Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mamlaka ya Palestina kupitia Maamuzi Yake ya Kidhulma Yanatishia Amani ya Raia na Kutaka Kuangamiza Jamii na Kufukarisha Watu na Kuwatumbukiza katika Haramu
(Imetafsiriwa)

Tangu kuanzishwa kwake, Mamlaka ya Palestina (PA) imekuwa ikifanya kazi kwa uovu, hofu na vitisho ili kuwatiisha watu wa Palestina na kuwafanya kuwa windo rahisi kwa maadui zao. Mara hufinika uhalifu wake kwa sheria na mara nyingine hupuuza sheria. Lengo lake ni kutekeleza mipango ya wakoloni, ambayo muhimu zaidi ni kuwaondoa watu wa ardhi iliyobarikiwa kutoka kwa Dini yao. Ni sera ya muda mrefu inayolenga kulipa nguvu umbile la Kiyahudi, kulilinda na kuimarisha uwepo wake sio tu nchini Palestina, bali pia kuwa na matawi yaliyopanuliwa katika nchi za Kiislamu.

Watu wa Palestina wameteseka na mazungumzo ya kujisalimisha ya PA na janga, maafa na kupuuzwa kwa ardhi na matukufu, na mradi wake wa "kitaifa" ambao ulibadilika kutoka kuwa ni mradi wa ukombozi kutokana na uvamizi hadi kuwa ni chombo cha usalama cha kutumikia uvamizi huo, na hadi kuwa ni mradi wa uwekezaji kwa viongozi wake ambao wanajali tu kudhibiti marupurupu na kuimarisha uwekezaji wao.

Mamlaka ya Palestina imekuwa ni chombo madhubuti cha maadui zetu katika kuua uthabiti wa watu wa Palestina. Utiaji saini wake muovu wa makubaliano ya CEDAW hauna lengo lolote zaidi ya kuvunja familia na kuzipa nguvu nchi za Magharibi juu ya wanawake na watoto wetu. Fahamu ya jinsia imekuuzwa katika taasisi zote, mihadhara na semina zinafanyika kwa ajili yake, na PA imeanzisha mitaala ya elimu, ili kuwafanya watoto wetu wajifunze kuwa kitambulisho cha kijinsia hakijawekwa kwa kuzaliwa. Badala yake, huathiriwa na mambo ya kisaikolojia na kijamii, na hubadilika na kupanuka chini ya ushawishi wa mambo ya kijamii. Mwanamume kuhisi kwamba yeye ni mwanamke ni hisia ya kimaumbile ambayo lazima iheshimiwe, na mivuto ya mwanamke kwa mwanamke kama yeye, ni mivito ya kimaumbile ambayo lazima ilindwe. Wanadai kuwa ushoga na usagaji ni haki za mtu binafsi ambazo lazima zilindwe. PA imeunda taasisi na vilabu vya mashoga ambavyo vinalindwa na vyombo vyake vya usalama, na mawaziri kwenye PA huwatetea, je huu ni uhalifu wa aina gani? Vyombo vyake vya usalama, na mawaziri walioko madarakani wanautetea, hivi huu ni uhalifu wa aina gani hili?!

Je, kudumisha na kutunza jamii kunahusisha kueneza ushoga na kuulinda?!

Kisha PA akasubutu kuwashambulia watu na kuendeleza uhalifu wake dhidi yao kwa kutunga sheria kadhaa chini ya jina la "uamuzi wa sheria", zinazolenga nyanja zote za maisha ili kuimarisha ukusanyaji wa kodi, na kunyonya damu yenu na kutabikisha sera za maadui zenu.

Kwa hivyo, PA imekula njama dhidi ya uwezo wa wafanyikazi na ada zao ili kupata uungaji mkono wao juu yao kupitia Sheria ya Hifadhi ya Jamii, na vile vile kuhusu mishahara ya majengo ambayo ndio mada ya mizozo ya haki za binadamu kati ya watu na ada anazozilazimisha, kisha marekebisho ya sheria ya kodi, ikiwa ni pamoja na kodi ya maarifa 7% juu ya kodi halisi ya majengo, ambayo sio kodi ya mali, mapato na kodi ya ziada. Kiwango cha uporaji wa pesa za watu ni aina ya kuwadhulumu na kuwasukuma kuuza mali zao. Kisha zikaja sheria za "uuwaji, taratibu za kiraia na za kuadhibu" na nyingine nyingi. Sheria hizo za kidhalimu ambazo zitaathiri amani ya raia na kuwasukuma watu kuchukua haki zao mikononi mwao, na kusababisha machafuko na mashambulizi ya mali na damu, na kupelekea jamii kuzongwa na mizozo kuzidi ndani yake. Zaidi ya hayo, imetungwa kwa uangalifu mkubwa ili kuwasukuma watu kwenye benki za riba ili wasakamwe na madeni na kuzama kwenye kinamasi cha haramu na katika vita na Mwenyezi Mungu (swt) ambavyo hawataviweza.

Kwa uamuzi wa dhulma, takriban dunum 73 za ardhi ya wakfu ya swahaba mtukufu Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, zilinyang'anywa ili ziwe chini ya milki ya Kanisa la Al-Maskobiya (Kanisa la Urusi). kwa ajili ya maandalizi ya uingizwaji wake kwa umbile la Kiyahudi, kama ilivyotokea katika baadhi ya mali za kanisa ambazo ziliingizwa kwa walowezi, na PA bado inatafuta kupitia kwa mkuu wa Baraza la Mahakama "Abu Sharar" ili kukwepa uamuzi wa mahakama uliotolewa na Mahakama ya Upeo ikibatilisha uamuzi wa kunyang'anywa mali. Hivyo, kwa nini msisitizo huu kwa upande wa PA kuhamisha umiliki wa ardhi ya wakfu iliyotolewa wakfu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?

Na kwa uamuzi wenye uadui kwa Ummah, sheria ya “Ulinzi wa Mtoto” ilitungwa, ambayo haikuwa ya kuwalinda watoto wenu kutokana na uhalifu wa uvamizi, wala kuwalinda na mashambulizi ya Magharibi ambayo yanalenga kuwatenganisha na Dini yao. Badala yake, sheria hii ilikuja kwa kutekeleza wa maagizo ya nchi wafadhili za Ulaya, kuwanyang'anya ulezi wenu wa watoto na familia zenu ili wawe mawindo rahisi kwa maadili ya Kimagharibi, na chombo mikononi mwa maaadui zenu.

Sheria ya Ulinzi wa Mtoto humpa haki mtoto kuchagua Dini yake, mavazi yake, na kuamua mwelekeo wake wa kijinsia kando na familia yake na maadili yanayoiongoza. Sheria hii inampa haki ya kuamua mwelekeo wake wa kijinsia na haimpi haki ya kuoa hadi afikishe umri wa miaka 18. Ni ipi nia ya hili? Inaufanya uitiaji adabu wa baba kwa mtoto wake wa kiume au utiaji adabu wa mwalimu kwa mwanafunzi wake kuwa kosa la unyanyasaji, na kumlazimisha msichana kuvaa mavazi ya Kiislamu kuwa ni uhalifu wa ubaguzi na unyanyasaji, je, huu sio uangamizi wa watoto na familia zetu?

Hawataki muwafundishe watoto wenu kuhusu swala na adabu za Uislamu, kwa sababu kwa kufuata kauli hii ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

»مُرُوا أَبْنَاءَكُمْ ‌بِالصَّلَاةِ ‌لِسَبْعِ سِنِينَ، وَاضْرِبُوهُمْ عَلَيْهَا لِعَشْرِ سِنِينَ، وَفَرِّقُوا بَيْنَهُمْ فِي الْمَضَاجِعِ«

Waamrisheni Watoto wenu kuswali wakiwa na umri wa miaka saba, na wapigeni (kwa kutoswali) wakiwa na umri wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi”. [Imesimuliwa na Ahmad]

Huu ni uhalifu unaostahili kuadhibiwa chini ya “Sheria ya Ulinzi wa Watoto”!

Haya yote yanathibitisha kwamba msingi wa Mamlaka ya Palestina ni uharibifu wa jamii na wizi wa pesa za watu, sio ulinzi wa haki zao. Lau msingi ungekuwa utunzaji na ulinzi wa haki za watu, ingefanya kazi ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa fedha uliokithiri katika taasisi zake zenye ushahidi mwingi, baadhi yao wana mafaili ya wazi, hasa mafaili ya wanaovujisha ardhi kwa umbile la Kiyahudi, na dori ya huduma za usalama katika hilo.

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Maamuzi ya PA yamekuwa chombo cha kubomoa jamii, mpasuko wake na kupoteza maadili yake, jambo linalolazimu kazi ya kuikomesha PA kufanya maamuzi haya, na kuihisabu kwa makosa yake. Na kwamba kukataa njia hii ya kiburi iwe waziwazi. Kulinda ardhi yenu, familia zenu, watoto wenu na pesa zenu kwa hitaji kusimama kidete kwa nguvu katika kukataa maamuzi yake yote ya kihalifu na kufanya kazi ya kuyafutilia mbali na kuyabatilisha.

Suala hili linahusiana na hatima yenu nyote. Vyombo vya usalama vinataka kuwakamata watoto wenu na kuwaweka kizuizini bila kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili kuwanyanyasa na kuwatesa katika majengo yake, kuvunja utashi wenu na kuwalazimishia mazingira ya hofu, yanayowawezesha viongozi wa PA na wale walio nyuma yao kuwasagasaga bila mtu yeyote kuwazuia. Kwa hiyo, tunawalingania mukabiliane na utawala wa PA, la sivyo utakuleteeni hatari na utakuvisheni vazi la aibu na hasara.

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Ikiwa nembo za PA zinazungumzia juu ya sheria na ubwana wake, basi kinachofanywa na PA ikiwakilishwa na rais wake, serikali na viongozi wa vyombo vyake vya usalama ni uhalifu kamili, na pamoja na maamuzi yake haituhumiwi kwa upuuzi au udikteta, bali imefanya uhaini wa hali ya juu kupitia kuratibu usalama unaoratibu pamoja na uvamizi huo, na kutabanni sera za maadui zenu na kushirikiana nao ili kukuangamizeni na kukufanyeni mupoteze uwezo wa kusimama kidete. Malengo ya sera na maamuzi yake yako wazi kama jua la mchana. Wanalenga kukuangamizeni, kuua ari yenu ya uasi inayokataa miradi ya kikoloni, kumaliza matamanio yenu ya Kiislamu na kuwatenganisha na Dini yenu na Ummah wenu, ili kurefusha uvamizi huu na kuuwezesha kuiguguna nchi na kupanua makaazi.

Kwa kumalizia: Tunatoa wito kwa watu wote wa ardhi iliyobarikiwa, koo, watu mashuhuri, vyama na makundi, wanaume na wanawake, vijana kwa wazee, kusimama imara mbele ya udhibiti wa PA. Tunasisitiza haja ya msimamo wa pamoja ili kukomesha maamuzi ya kidhalimu ya PA na kuyafutilia mbali yote, na sio kujadiliana au kujadili marekebisho rasmi kwao. Kwa sababu sheria hizi zitakuwa ni balaa kwenu na kwa familia zenu na maangamizi kwa ajili yenu, na kwa fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu, Hizb ut Tahrir itabaki pamoja nanyi na baina yenu, ikisimamia haki, ikimkabili kila anayeitakia Dini yetu na Ummah wetu shari na uovu.

Hatimaye: udumishaji wa jamii na kupatikana kwa ustawi na utulivu kwa wanajamii wake, kunaweza tu kupatikana kupitia hukmu za Uislamu na kupitia uongozi mwema wenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kwa msaada na mafanikio ya Mwenyezi Mungu (swt), tutausimamisha kama Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Tutaifanya dunia ishuhudie heshima na uadilifu utakaowafanya watu kuingia katika Uislamu makundi kwa makundi. Nusra ya Mwenyezi Mungu iko karibu.

(وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ ‌مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ)

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. [Ash-Shu’ara: 227]

H. 7 Muharram 1444
M. : Ijumaa, 05 Agosti 2022

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu