Jumapili, 05 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ]
“Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.”[Adh-Dhariyat: 55]
Rajab Mwezi ambao watu wa Yemen waliukubali Uislamu na ndani ya mwezi huo huo Khilafah Ilivunjwa

(Imefasiriwa)

Tarehe Ishirini na nane Rajab yapita kila mwaka kwa Ummah wa Kiislamu ikileta ndani yake machungu ya kumbukumbu ya kuvunjwa Khilafah mwaka wa 1342 Hijria sawia na 3 Mach 1924 Miladi. Mwaka huu 1440 Hijria, tunakaribia mwisho wa karne moja bila kua chini ya kivuli cha Khilafah (wala sio siku tatu na usiku wake), wakati wa kuchagua Khalifah na kumpa bay’ah kuhukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wetu Muhammad (saw). Maswahaba (ra) walienda mbio kumchagua Abu Bakr As-Siddiq (ra) kama Kiongozi (Khalifah) wa Waislamu baada tu ya kifo cha Mtume (saw). Khilafah ikavunjwa na wakoloni makafiri wakisaidiwa na vibaraka wao na kubadilishwa kuwa serikali za kitaifa zilioko leo katika nchi za Waislamu zikitawala na kutekeleza sheria kinyume na Uislamu. Natija yake ni kuwa Waislamu wakagawanyika vijidola dhaifu visivyoweza kusimama mbele ya adui yao aliye mnyonge na dhaifu.

Hali yetu kwa kipindi cha karne iliyopita imekua mbaya, ya uchungu na kusikitisha hali inayokataliwa na mioyo, chini ya mpango wa Sykes-Picot wa mipaka, na mipaka mipya iliyowekwa kwa kisingizio cha vita na migogoro, kuwashughulisha Ummah unaoamka wa Kiislamu kwa kupigana wao kwa wao baada ya kuishi bila kutekeleza Uislamu na maisha duni kwa kukosekana kwake.

وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. [Ta-Ha: 124]

Kwa kuwa Ummah unaelekea kufikia ngome yao thabiti iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu Al-Qawi, Al-Aziz, Al-Hakeem, Al-Mateen. Na kwa nini wasiifikie ilhali waliishi katika maisha ya nguvu na hifadhi chini ngome hii na kufikisha Uislamu kwa farasi wao kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Lakini leo chini ya kivuli cha watawala vibaraka, Waislamu wanauwawa mikononi mwa watoto wao wakilala njaa ilhali utajiri wao ukiporwa chini ya nyayo zao.

Watu wa Iman na Hekima wa Yemen mnamo Ijumaa ya kwanza ya Rajab wanasherehekea kuongoka na kuingia katika Uislamu na kujiwa na swahaba Mu’ath bin Jabal (ra) mwaka wa 9 Hijria kuwafundisha jinsi ya kuishi katika Uislamu na kuwakuhukumu kwa Uislamu. Itikadi pasina kutekeleza hukmu za Kisharia zinazo mpangilia mwanadamu maisha yake hua haina maana. Laajabu hawazungumzii janga la kuvunjwa Khilafah mnamo 28 mwezi huo wa Rajab. Wanafaa kushirikisha kuongoka kwao kwa Uislamu ndani ya Rajab, ambapo kuliwapangia maisha yao na

kumbukumbu ya kuvunjika kwa Khilafah na msiba wa kuanguka kwayo wakapoteza utekelezaji wa Uislamu. Haya ni matukio yasiyoweza kutenganishwa

Waislamu wanafaa wajue faida ya kumbukumbu hii inaweza kupatikana tu kwa kubadilisha mtazamo wao wa dunia na matokeo ya kisiasa kutoka kwa mtazamo wa kizalendo, na kujitenga na vazi lake ambalo wakoloni walitufunga nalo, kwa mtazamo wa kuwa hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwa ukubwa wa Uislamu nao ni kusimamisha Khilafah tuliyopewa bishara na Mtume (saw):

 «...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“…Kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza”.

Khilafah ni dola ya Waislamu ikiwatenganisha na watu wengine wote ikitekeleza Uislamu na kuziunganisha nchi zote za Waislamu chini yake, na sio taifa la kundi ama chama chini ya kivuli cha dola ya kitaifa ambayo watu wametaabika kutokana na moto wake na kuweka vipimo vya uteuzi ni kua katika chama tawala.

Kwa kukosekana Khilafah, mlinzi wa Muislamu, mzozo wa Yemen baina ya pande mbili za mzozo wa kimataifa baina ya Uingereza na Marekani, ambao wanataka kupata tena udhibiti wa iliyobakia katika fuo za Bahari Nyekundu nje ya tawala zao, kuizunguka kama kikuku kiganjani.

Enyi watu wa Yemen! Musiwafanye watoto wenu kuni za mzozo baina ya nchi za kikafiri wanaopapatia utajiri wa nchi, haya ni makosa makubwa, lakini badala yake washajiisheni watoto wenu kusimamisha kile kinachopendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni kazi ngumu ya kuismamisha dola ya Khilafah. Zifanyeni hukmu za Uislamu ndio kitovu cha juhudi zenu na sio pesa kuwa ndiyo dira inayowaongoza.

Khilafah ni suluhisho pekee la msingi litakalo tatua shida zote na migogoro si kwa Waislamu tu, bali ulimwengu mzima, twasema hili na tuna Imani kamili nayo. Khilafah si ruwaza wala njozi kwa sababu Kitabu cha Bwana wetu na Sunnah za Mtume zimeizungumzia kwa maelezo, na dola ya Khilafah iliyotawala karne kumi na tatu inathibitisha hili.

Inatoshelezea watu wa Iman kufuta kumbukumbu za uchungu wa kuvunjwa Khilafah na kuwazuia wale wenye tamaa ya nchi yao, wafanye kazi na Hizb ut Tahrir na kuipa nusura ili iweze kusmamisha Khilafah kwa njia ya Utume, kufuata mababu zao walio unusuru Uislamu kwa kuismamisha dola ya Mtume (saw) Madina Al-Munawara. Wawacheni waitikie mwito.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele…” [Al-Anfal: 24]                 

H. 24 Rajab 1440
M. : Jumapili, 31 Machi 2019

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Yemen

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu