Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Katika Nchi Ambayo Inadai Kulinda Haki za Wanawake, Wabebaji Dawah Wanawake wa Hizb ut Tahrir Wanakamatwa kwa sababu Wanafanya Kazi Nje ya Mfumo wa Kisekula!

(Imetafsiriwa)

Mnamo jioni ya Ijumaa, 02/02/2024, mbele ya Msikiti wa Al-Lakhmi katika mji wa Sfax, wanawake wawili kutoka Hizb ut Tahrir walikamatwa katika mazingira ya kusambaza taarifa ya kuinusuru Gaza. Kabla ya hili, kulikuwa na uvamizi katika nyumba ya mmoja wa wanawake mashabaat wa Hizb katika mji wa Hammamet siku ya Ijumaa iliyopita, tarehe 26/01/2024, ambapo jeshi kubwa la polisi liliingia kwa nguvu ndani ya nyumba hiyo bila kibali. Polisi walijaribu kuwakamata wanawake hao na kuwapeleka katika eneo la usalama kwa ajili ya mahojiano, lakini wanawake hao walikataa na kupendelea kwenda eneo la usalama kwa usafiri wao wenyewe, ambako walihojiwa kwa muda mrefu. Baadaye waliachiliwa ili kufika mbele ya mahakama mnamo Jumatatu, 29/01/2024.

- Katika wakati ambapo hatuwezi tena kustahamili kuwasha televisheni na kushuhudia mauaji ya watu wengi yakitokea baada ya karibu miezi minne isiyokoma ya vita visivyo na huruma vya umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, likiungwa mkono na kiongozi wa uovu, Marekani, dhidi ya watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa.

- Katika wakati ambapo watu wamechoka, wakikabiliwa na bumbuwazi na kukosa msaada wa jinsi ya kuwasaidia ndugu zao huku mipaka ya wakoloni ikiwagawa.

- Katika wakati ambapo wanaume wanatembea wakiwa wameinamisha vichwa chini ya uzito wa aibu ya unyonge wao, wakihisi kutokuwa na nguvu mbele ya sauti kuu za wanawake wa Palestina wakiwataka wainuke na kulipiza kisasi dhidi ya wanyakuzi wa ardhi na heshima.

- Katika wakati ambapo Mayahudi wanakiuka utakatifu wa wanawake na mzee wa Kiislamu wa Palestina - anayewakilisha mama yangu na mama yenu - anaamrishwa kuvua nguo yake ili apekuliwe na mikono michafu ya Mayahudi...

Katika wakati huu, wanawake wachanga kutoka Hizb ut Tahrir wanatiwa mbaroni, licha ya majukumu mazito waliyo nayo, kwa juhudi zao za kuukusanya Umma ili kuwanusuru watu wetu wa Gaza na wito kwa majeshi huru ya Ummah kusonga kwenda kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Tangu lini wanawake wakakamatwa na kudhalilishwa katika nchi ya Uislamu na ardhi ya mzaituni?!

Mfumo wa kisekula uliopandikizwa kwa nguvu unawaambia wanawake wa Tunisia: "Mmewezeshwa kisiasa, lakini haki ya kujieleza, ukombozi, fikra na utawala zinapeanwa pale tu wanapokabiliana na kupambana na wanaume. Huu ndio ukomo wa hatua za kisiasa zilizowekwa kwa wanawake nchini Tunisia!" Hata hivyo, lau wanawake watabeba mzigo wa Umma katika nyoyo zao juu ya mzigo wa familia zao na watoto wao, katikati ya uchungu wa kuishi chini ya ukandamizaji wa mfumo wa kibepari, basi hili - kwa mtazamo wa mfumo wa kisekula - ni dhambi kubwa na kikomo kisichopaswa kuvuka!

Hakika, tunazihurumia ala za ukoloni ambazo, huku zikijihusisha na vitendo vya aibu na fedheha, zinadai: "Tulilazimishwa, na hatukutaka hivyo!" Tunawakumbusha kwamba hata makafiri wa Kiquraish, pamoja na ukafiri wao na ujinga wao, walikuwa na hali ya heshima iliyowazuia kuivamia nyumba ya Mtume (saw) wakisema: “Wallahi ni fedheha miongoni mwa Waarabu kusemwa kuwa tumevamia nyumba ya binamu yetu na kukiuka utakatifu wetu wenyewe." Na tunawakumbusha kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللهُ إِنَّ اللهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” [At-Tawba:71].

Vile vile tutaendelea kuwakumbusha kuwa kuunusuru (nusrah) Ummah ni wajibu juu yetu, kwa kufuata kauli ya Mtume wetu Muhammad, Rehema na amani zimshukie:

«مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلاَّ خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلاَّ نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»‏

“Hakuna mtu (Muislamu) yeyote atakayemtelekeza Muislamu mwengine mahali ambapo utukufu wake unavurugwa na heshima yake inadunishwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza mahali hapa anapotaka msaada wake; na hakuna mtu (Muislamu) yeyote ambaye atamnusuru Muislamu mahali ambapo heshima yake inavunjwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu hatamnusuru mahali anapotaka nusra yake.”

H. 25 Rajab 1445
M. : Jumanne, 06 Februari 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu