Ijumaa, 12 Sha'aban 1445 | 2024/02/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utawala Usiokuwa na Ruwaza wa Bajwa-Imran Inaunyonga Uchumi Wetu Hadi Kuukosesha Uhai, kwa Kutekeleza Sera za Kikoloni za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Tulishangazwa na mfumko mkubwa mno wa bei ambao hatujawahi kuuona katika miaka kumi na mbili, wa asilimia 14.5, mnamo Januari 2020, huku mfumko wa bei za vyakula ukisimama pabaya kwa asilimia 20. Migongo yetu imevunjwa; noti tulizo zichuma kwa taabu zikituponyoka mikononi mwetu, bila kuona malipo yoyote. Huku maumivu yetu yasiyovumilika yakiongezeka kufikia hadi kupiga mayowe, mshauri mteule wa IMF kwa Waziri Mkuu kuhusiana na Fedha na Mapato, Dkt. Abdul Hafeez Shaikh, alidai mnamo 3 Februari 2020 kuwa, "taifa hili hivi karibuni litaona bei zikianza kushuka." Lakini, serikali inadanganya ili kututuliza, tusipinge ushirikiano wake wa kuendelea na chombo hiki cha kikoloni, IMF, ambacho kimeharibu uchumi wa nchi zenye rasilimali tajiri kote ulimwenguni.

Utekelezaji wa kiupofu wa matakwa ya IMF wa kushusha thamani pesa zetu, umeifanya serikali kuidhoofisha vibaya rupee dhidi ya dola kufikia kiwango cha ubadilishanaji cha Rs. 154.2 mnamo Januari 2020, tulipozama ndani ya mfumko mbaya sana wa bei. Serikali imedhoofisha pesa zetu, kuufanyia marekebisho ya kila mara uchumi wetu ili kupata dola kama pesa za kigeni, kwa lengo tu kulinda malipo ya riba kwa wakopeshaji wa kikoloni pekee. Lakini, kupitia kudhoofisha nguvu ya ununuzi ya Rupee, bei za kila kitu tunachonunua kwa rupee, huongezeka pakubwa. Kuidhoofisha rupee, pia huongeza gharama za bidhaa muhimu kutoka ng'ambo kwa ajili ya sekta ya usafiri, ukulima na viwanda. Na kuidhoofisha rupee huongeza gharama za mikopo na kuongeza deni la kigeni la Pakistan. Zaidi ya hayo, viwango vya juu vya riba vinavyofuata kutoka Benki Kuu ya Dola huongeza pakubwa malipo ya riba, huku ikiwa tayari thuluthi moja ya bajeti hutumika kulipa riba iliyoko juu ya deni, mbali na kiwango asili cha mikopo hiyo. 

Kujisalimisha katika maagizo ya IMF kuhusiana na kawi, serikali iliamrisha kupandishwa kwa ushuru wa gesi na umeme kati ya Julai na Septemba 2019. Serikali hii ilifanya hivyo kulinda faida za wamiliki kibinafsi wa sekta ya kawi kwa gharama yetu. Ubinafsishaji wa rasilimali za kawi huinyima hazina ya dola mapato makubwa kutoka katika sekta ya kawi, ambayo badala yake huyakabidhi kwa maslahi kibinafsi kwa muundo wa mapato na uwekezaji uliodhaminiwa, ikiifanya Pakistan hata kutegemea zaidi juu ya mikopo ya riba ili kukimu gharama za dola. Na kwa kuwa kawi ni hitajio muhimu kwa usafiri na uzalishaji, ongezeko la bei za kawi huongeza bei za bidhaa nyingi, na kuifanya hali yetu kuwa mbaya zaidi.

Ili kuhakikisha ulipaji riba wa kujirudiarudia kwa wakoloni haukatizwi, serikali imefanya kazi na IMF kutekeleza ongezeko la utozaji ushuru na kuondoa ruzuku, ikiongeza gharama za bidhaa nyingi muhimu. Inatoza ushuru kikatili juu ya mafuta kufikia hadi hata kushuka kwa bei za mafuta kimataifa hakukupunguza bei ya mafuta. Imetekeleza utozaji ushuru wa kidhuluma wa kirasilimali kwa kila mtu, ovyoovyo, bila ya kuzingatia uwezo wetu wa kushibisha mahitaji yetu msingi. Hivyo basi imeunyonga uchumi wetu hadi kukosa uhai, mpaka masoko yetu yamekuwa matupu, viwanda vyetu kufungwa, biashara zetu kuporomoka na vijana wetu kuzurura mitaani, macho yakiwakodoka kwa msongo wa mawazo, pasi na ajira ya maana kupatikana popote.  

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Kiburi cha kutojali wingi wa kuteseka kwetu, utawala usiokuwa na ruwaza wa Bajwa-Imran una nia ya kunyakua mpaka tonge la mwisho la chakula midomoni mwa watoto wetu, ili kuhakikisha tu ulipaji wa madeni ya riba kwa taasisi za kifedha za wakoloni, zinazozingira kama tai juu ya uchumi wetu unaokufa, kuendeleza mikopo ya riba mmoja baada mwingine kurefusha na kuongeza mateso yetu. Ni dhahiri, hatuwezi kufanikiwa, si hapa Duniani wala Akhera, ikiwa tunatawaliwa na watawala wanaopuza muongozo wa Mwenyezi Mungu (swt).  

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَمَنۡ اَعۡرَضَ عَنۡ ذِكۡرِىۡ فَاِنَّ لَـهٗ مَعِيۡشَةً ضَنۡكًا وَّنَحۡشُرُهٗ يَوۡمَ الۡقِيٰمَةِ اَعۡمٰى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Ta-Ha 20: 124].

Kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiko kutakako makinisha pesa imara juu ya nidhamu ya dhahabu na fedha, na kutatua tatizo la mfumko wa bei katika mzizi wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliidhinisha Dinar ya dhahabu, yenye uzani wa gramu 4.25, pamoja na Dirham ya fedha, yenye uzani wa gramu 2.975, kama pesa, na sheria imezifungamanisha hukmu za kifedha kwa dhahabu na fedha, kama vile Diyah na Nisab ya Zaka. Pesa zinazotegemezwa kwa dhahabu na fedha hutoa thamani ya kindani ya pesa, na kuzipa ustawi. Ni Khilafah pekee ndio itakayo makinisha pesa kwa msingi wa dhahabu na fedha, kujenga hifadhi za dhahabu na fedha, kutumia miamala ya ubadilishanaji bidhaa kwa bidhaa ili kuhifadhi akiba na kusisitiza kuwa dhahabu na fedha zitumiwe kama msingi wa biashara ya kimataifa, kuvunja udhibiti dhalimu wa pesa za Kimagharibi kwa biashara ya kimataifa.   

Mtawala anaye tawala kwa Qur'an na Sunnah pekee, atatekeleza hukmu ya Kiislamu ya kawi na madini, ambayo ni kuwa ni mali ya umma, inayosimamiwa na dola ili kuhakikisha manufaa yake yote ni kwa ajili yetu sote, na sio kwa wachache wetu, kama inavyotokea katika ubinafsishaji. Atafanya hivyo kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika juu ya vitu vitatu, maji, malisho na moto (kawi).” (Ahmad). Hakika, ardhi yetu imebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa mali tele za umma, ikiwemo makaa ya mawe, gesi, kawi ya jua, mafuta, dhahabu na shaba, ambazo zitatuwezesha kusimama imara kwa miguu yetu wenyewe, bila ya madhara yasiyokwisha ya mikopo ya riba.

Katika Dini yetu tukufu, mapato huzalishwa kutoka kwa wale miongoni mwetu walio na uwezo wa kifedha, kama vile Zakah kutoka kwa wale wanaomiliki bidhaa za biashara zilizo juu ya Nisab na Kharaj kutoka kwa wale wanaomiliki ardhi ya ukulima, huku mapato yakigawanywa kwa masikini wetu na walio na madeni. Kwa hivyo, kuhukumu kwa Uislamu kutainua mapato pasi na kutunyonga hadi kutukosesha uhai, kuhakikisha uchumi unaokua kwa nguvu, kama ilivyo kuwa karne kadhaa zilizopita, kiasi ya kuwa bara dogo la India chini ya Uislamu lilikuwa na hisa ya asilimia 23 ya uchumi wa ulimwengu, likifikia kilele cha asilimia 27 wakati wa zama za Aurungzeb Alamgir.

Na, Uislamu umeharamisha kuchukua mikopo kutoka kwa wakoloni. Sio kwa sababu tu mikopo hiyo ina riba pekee, bali pia mikopo hiyo huwaruhusu makafiri kuwa na ubabe juu ya mambo yetu, na kutusababishia madhara makubwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema,

  «لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ» “Hakuna kudhuru wala kudhuriwa.” [Muwatta Imam Malik, Ibn Majah]

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Hebu natumalizeni mateso yetu mikononi mwa uongozi usiokuwa na ruwaza, kupitia kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kulingania Khilafah kwa njia ya Utume. Na hebu tuwatakeni masimba wetu katika wanajeshi kutoa Nusra kwa Hizb ut Tahrir, chini ya Amiri wake, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, ili utekelezaji wa kivitendo wa Uislamu uanze. Ni wakati huo pekee ambapo, tutafurahia uongozi unaolinda mali, ardhi, maisha na heshima zetu kupitia Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

H. 20 Jumada I 1441
M. : Ijumaa, 14 Februari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu