Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Miaka Tisini na saba ya Kejeli na Hasara
(Imefasiriwa)

Mnamo 28 Rajab 1324 Hijria sawia na 3 Machi 1924 Miladi, bunge lilikutana kwa kikao chao cha pili Ankara saa tisa na dakika ishirini na tano mpaka saa moja kasrobo. Siku hio, mkutano uliisha na maamuzi hatari kwa Ummah wa Kiislamu nao ni kuvunjwa kwa Khilafah. Kejeli ya maamuzi hayo ni kua kulipigwa kura kwa kuenua mikono na si kwa kura ya siri, katika mazingira yaliyojaa khofu, ikaonyesha wote waliopiga kura jambo ambalo lilikua hatari kwa wenye kupinga kuvunjwa kwa Khilafah kwani walikua wapate hatima ile ile ya wale waliopinga kabla ya kikao, nao ni kuuwawa ama kuadhibiwa.

Kwa maamuzi haya, nchi za kikafiri hususan Uingereza kupitia msaada wa wasaliti katika Waarabu na Waturuki wakiongozwa na msaliti Mustafa Kamal, walitekeleza masharti ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza na mkuu wa wawakilishi wao katika mkutano wa Kongamano la Lausanne mwaka 1922, ambalo liliweka masharti manne ili waeze kuipa uhuru Uturuki nayo ni: Kuvunjwa kwa Khilafah, kufukuzwa Khalifah nchini, kutaifisha mali ya Khalifah na kutangaza dola ya kisekula. Hivyo basi, wakafanya kosa kubwa dhidi ya Waislamu, wakavunja Khilafah na Uislamu ukaondolowa kama katiba ya nchi, nidhamu ya maisha na yenye kuhukumu Ummah. Kuhukumu kwa kile alichoteremsha Mwenyezi Mungu kuliondolewa ulimwenguni kote na hukm za Kikafiri zikatawala.

Tangu siku hiyo ya giza, Ummah wa Kiislamu umedhoofika kihali na katika nafasi yake miongoni kwa mataifa, baada ya kuwa Ummah mmoja, dola moja, Waislamu wakawa zaidi ya dola hamsini, na baada ya Waislamu kufungua ardhi zao na kueneza mali yao, nchi zao zikawa ni zenye kulengwa. Khalifah wao alikuwa ndio mlinzi wao, lakini watawala wa Waislamu wakawa ndio maadui zao, wakishindana kuwatumikia Wamagharibi na kushindana kupanga njama ovu dhidi yao. Wamemzidi Abu Raghal katika uhalifu. Hali hii ikawafanya Waislamu jawa na ukhaini, khofu, njaa na maradhi.

Suluhisho katika hali hii imewekwa wazi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Tunapaswa kufanya kazi kuiregesha Khilafah. Hili suluhisho litatufikisha katika kuongoza dunia. Mwenyezi Mungu (swt) aliubariki huu Ummah na mali na kuwafanya bora ya mataifa yote lau wangelikua na Khalifah na dola; utajiri wao uko chini na juu ya ardhi. Ummah huu ulikua wa kwanza kuzalisha mafuta na gesi ambayo Makafiri Wamagharibi wanazitegemea kwenye viwanda vyao na kufanikiwa kwao, kando na hizo ni raslimali za madini na za ukulima katika maeneo ya kimikakati yanayo unganisha mabara matatu na kudhibiti njia za biashara za dunia kupitia milango na njia za maji: Gibraltar, Dardanelles, Bosphorus, na Suez Canal, Bab al-Mandab, na mlango wa Hormuz na mlango wa Malacca ndani ya Asia Kusini mashariki, na zaidi ya haya yote Ummah uko na utajiri wa kifikra na njia ya maisha inayotokamana na bwana wa viumbe vyote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ)

“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu na rehema, na bishara kwa Waislamu” [An-Nahl: 89]

Leo wanaadamu wamegundua kufeli kwa uongozi wa nchi za kirasilimali; wale wanaofahamu kati yao wanatafuta suluhisho na tiba za shida zilizo sababishwa na mfumo huu. Urasilimali umefanya wanaume kuwa watumwa na wanawake kuwa ni bidhaa, inatambua thamani ya kimada tu, nchi zinazo tekeleza nidhamu hii huharibu kila kitu, huvamia dola nyingine kupata mafuta, kuanzisha vita baina ya nchi tofauti ili wapate kuendeleza viwanda vyao vya silaha, wala hazijali watu wangapi wanalala njaa wala watoto wanaokufa!!

Khilafah ndugu zangu ni chimbuko la fahari ya Muislamu na alama ya nguvu na hili lajulikana na wakoloni. Ndio maana Curzon alisema katika Bunge la Uingereza la Wabunge pindi Khilafah ilipovunjwa: “Kadhia ni kuwa Uturuki imetokomezwa na haito inuka tena kwa sababu tumeivunja nguvu yake ya maadili nayo ni Khilafah na Uislamu,” na kwa sababu wanajua hili hawatatosheka na kuvunjwa kwa Khilafah bali wanatumia nguvu zao zote kuzuia kurudi kwake. Wanawapiga vita vikali wanaoifanyia kazi kurudi kwake, na kwa hilo walikasirishwa kwa kuzinduliwa Hizb ut Tahrir miaka sitini iliopita, na kwa sababu chama cha Hizb ut Tahrir kilifanya kadhia yake kubwa ni kufanya kazi kuregesha tena Khilafah. Wamekipiga vita bila huruma, wao na mawakala wao kwa njia zote za uovu, kwa kejeli, vifungo na mateso kufikia kuuwa na kuwatilia simu wanachama wa Hizb ut Tahrir, lakini walifeli kwa yote hayo na chama kimebakia imara kikielekea kwa Mwenyezi Mungu tu.

Mwisho kabisa, walikipiga vita, kwa kutumia uhalifu wa baadhi ya harakati za Kiislamu zilizotangaza khilafah kwa njia isiyokua ya kisheria, na kufanya vitendo vya makosa vya kuua, kuchoma, mashambulio na uharibifu. Wakoloni walipatiliza makosa ya harakati hizi na kuzimulika. Wakatumia fursa hii kuwatishia Waislamu kuwa Khilafah wanayoitaka inafanya makosa ya kihalifu ya ina hii, kufanya watu waichukie Khilafah iliyo sawa. Lakini walifeli wakati huu kama walivyo feli walipotumia mbinu zao za nyuma. Watu wanaielewa Khilafah ya sawa kwa njia ya Utume na wanaweza kutofautisha na Khilafah bandia iliyotangazwa na harakati hizi. Khilafah ya kweli inatambulikana.

Ni mfumo wa kipekee ulioelezwa na Mtume (saw) na makhalifa walioongoka wakaifuata baada yake. Khilafah sio himaya wala ufalme, Jamuhuri, urais wala ubunge, au udikteta au demokrasia, bali inahukumu kwa mpangilio wa Mwenyezi Mungu na sio sheria zilizotungwa na mwanadamu, bali Khilafah ya haki, na viongozi

 

wake ni warithi wa maimamu, Ummah ukihifadhiwa na kupigana nyuma yao… ni Khilafah inayo hifadhi damu na heshima ya Ummah, kuhifadhi mali yao na kutimiza ahadi… Inachkua ahadi ya utiifu kutoka kwa Ummah kwa ridhaa yao, sio kwa kulazimishwa au kwa kutenzwa nguvu. Watu watahamia pale itakaposimama kwa usalama na wala sio kuikimbia kwa khofu.

Ni katika kumbukumbu ya hili tukio la uchungu la kuvunjwa kwa dola ya Khilafah, tunawaalika kujiunga na kufanya kazi na sisi na kukataa fikra ambazo zilikua miongoni mwa sababu ya kufeli kwake: mafungamano ya kitaifa na kizalendo, na kufanya fungamano la Aqeedah kuwa ni lenye kutujumuisha pamoja. Hatuwaiti mujiunge na kufanya kazi na sisi ili tuwapeleke kwa ulimwengu wa ndoto, lakini tunafanya kazi miongoni mwenu na nyinyi. Tumetayarisha katiba kamili tayari kutekelezwa katika muundo wote wa dola, ikiwa wazi na safi kutokamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw) na vyanzo vinavyo elekeza kwake, Ijma ya Maswahaba na Qiyas kulingana na sababu za kisheria.

Tukitamatisha, adui wetu ni mmoja, ni Kafiri Mmagharibi, tufanye migogoro baina yetu na adui wetu wa kweli, wanaopanga vitimbi dhidi yetu usiku na mchana na kujaribu kuchukua Waislamu kuwa pamoja nao. Vita vyetu ni vimoja, uchungu wetu ni mmoja, kitabu chetu ni kimoja, Qibla chetu ni kimoja, na Aqeedah yetu ni moja. Ummah wenye yote haya unafaa kuwa na kiongozi mmoja na dola moja, na juu ya yote haya, Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha kuungana na kukataa mgawanyiko. Hakuna mgawo mkubwa kuliko uanzilishaji wa mipaka, mataifa, vibali vya kusafiria, visa, bendera na kanuni zilizowekwa na wakoloni makafiri na kufanya watu kuzitukuza kana kwamba ni ufunuo kutoka mbinguni?! Ni fikra kama hizi za wamagharibi walizotuekea na vibaraka vyao zinazo tugawanya. Kwa hivyo basi, tuzikatae na turegeshe Khilafah yetu na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi na ndio msaada wetu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele” [Al-Anfal: 24].

H. 14 Rajab 1439
M. : Jumapili, 01 Aprili 2018

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Yemen

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu