Jumanne, 01 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kutoka Tunisia hadi Kimbunga cha Al-Aqsa

Mapinduzi ya Umma Yataendelea Hadi Khilafah Isimame na Ukombozi wa Palestina
(Imetafsiriwa)

Leo tunaadhimisha kumbukumbu ya Januari 14, ambayo ilisababisha Mapinduzi ya Umma na kupindua watawala wenye nguvu zaidi katika kanda hii. Ilikuwa fursa ya kihistoria ya kukombolewa kutokana na ushawishi wa Magharibi na ala zake za kindani. Mahitaji ya kimsingi ambayo kwayo watu walijitokeza yalikuwa wazi katika kile kilichojulikana kama kilele cha mapinduzi ya Kiarabu: “Watu wanataka kuipindua serikali.” Pamoja na matwaka haya, watu hawataki machafuko, lakini badala yake wanataka mfumo mbadala kwa serikali za mwanadamu ambazo zimewaacha watu wao bila ya chochote isipokuwa umaskini, dhulma, na ufisadi.

Kile Magharibi ilichokiogopa zaidi kutokana na mapinduzi ya Ummah ni kwamba kanda hii ungeelekea kwenye mabadiliko halisi, yenye natija kwa msingi wa Uislamu. Kwa hivyo, ilikuwa makini katika kuutenga Uislamu kutoka kwa utawala na sheria, haswa baada ya Uislamu kama mfumo na Khilafah kama nidhamu serikali ya OCAVF ikawa ni rai jumla inayoenea katika nchi za Kiislamu, ikiwemo Tunisia.

Hivyo basi, maamuzi ya dola kuu za Kimagharibi katika Mkutano wa Deauville  (uliofanywa mnamo Mei 2011 na ambayo Misri na Tunisia ziliitwa) ulipaswa kuiweka Tunisia chini ya udhibiti wa Magharibi, kama ripoti ya siri iliyovuja kwenye Benki Kuu, iliyotolewa mnamo 2016 , ilivyofichua kwamba sera zote, machaguo ya kiuchumi, na sheria rasimu zilizofuatiwa na serikali za baada ya mapinduzi, ziliainishwa katika kongamano hilo, kama vile uhuru wa benki kuu, makubaliano ya ushirikiano na Muungani wa Ulaya (ELICA), sheria za uwekezaji, na barua rasimu ya kwanza na ya pili ya dhamira ambayo serikali ya Tunisia ilijitolea kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kufuata mageuzi makubwa, ikiwemo ubinafsishaji wa sekta ya umma, yaani kukabidhi taasisi za umma zilizobaki kwa magharibi baada ya rasilimali asili za gesi, mafuta na madini hapo awali kukabidhiwa kampuni za Kimagharibi.

Sera ya utegemezi ambayo serikali za baada ya mapinduzi zilifuata haikuleta chochote isipokuwa mateso na maangamivu, ambayo yaliharakisha kuanguka kwazo. Harakati ya Julai 25, 2021 ilikuja na kukipindua kikundi ambacho kilikuwa kimetawala kwa miaka kumi na kuwahubiria watu kuregesha ufanyaji maamuzi na kuvunja utegemezi, sera za kikoloni, ufisadi, na upendeleo. Walakini, hali ya maisha ya watu ilizidi kuwa mbaya, na foleni za watu mbele ya matanuri ya mikate, maduka ya Magaza na vituo vya petroli zikawa jambo la kawaida. Ama kuhusu ubwana, ulipotea katika vichochoro vya makubaliano na Muungano wa Ulaya, ambapo ilifanya usalama wetu na jeshi, walinzi na polisi, kuwa kwa ajili ya Magharibi na ajenda zake, na kuifanya nchi yetu, Tunisia, kituo cha kuwachagua na kuwachunguza wale wanaovuka Bara la Zamani, wakiwazuia kuhama na kubeba mzigo wa vituo vya hifadhi na matokeo yao. Habari za kuwatupa wapinzani na watu mafisadi magerezani hazikuwakuvutia tena watu au walipata umakini wao baada ya kugundua ukweli mchungu, ambao ni:

Utawala ambao waliasi dhidi yake haujabadilika, hata ingawa nyuso zimebadilika. Magharibi iliweza kuzalisha serikali ile ile, lakini kwa sura mpya ambazo sera zake hazikuwa mbaya zaidi kuliko zile zilizokuwa kabla yao. Hii ni kwa sababu sera zile zinazoitwa mpangilio mpya zinatokana na malalamiko ya mifumo ya zamani ya kibinadamu ambayo inatawala na yasiyokuwa ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na hazijazalisha chochote isipokuwa ugumu na mateso. Badala yake, zimefanya mambo kuwa mabaya zaidi kwa kupandikiza ukataji tamaa nyoyoni mwa watu ili wasifikirie juu ya kuleta mabadiliko au mapinduzi tena dhidi ya mfumo wa "kisasa" wa kisekula, ambao umewaadhibu vikali. Kwa hivyo, uhalisia wa jambo hilo, ni kwamba hakuna tofauti kati ya serikali ambazo zimewadhibiti watu, hata ikiwa maelezo yao yanatofautiana kati ya demokrasia ya kibunge na demokrasia ya kirais.

Mapinduzi yetu hayatafanikiwa isipokuwa yaimarishwe kwa vitu vitatu:

1- Kujihamu nafsi zetu na mradi wa kihadhara unaotokana na itikadi ya Waislamu, ambayo hutukomboa kutokana na utawala wa Magharibi na kufafanua mbadala, njia, na lengo.

2- Uwepo wa uongozi mwaminifu kwa mradi wa Umma na unaofahamu hila za Magharibi, na kuuongoza Ummah kuelekea mabadiliko halisi, yenye natija kwa msingi wa Uislamu.

3- Uwepo wa kikundi cha watu chenye ikhlasi wenye nguvu wenye uwezo wa kulinda na kutetea mradi wa kihadhara ili kuzuia matarajio ya Magharibi dhidi ya ardhi yetu.

Matukio ambayo yameusibu Ummah katika miaka ya hivi karibuni yamethibitisha pasi na shaka kuwa haiwezekani kuikata minyororo ya jamii ya kimataifa, ambayo ndio sababu msingi masaibu haya, isipokuwa kupitia mradi wa kisiasa kwa mizani ya Umma wa Kiislamu, ambao unavuka siasa za bandia, dola za kitaifa, na mipaka ya kitaifa. Ili kwamba Ummah uwe tayari wakati wowote wa kihistoria kuungana chini ya bendera moja, nyuma ya mtawala mmoja, ndani ya dola moja, ambayo ni dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo ndipo Umma na majeshi yake yatakombolewa kutokana naa utawala wa Magharibi na ala zake za ndani, na nguvu za Ummah zitakusanyika, na kuuwezesha kufikia moja ya vipaumbele vyake muhimu: kuinusuru Gaza na kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, kisha kutoka kuijaza dunia kwa uadilifu na haki, baada ya kujazwa na dhulma na ukandamizaji.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُور]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj: 41].

H. 2 Rajab 1445
M. : Jumapili, 14 Januari 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu