya kazi ndani ya ajenda za kikanda, ama zilizowekwa na Marekani, kama vile serikali ya Syria, au ndani ya mzunguko wa Marekani, kama Iran.

- Vikosi vya usalama vya Lebanon, vinavyojulikana kwa kuingilia kati kwao kumaliza mapigano ndani ya masaa, vinaonekana kuruhusu hali hiyo kuongezeka kwa kiwango kamili. Hii inaambatana na majaribio ya kisiasa ambayo yameshindwa kushughulikia uzito wa hali hiyo. Hii inazua mashaka juu ya asili ya ziara ya Majed Faraj, mikutano yake, na kile kilichojadiliwa wakati wa hayo.

Na hapa tunatoa onyo:

- Matokeo ya kitendo hiki kiovu - kuwaua watu, kuwatisha, na kuharibu mali zao - yatakuwa ni udhibiti wa vikundi vinavyonasibishwa na Marekani juu ya kambi, ima moja kwa moja kupitia Mamlaka ya Dayton au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia serikali ya Syria na Iran.

- Kuendelea na mipango kama hiyo ya uharibifu, ya umwagaji damu inapaswa kuhamasisha mamlaka za Lebanon kuingilia kati haraka na sio kuchelewesha kwa kisingizio cha miradi ya nje. Hili ni jukumu lao kwa ustawi kama serikali na mamlaka.

- Tunatoa ushauri wetu kwa wakaazi wa kambi ambao wana silaha, tukiwasihi wasiingizwe katika njama hii. Haiwezi kukanwa kuwa kuna msaada unaopeanwa kwa harakati za Fatah kutoka kwa vyama fulani na vikundi ambavyo vinaona upanuzi wa udhibiti wa Fatah juu ya kambi kama wa kweli zaidi kuliko madai ya udhibiti wa "wenye msimamo mkali."

- Na kwa washiriki wa harakati ya Fatah, tunasema: Munamfyatulia risasi nani? Hasa kwa kuwa munatumia silaha nzito kama mabomu na zenginezo. Je! Hili ni kwa ajili ya kuua watu, au ni kwa ajili ya uharibifu wa makusudi na uharibifu wa vitongoji ili kuendeleza mpango? Jihadharini na wale wanaokuongozeni dhidi ya watu na nyumba zenu wenyewe, na katika kuhudumia njama yao!

[وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.”  [Al-Anfal: 25]

H. 13 Muharram 1445
M. : Jumatatu, 31 Julai 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu