Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mkurupuko wa Ugonjwa wa Korona (Covid-19) Umedhihirisha Kheri katika Waislamu na Mapuuza kwa Watawala

Kama ilivyo katika kila mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), iwe ni tetemeko la ardhi au mafuriko, Waislamu watukufu wa Pakistan waliitikia kwa subra na upole mtihani wa mkurupuko wa virusi vya Korona (Covid-19).

Licha ya machafuko na usumbufu, wengi walijitahidi kuzuilia madhara yasiisibu jamii ya Waislamu kwa kutumia njia yoyote wanayoijua. Na hivi ni kutenda sambamba na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipo sema,

«لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ»

Kusiwe na madhara wala kudhuruiana.” (Ibn Majah)

Kinyume na ubinafsi, ununuzi wa bidhaa kwa hofu eneo la Magharibi wakati wa mkurupuko, Waislamu nchini Pakistan walikuwa wakijali wenzao wakati wa ununuzi wao, na hata kutumia mali zao na wakati wao katika kusaidia mafukara na walio dhaifu. Na hii ilikuwa sambamba na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipo sema,

«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ»

“Yeyote atakaye msaidia Muislamu tatizo kutokana na matatizo ya ulimwengu, Mwenyezi Mungu atamuondolea tatizo kutokana na matatizo ya Siku ya Kiyama.” [Tirmidhi].

Kupitia uvumilivu, Dua na mbinu za kivitendo, Waislamu wa Pakistan wamethibisha kheri yao mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«عِظَمُ الْجَزَاءِ مَعَ عِظَمِ الْبَلاَءِ وَإِنَّ اللَّهَ إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاَهُمْ فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا وَمَنْسَخِطَ فَلَهُ السُّخْطُ»

“Ujira mkubwa zaidi unakuja na mitihani migumu zaidi. Pindi Mwenyezi Mungu anapowapenda watu, huwaonja (huwajaribu) yeyote atakaye ridhia moyoni mwake atafaulu radhi za Mwenyezi Mungu na yeyote atakayechukia moyoni mwake atapata hasira za mwenyezi Mungu.” [Ibn majah]

Kwa kushikamana kwao imara na Uislamu, kunatafautiana kukubwa kulioje kati yao na watawala wa Pakistan, kwa kutawala kwao na sheria zisizokuwa zile alizoziteremsha Mwenyezi Mungu (swt)! Badala ya kuwaondolea matatizo Waislamu katika wakati huu wa mitihani, viongozi wanawaongezea madhila Waislamu kinyume na maamrisho wazi ya Uislamu.

Hivyo, ni hata baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuamrisha,                              

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلَا تَدْخُلُوهَا وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا مِنْهَا»

Mtakapo sikia kuzuka ugonjwa wa kusambaa katika mji fulani, msiuingie na kama itatokea katika mji mliopo, msiutoke” [Bukhari], watawala waliwaweka wale waliorudi kutoka Iran wakiwa na maradhi haya katika sehemu moja na wale waliorudi wakiwa hawana maradhi. Kisha wakawaachilia wote pamoja kwenda majumbani mwao kote nchini Pakistan, hivyo kuongeza kusambaa kwa maambukizi ya virusi hivi ndani ya Baluchistan, Punjab na Sindh.

Licha ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«لاَ تُورِدُوا المُمْرِضَ عَلَى المُصِحِّ»

msiwachanganye walio ambukizwa na walio wazima” [Bukhari], watawala waliwachanganya pamoja walio ambukizwa na walio wazima, ndani ya vituo vya karantini vilivyo mpakani na katika hospitali zilizo mikoani, wakiruhusu kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa walioathirika hadi kwa waliowazima. Watawala walishindwa hata kupeana vifaa na mavazi mwafaka ya kujilinda (PPE) kwa madaktari na wauguzi jasiri, licha ya kuwa inajulikana kwamba virusi vya Korona hunawiri vyema katika viyeyuzi vinavyo patikana katika mazingira ya hosipitali. Walifanya hivyo huku wakidai kuwataka watu wadumishe masafa salama ya kijamii nje ya hospitali!

Na licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,    

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِنْ كُنتُمْ مُؤْمِنِينَ -فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ]

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni waumini, basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Watawala wa Pakistan wamedumu na malipo ya riba, ambayo kwa sasa yanakula sehemu kubwa ya bajeti, licha ya kuwa watu wanateseka kwa athari mbaya za utumiaji wa kiwango cha chini cha pesa katika mfumo wa afya. Badala ya kukomesha malipo ya riba juu ya msingi kwamba kuna udharura wa kitaifa na ni kinyume na Dini, watawala wanakubaliana na IMF kuongeza mikopo na kuruhusu utoaji wa bondi za mikopo ya hazina, yote kwa msingi wa riba.

Na kwa msaada wa mfuko wa kiuchumi uliotangazwa na serikali, baada ya kulazimisha marufuku ya kutotoka nje (lock-down) kwa umma, bila ya juhudi zozote za kuwatenga walio wazima na walioathirika, si chochote ila ni upofu wa kuiga serikali za Kimagharibi, ambazo zinajaribu kuhimili kuanguka kwa mfumo wa urasilimali, ambao kwa mara nyengine tena umedhihirisha kuwa tete katika kukabiliana na changamoto mpya.

Hivyo, hata katika wakati wa mtihani wa mkurupuko wa Covid-19, watawala madhalimu wa Pakistan wanapanga kuzindua mateso ya kujitengenezea ya malipo zaidi ya riba na kudhoofisha zaidi rupee kupitia uchapishaji wa pesa zaidi, hivyo kutoa mwanya wa kudhoofisha zaidi mfumko wa bei kutokana na kudhoofika kwa Rupee. Na hili litasababisha ushuru zaidi ili kulipa riba, baada ya janga la Korona kuisha. Kwa kuendelea kukiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), watawala wa Pakistan wamethibitisha kauli Yake (swt),

 [وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكً]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki…” [Surah Taha 20:124)

Na kuongeza katika mapuuza yao, watawala hawa wamewanyima Waislamu haki ya kuabudu ndani ya Misikiti, hata pamoja na tahadhari, ili Waislamu waombe Msamaha na Usaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za Uislamu kuhusu kutekelezaji wa swala Misikitini, ambayo hutangaza swala ya jamaa Miskitini, kama Fardh Kifaya (Faradhi ya kutoshelezana)

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Kama vile fimbo ya Musa (as) ilivyo weka wazi udanganyifu wa wachawi wa Fir’aun, nidhamu tete za utawala zilizo undwa na wanadamu zimefichuliwa na kiumbe kidogo zaidi ya viumbe vya Mwenyezi Mungu (swt), kirusi cha Korona, ambacho kinaweza kuonekaniwa kupitia usaidizi wa darubini ya kielektroni pekee. Ni mripuko wa ugonjwa yake umefichua kushindwa kukubwa kwa Urasilimali pamoja na nidhamu yake ya tawala, Demokrasia, katika kuangalia hali ya afya na uchumi wa watu, si Pakistan pekee bali ulimwengu mzima.

Kwa kweli, kwa mojawapo ya viumbe Vyake (swt) vidogo zaidi, Mola wa Walimwengu (swt) ameonesha watu wote wanaoishi katika Dunia Yake (swt), kwamba nidhamu ya Demokrasia iliyo tengenezwa na wanadamu ni dhaifu, isiyo wajibika na isiyofaa kuangalia mambo yao na imepitwa na wakati.

Nidhamu hii iliyo feli ya Demokrasia, lazima ing’olewe kwa haraka na ubadilishwe na Khilafah kwa Njia ya Utume, ili uangalizi wa makinifu na wa kivitendo wa mambo ya Waislamu wazuri, watukufu na walionyoka wa Pakistan ufanyike kupitia Dini ya Haki, bila hasara zaidi kwa uhai na mali.

Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) ametupa nafasi adhimu ya kuiregesha Khilafah kwa Njia ya Utume ndani ya Pakistan. Kwa sasa inaweza kutabikishwa bila ya mvutano wala upinzani mkubwa, kwani janga la virusi vya Korona limezishughulisha dola za maadui za kikoloni katika kuzuia dhidi ya kuanguka kwa uchumi wao, pamoja na mmomonyoko mkubwa wa imani ya ummah, uaminifu na ushirikiano.

Hivyo, tunapo kimbilia kuukaribisha mwezi ulio barikiwa wa Ramadhan, tufanye kazi bila kuchoka kumaliza utawala dhalimu na kurudisha utawala kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wake (saw). Hakika, ulimwengu uko zaidi ya kuwa tayari kutupilia mbali mzigo wa Demokrasia iliyo tungwa na wanadamu na unasubiri kunyanyuka kwa Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

 “Nyinyi mmekuwa bora ya Umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini mwenyezi Mungu. [Surah al Imran 3:110]

#Covid19     #Korona    كورونا#

H. 7 Sha'aban 1441
M. : Jumanne, 31 Machi 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu