Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  7 Muharram 1443 Na: Afg. 1443 H / 03
M.  Jumapili, 15 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Afghanistan Imo Ndani ya Majaribio ya Kihistoria baina ya Kusimamisha Khilafah au Kutabikisha Nidhamu Zilizotungwa na Wanadamu; Msipoteze Wakati Simamisheni Khilafah!
(Imetafsiriwa)

Matukio ya ghafla na yasiyotabirika nchini Afghanistan kwa mara nyengine tena yameiweka nchi hiyo katika njia kwa vikundi anuwai vya kisiasa, viongozi wa kikabila na watu wenye ushawishi kufanya uamuzi juu ya mfumo wa kisiasa wa mustakbali nchini Afghanistan.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inawashauri viongozi wote wa kisiasa, washawishi wa kikabila, Mujahidina wa zamani, makundi anuwai, watu wenye nguvu kwamba nchi inapitia fursa ya kihistoria, inayowataka watu kukamata moja ya machaguo makuu mawili : 1) kusimamisha mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kurudisha Khilafah, na / au 2) kutabanni mfumo uliotengenezwa na wanadamu kwa kurudia hali ile ile chungu ya zamani.

Hivi sasa, Amerika, Ulaya, UN, na nchi za eneo zinashauriana na vyama anuwai vya kisiasa vya Afghanistan juu ya pendekezo la 'mfumo shirikishi', ambao utabeba viambishi vya Uislamu, kuzingatia sheria za Kimataifa, kujifunga na mipaka ya kitaifa na mchanganyiko wa Usekula na Uislamu, ambao ni lazima uidhinishwe na Jamii ya Kimataifa - mfumo ambao nyuso zingebadilika lakini sheria, nidhamu na muundo wa sasa zingebakia. Kunyakua aina kama hazo kumesababisha Afghanistan kutumbukia kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutofaulu na kukwama kisiasa katika miongo michache iliyopita. Badala yake, Waislamu wengi wa Afghanistan wanatamani kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu na utawala wa sheria ya Kiislamu. Kwa hakika ni fursa nzuri, iliyopatikana baada ya miaka mingi ya mapambano ya kifikra, kisiasa na kijeshi dhidi ya uvamizi, na haipaswi kupotezwa na mawazo finyo na ukurupukaji, kitu ambacho kilipotea mara kadhaa kwa sababu ya makosa ya vyama vya kisiasa na watu wenye ushawishi.

Hizb ut Tahrir, kwa heshima ya dhati, kwa mara nyingine tena inatoa wito kwa viongozi wote wa kisiasa, watu wenye ushawishi wa kikabila na makundi kukataa kata kata mapendekezo yoyote ya Amerika, UN, na nchi za eneo kuhusiana na mfumo wa kisiasa wa Afghanistan, na kutoruhusu kujitolea muhanga kwa Waislamu (ambako lengo lake lilikuwa ni kuregesha Sharia ya Kiislamu) kuharibiwa, bila kuleta matokeo yoyote yaliyotarajiwa. Badala yake, jaribuni kukusanya nguvu zenu kusimamisha mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kurudisha Khilafah - itumieni fursa ya sasa kwa ukamilifu! Kwa kweli, Afghanistan na eneo hili limekuza uwezo mkubwa wa kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijeshi nyoyoni mwao, na endapo mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) utatabanniwa na kuitikiwa, In Sha Allah, mabadiliko makubwa yatafanyika katika pembe hii ya ulimwengu chini ya uongozi wa watu wanaofadhaika wa ardhi hii. Hii inahitaji watu wenye nguvu walio na imani na lengo kama hilo na waonyeshe uvumilivu dhidi ya shida kwa kutenda vitendo vyao kulingana na hukmu za Shari'a. Ni fursa kubwa kwa wale wanaotaka kuwa Ansar ullah (Wafuasi wa Mwenyezi Mungu) ya kusimamisha mfumo wa Mwenyezi Mungu, na kwa wale wanaotaka kutembea katika njia ya Maswahaba na kuchagua Jannah badala ya raha za muda za ulimwengu. Ni fursa kubwa iliyoje hii kwa watu wenye hekima!

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.”

#أفغانستان                                #Afganistan                #Afghanistan

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu