Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa kwa Khilafah Palestina itakombolewa na Khilafah, kwa hiyo Uhamasisheni Ummah na Majeshi yake Kuisimamisha
(Imetafsiriwa)

Kila siku, umbile la Kiyahudi linakoleza dhulma yake, ukosefu wa adili, na uonevu. Kumwaga damu tukufu asubuhi na jioni, kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa kila siku, na kuzuia harakati ndani yake hata mbele ya wamiliki wa uwongo wa “usimamizi wa Hashemiya”. Ndege zake zavamia Ukanda wa Gaza. Serikali ya Netanyahu inatoa wito wa kunyakuliwa kwa kile kilichosalia cha ardhi. Yote haya yanafanywa bila kizuizi. Hii ni kwa sababu Mamlaka haini ya Palestina ingali inaning'inia kwenye mangati ya madai ya amani, na mradi wa Utatuzi wa serikali mbili wa Marekani, na ingali ni mwaminifu kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.

Ama tawala za vibaraka zinazoshirikiana, ziliufunga Ummah minyororo kutokana na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Bali, walikula njama, kuhalalisha mahusiano, na kushutumu ushujaa wa watu wa Palestina.

Enyi Watu Wetu Katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina: Nyinyi ni kizazi cha washindi na wakombozi, nyinyi ni kizazi cha Umar, Salah ud-Din, al-Dhahir Baybars na Sultan Abdul-Hamid, hivyo kuweni wastahiki kuaminiwa na hifadhini Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na kupotea, achaneni na mikataba ya kisaliti iliyotiwa saini na Jumuiya ya Ukombozi na tawala za wasaliti kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ikanyageni miradi ya kimataifa, ukiwemo mradi wa suluhisho la dola mbili wa Marekani ambao unaipa sehemu kubwa ya Palestina kwa wavamizi. Jueni kwamba kwa ulinzi wenu, ukakamavu wenu, na kushikamana na Ummah wenu na kutokuwa na hatia kwenu kwa makhaini kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mutakuwa mwenge unaoyasukuma majeshi ya Kiislamu kuling'oa umbile la Kiyahudi na kuitakasa Masra (eneo la Isra) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kutoka kwenye makucha ya wavamizi.

Enyi Mujahidina katika Ardhi Tukufu ya Palestina:

Hii ni nasaha tunayokupeni, basi zifungueni nyoyo na akili zenu, jihadharini na utegemezi kwa wasaliti na wapatanishi wao, hao ni washirika wa Mayahudi katika uvamizi na jinai zao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ]

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa. [Hud: 113].

Na jueni kwamba ushujaa wa mtu binafsi pekee hautoshi kukomesha jinai za umbile la Kiyahudi, kwani jinai za ukaliaji kwa mabavu hazimaliziki isipokuwa kwa kuangamia kwake, na hili lahitaji kuhamasishwa mara kwa mara kwa nguvu za Umma, hususan majeshi, ili kuwanusuru watu waheshimiwa wa Palestina pamoja na Dini yao.

Kadhia ya Palestina ni kadhia ya Ummah, na kheri hii lazima ifasiriwe katika hotuba zenu, basi hutubieni Umma na majeshi yake kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ]

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. [At-Tawba: 38].

Ili wasonge, kwa kusukumwa na Taqwa (uchamungu) na wajibu, kuchukua uamuzi wa vita na jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa na viunga vyake.

Enyi Waislamu: Ardhi Iliyobarikiwa itabakia kuwa mwiba katika upande wa Mayahudi, Marekani, wakoloni na wenye kuhalalisha mahusiano kwa jumla, na hakuna mkoloni wala mhaini atakayetulia humo.

[وَلَقَدْ كَتَبْنَا ‌فِي ‌الزَّبُورِ مِنْ بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ]

“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.” [Al-Anbiya: 105]

na jueni kwamba Palestina ilipotea siku ile Khilafah ilipovunjwa, ambayo tunaishi katika kumbukumbu ya kuvunjwa kwake leo. Kwa hiyo, enyi Waislamu, tunakulinganieni kwenye kazi nzito kwa ajili yake, ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na kuwanusuru wafanyao kazi kwa ajili yake. Ni kwa Mwenyezi Mungu, izza na njia ya kuwaokoa wanadamu, basi itikieni mwito wa Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنْصَارَ اللَّهِ]

Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu [As-Saf: 14]

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ ‌يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

H. 26 Rajab 1444
M. : Ijumaa, 17 Februari 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu