Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mpaka Lini, Enyi Ummah wa Muhammad?!
(Imetafsiriwa)

Uharibifu na kukatwa vipande vipande, kulipuliwa kwa mabomu na mauaji makubwa, kunajisiwa Msikiti wa Al-Aqsa na kumtukana Mtume (saw) ndani ya nyua zake. Hivi, mpaka lini, enyi Umma wa Muhammad (saw)?!

Kwa muda wa miezi saba tumekuwa tukiulingania Ummah wetu na majeshi yake kwa ajili ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, tukiwalingania kwa wito wa Mwenyezi Mungu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawba:38-39]. Hivi, mpaka lini, enyi Ummah wa Islam?!

Je, sio wakati wa nyinyi kuzipindua tawala za khiyana na watawala vibaraka? Je, maneno yao matupu hayakukasirishi, ambayo kwayo wanamwita adui wa Kiyahudi kuzingatia sheria na maazimio ya kimataifa? Je, ni sheria na maazimio gani wasaliti hawa wanazozungumzia? Kwa muda wa miezi saba wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu (Mayahudi) wamekuwa wakiwaua watoto, wanawake, wagonjwa na wafungwa, wakiharibu hospitali, misikiti na taasisi za elimu. Wamelenga hata mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada, wakiua wanachama wao na kuharibu makao yao makuu. Ni kipi kimesalia kutoka kwa sheria za kimataifa ambacho hawajakiuka? Ni matukufu gani yanayobakia ambayo hawajayachafua?

Enyi Umma wa Muhammad (saw): Damu yetu inamwagwa kwa kiasi kikubwa, na kwa upande wake, Marekani na vibaraka wake wanazungumza kuhusu misaada ya kibinadamu, suluhisho la dola mbili, na uhalalishaji mahusinao na wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu. Je, kuna uhalifu mkubwa kuliko huu?! Wanatuma misaada pamoja na mabomu ya kifo, wanazungumza kuhusu amani na uhalalishaji mahusiano huku wakiendelea na mauaji na uharibifu wao. Na sasa, kundi la wasaliti la watawala vibaraka nchini Misri, Jordan, Qatar, na ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu wanashirikiana na Marekani kwa ajili ya mipangilio ya baada ya vita, mipangilio hiyo inayolenga kurekebisha sura ya dola halifu na inayokalia kimabavu, kuiunganisha katika eneo hilo, na kuzima kadhia ya Palestina.

Enyi Waislamu: Uthabiti na ushujaa wa mujahidina unakulazimuni kuwanusuru kikweli, na hivyo kupelekea kukombolewa kwa Ardhi Iliyobarikiwa na Msikiti wa Al-Aqsa. Hata hivyo, watawala vibaraka na mashirika yao ya kijasusi wanafanya kazi kwa nguvu zao zote kubadilisha ushujaa wa mujahidina na damu na mateso kuwa kushindwa kukubwa kuliko kule kwa 1948 na kikwazo kibaya zaidi kuliko kile cha 1967. Ushujaa wa jeshi la Misri katika Ramadhan 1973 ilihujumiwa na makubaliano ya amani ya khiyana yaliyotiwa saini na Sadat, ambayo watu wa Misri na Palestina bado wanateseka nayo.

Kile ambacho Marekani, Mayahudi na watawala vibaraka wanapanga dhidi ya watu wa Palestina ni njama kubwa. Vipaumbele vyao vya sasa ni kuwaondoa mujahidina na hamasa ya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kuanzisha mamlaka katika Gaza ambayo inayofanya uratibu pamoja na Uvamizi sawa na chombo cha Mamlaka ya Palestina mjini Ramallah. Wale waliopata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu wanapiga dau juu ya fursa, na uhalisia wao umeelezwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[أَمْ لَهُمْ ‌نَصِيبٌ ‌مِنَ الْمُلْكِ فَإِذاً لَا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيراً] “Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.” [An-Nisa:53]. Wanataka Palestina yote, na macho yao yatulizwa kwenye ardhi vilevile. Ama kuhusu mradi wa Marekani wa suluhisho la dola mbili, umekosa maana.

Enyi Umma wa Muhammad (saw): Matukio ya Gaza yameamsha fahamu ya ukombozi na faradhi ya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kujenga hisia ya jumla kwa Waislamu kwamba ukombozi wa Masra ya Mtume (saw) uko karibu zaidi kuliko wakati mwengine wowote. Hata hivyo, Marekani na watawala vibaraka wanataka kuupotoa Umma wa Kiislamu kutoka katika ukombozi na jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kupigia debe suluhisho la dola mbili na kuuonyesha Umma wa Kiislamu kuwa ni dhaifu na usio na nguvu, ambao lazima ujisalimishe na kusalimu amri kwa matakwa ya Marekani na umbile la Kiyahudi.

Usaliti wa tawala hizo utawatumbukiza Waislamu katika dimbwi la njama, udhalilifu na ukandamizaji. Hili linawalazimu Waislamu kwa jumla na hasa majeshi kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kujinasua kutoka katika utegemezi na uwakala, kuzipindua tawala, kuondoa mipaka ya Sykes-Picot, na kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu duniani.

Ewe Umma Bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu: Jukumu la Umma wa Kiislamu kwa ulimwengu ni kubwa sana. Inaulazimu Ummah kusimama kwa ajili ya Dini yake kama alivyokusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuwa shahidi kwa watu, shahidi kwao ukisimamisha Dini na kupiga vita dhulma na jeuri.

Hakika ni wakati wa sisi kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhulma hii halifu ya kibepari. Harakati ya uhamasishaji inayoshuhudiwa hivi sasa ulimwenguni ni ishara ya matumaini kwa wanadamu wote. Wanafunzi hawa walikua wakitukuza uhuru na kuuzingatia kuwa ni dhihirisho la ukuu wa Marekani, lakini sasa wako kwenye mgongano na dola yenye jukumu la kutabikisha mfumo na kudhamini haki yao ya kujieleza. Kukandamiza na kutawanya kwa nguvu vikao ni pigo kwa kanuni msingi za mfumo wa kibepari, na huu ni utangulizi wa kuporomoka kwa Marekani na mifumo ya Kimagharibi.

Muungano wa Kisovieti uliporomoka pale imani katika mfumo wa Kikomunisti na fahamu zake za kimsingi za maisha ilipopotea, na Khilafah iliporomoka pale fahamu za kimsingi za Waislamu zilipopotoshwa, na kusababisha Uislamu kupoteza ushawishi wake kwa serikali na jamii. Hiki ndicho kinachotokea Magharibi sasa. Kinachotokea sio tu kukandamiza uhuru wa mtu binafsi wa kujieleza bali ukandamizaji wa fikra hiyo katika jamii. Haya ni matokeo yasiyoweza kuepukika ya kupoteza imani katika demokrasia kama njia ya maisha na kupoteza imani katika mfumo wa kidemokrasia unaotawala.

Mtegemeeni Mwenyezi Mungu Al-Qawii Al-Aziz na mufanye kazi kwa bidii pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu duniani. Mwenyezi Mungu (swt) ataleta nusrah (ushindi) yake kupitia mikono yenu kwa uwezo wake usioshindika.

[إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللهُ ‌فَلَا ‌غَالِبَ لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aal-i-Imran:160]

Ewe Mwenyezi Mungu, zifungue nyoyo za Waislamu kwenye utiifu Wako, radhi Zako, na nusra ya Dini Yako. Tujaaliye kutoka Kwako mamlaka yenye kunusuru. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

H. 5 Dhu al-Qi'dah 1445
M. : Jumapili, 05 Mei 2024

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu