Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Taarifa kwa Rai Jumla Nchini Lebanon

Kufilisika Kifikra katika Kupendekeza Suluhu ya Mgogoro wa Kiuchumi

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu Hassan Diab alitangaza katika hotuba moja – baada ya kutia saini pamoja na Waziri wa Fedha Ghazi Wazni, mnamo Ijumaa 1/5/2020 – “Tumeanza na hatua ya kwanza kuelekea katika warsha ya kuiokoa Lebanon kutokana na pengo la kiuchumi ambalo ni vigumu kuliepuka bila uzalishaji na msaada fanisi: - (Chanzo: Al Jazeera Net 2/5/2020), hii ni wakati wa maoni yake juu ya kutia sahihi kwa ombi rasmi la serikali ya Lebanon la kuomba msaada kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, akielezea – kulingana na baadhi ya habari – “matumaini yake kwamba ombi la kutaka msaada kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa litaanzisha hatua ya mabadiliko katika njia ya mporomoko wa kifedha na uhalisia wa kiuchumi.”

Hii ni sera ya kijinga ya kiuchumi ambayo ilipitishwa nchini Lebanon baada ya kumalizika kwa vita vya Lebanon na kurudi kwa hali ya kawaida, sera ilioundwa juu ya mtazamo wa kujisalimisha, ambao ndio utambuzi wa awali kwamba mizani ya kibiashara iko na upungufu wa daima, na kwamba hasara hii itafidiwa – katika hali ya muendelezo – kwa pande mbili za “Zakum (mti wenye miiba (motoni) na Hamim (maji yachomayo)”; ya kwanza ni mkopo wa nje wenye riba, na ya pili ni kwa kuvutia uwekaji wa ndani na nje kupitia vishawishi vya riba.

Kwanza, mfumo wa fedha umedungwa sindano ya ganzi ya deni la nje “Paris 1, 2 na 3, kisha Sidar...” Itafufua uchumi uliolewa na dozi ya pesa za mara kwa mara, mpaka athari yake imalizike kwa kila hisa za sarafu zinapo malizika, na hivyo uchumi kuingia katika kimbunga cha kuzima moto kwa mafuta, kisha kuwasha moto kwenye mafuta!

Pili, inauwa uwekezaji wa uchumi halisi, kwa sababu viwango vya juu vya riba (fa’ida) vinawafanya wamiliki wa mitaji kusitisha kuwekeza katika uzalishaji wa mali ya kutosheleza soko la ndani na kuimarisha lira, ama kuwekeza katika kuzalisha bidhaa za ziada ili kuleta sarafu nchini!

Leo, nchi inaongeza janga la tatu, mpango na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao wanasiasa wa Lebanon wanajaribu kuuonesha kama mkombozi, kana kwamba Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni shirika la hisani, ambalo litatumia kutoka katika pesa za nchi kuu kwa Lebanon kupeana ruzuku bila ya kuzilipa, masharti au matokeo!!!

Licha ya sifa yake mbaya kwa karne nyingi zilizopita, na licha ya kufeli kwake katika kusaidia nchi yoyote hapo mbeleni, nchi ya Lebanon badala yake ilienda kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuomba dolari bilioni 15, ambazo inahitajika kutekeleza sheria ilizopewa na IMF, ikiwemo kusitisha ruzuku katika mali asili, kuongeza kodi kwa watu, kushukisha thamani ya lira ya Lebanon, ama kusitisha sera za kudhibiti kiwango cha ubadilishanaji, sheria ambazo zimeleta hasara kwa thamani ya lira kwa zaidi ya asilimia 57, kulingana na waraka uliopitishwa na serikali, yote haya kiasili huongeza umaskini baina ya watu wa kawaida, umaskini ambao umekuwa wazi; Dolari ya Amerika imekuwa dhidi ya lira kufikia takribani lira 4400 kwa dolari moja, kisha ikarudi na kushuka mpaka 3550 baada ya dolari kabla 17/10/2019 ilikuwa sawia na lira 1508 kwa dolari moja; mshuko uliopelekea watu kupata hasara katika thamani ya mishahara yao ya kila mwezi na malipo ya uzeeni.

Njia ya kufeli kwa dola hii imekuwa dhahiri! Lakini nini baadaye? Je, suluhu zilizo peanwa na watu na vuguvugu lao zitabakia kuwa ndani ya duara hilo hilo lililoasisiwa juu juu ya mfumo na kundi lenyewe?

Baada ya vuguvugu la 17/10/2019, utambuzi wa ukweli muhimu miongoni mwa watu uliimarishwa; kwamba Lebanon ni nchi iliyotekwa nyara na kikundi cha wanasiasa, ambo mali zao zinapotea kwa sababu ya ufisadi, na kufilisika ama karibu na kufilisika. Hii ni hatua ya mbele katika kuitazama dola, na kuzikataa nyuso za jadi ambazo Lebanon imezirithi baada ya athari za vita. Hata hivyo, watu bado wanaonekana kuwa hawaja tambua kwamba pale walipo sio kwa sababu ya kufilisika kimwili pekee, lakini ni kwa sababu ya kufilisika kukubwa, ambako kunachangia hali ngumu za kimaisha. Ni kufilisika kwa kifikra ndiko kunako wafanya wanasiasa nchini Lebanon, iwe utawala wa jana ama wa leo, kufuata mienendo hiyo hiyo, ambayo kwayo Lebanon inachinjwa mshipa hadi mshipa,  mbinu ya kiuchumi imesababisha - kwa miaka mingi – kupotea kwa pesa za ummah, na kutua fedha, na kufanya jabali la deni kutua katika mabega ya nchi na watu, bila mwangaza wa matumaini wala taa mwishoni mwa kiza cha handaki!!

Kwa hivyo, mawazo ya serikali hii, inayoitwa kama serikali ya wajuzi, huja tu (na suluhu sawia na zile za jadi), na mkanganyo wote huu, kujiiga na kurudia mbinu, hayafanywi isipokuwa kwa sababu ya kupotoka kuhusu suluhisho msingi kutoka nje ya nidhamu ziliopo, nidhamu zilizo fichuliwa na janga la virusi vya Korona, na zikatingishwa katika viwango vyote.

Suluhisho msingi ni suluhisho la kiroho, suhuhisho linalo haramisha kuamiliana na riba katika viwango vyote, kibinafsi, kiserikali au kimataifa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ * فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ﴿

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe. [Al-Baqara 278-279]

يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ﴿

 “Mwenyezi Mungu huiondolea Baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.” [Al-Baqara:276]

Wakati huo huo, inafanya pesa kuzunguka miongoni mwa watu,sio miongoni mwa matajiri.

مَّا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ﴿

“Mali alioileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Mtume wake, na jamaa, na Mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. [Al-Hashr:7] Na akaharamisha kuficha mali.

وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿

 “Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.” [Tawba: 34]

Ni lazima kutoa pesa za msaada kutoka kwa mifuko ya wale wanaomiliki mali iliofikia kiwango cha kisheria (nisab), kwa mifuko ya wale wanao hitaji.

إِنَّما الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿

 “Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima” [Al-Tawba: 60].

Pia inagawanya ardhi nyingi bure kwa wale wanaotaka kuwekeza katika ardhi hizi katika kilimo ama viwanda, ili uzalishaji uongezeke na kufurika na kurudia watu wa nchi hiyo kwa bidhaa nyingi. Omar Ibn Al-Khattab (ra) alisema katika hotuba yake juu ya Minbar: Yeyote atakaye fufua ardhi tasa, ni yake, na atakaye iacha ardhi, basi hana haki juu yake baada ya miaka mitatu.” Omar alisema hivyo na akatenda kulingana na mtazamo na elimu ya Maswahaba – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – na hawakulipinga hilo, hivyo ilikuwa ni makubaliano.

Lebanon ni nchi tajiri kiasili, mali asili, eneo, na viwango vya utaalamu, lakini inahitaji falsafa ya kikweli ili yenye kuokoa akili kabla kufufuka kwa uchumi; hili laweza kuwa pekee kupitia suluhisho za kiroho, Uislamu na suluhu zake.

Katika taarifa hii kwa rai jumla nchini Lebanon, tunataka kuonesha, angalau kiufupi, kufilisika kwa suluhu za kibinadamu na tiba ambazo serikali za Lebanon mtawalia inazikariri na kuzirudia, na tunataka kuelekeza fikra kwa mfumo wa kiroho ambao karibuni utatawala ulimwengu, Mwenyezi Mungu akipenda. Hizb ut Tahrir inafanyakazi kwa bidii kuasisi dola moja, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, chini ya bendera ya Khalifa mmoja, na kwamba Lebanon itakuwa ni sehemu muhimu yake kama ilivyo kuwa nyuma. Ikitekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika siasa, uchumi na jamii, ili raia wa dola hiyo, Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, waishi kwa mafanikio, yaliyo dhaminiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa wale wanaoishi chini ya utawala wake.

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-A’raf: 96]

H. 12 Muharram 1441
M. : Jumanne, 05 Mei 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu