Jumanne, 18 Safar 1447 | 2025/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Al-Waqiyah TV: Je, hili linakutosheleza Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ?

[Al-Waqiyah TV]

Je, hili linakutosheleza Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ?

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (ra) kuwa amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “Hajaamini yule ambaye analala tumbo lake likiwa limeshiba na hali ya kuwa jirani yake ana njaa na yeye anajua.” Basi vipi kuhusu mji wa Gaza ambao watu wake wanakufa njaa, huku pambizoni mwake kuna ardhi zilizo jaa neema na kheri nyingi, chini ya utawala wa watawala walioisaliti, na kula njama dhidi yake pamoja na maadui zake, wakafunga mipaka na kuziba midomo ya wale walioomba msaada na nusra. Hawakuridhika na kuisaliti tu, walizuia nusra yake na wakajitahidi kuizingira, wakiinyima chakula na dawa. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, tunakulalamikia juu ya hali zetu. Majeshi yetu hayakuwanusuru Waislamu, yakawa ni walinzi wa viti vya madhalimu na wakandamizaji. Basi ni lini tutajikusanya kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwani kupitia hiyo ndio wokovu wetu na maregeo ya maamuzi yetu, na kupitia kwayo huzuni zetu zinaondolewa na haki zetu zinaregeshwa. Kupitia kwayo, tutaiokoa Gaza na Palestina yote. Kupitia kwayo, tutaukomboa Al-Masjid Al-Aqsa na matukufu yote. Kupitia kwayo, tutauunusuru Umma wa Kiislamu na watu wake wanaodhulumiwa Mashariki na Magharibi mwa ardhi. Dola ambayo kwayo, na ndani yake, Dini ya Mwenyezi Mungu na waja wake itaheshimiwa. Ewe Mwenyezi Mungu, tuharakishie Ushindi Wako, na Utupe nusra Yako, na Utusaidie tusimamishe Dini Yako, Utawala Wako, na Dola Yako Uliyotuahidi sisi na Mtume wako Mtukufu akatupa bishara njema.

Chapisho la Al-Waqiyah

Jumanne, 11 Safar 1447 H - 05 Agosti 2025 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu