Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  28 Jumada I 1442 Na: Afg. 1442 H / 07
M.  Jumanne, 12 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jamhuri ya Afghanistan Imegeuka kuwa Kichinjio; Je kuna Njia Yoyote ya Kutoroka?
(Imetafsiriwa)

Katika miezi ya hivi karibuni, idadi ya mauaji, mabomu, milipuko, mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya ovyo ovyo katika miji na vijiji vya Afghanistan yameongezeka sana, ambayo yalisababisha kuuawa kwa maimamu wa misikiti, viongozi wenye ushawishi, maafisa wa serikali, waandishi wa habari, wachambuzi, watu maarufu na raia wasio na hatia kwa njia tofauti. Hakika, watu wamezoea kuanza asubuhi na sauti za milipuko kwani jioni huishia na hasara ya kusikitisha kwa wapendwa wao. Afghanistan inatambuliwa kuwa moja ya nchi hatari zaidi kwa raia, watu wenye msemo na waandishi wa habari; lakini, serikali ya Afghanistan inalaani, kuasisi tume na kuhesabu idadi ya maiti pekee! Hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan iliwasiliana na idadi kadhaa ya maripota ili wafunge vituo vyao vya habari ikiwa hawangeweza kununua silaha ili kulinda wafanyikazi wao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inatoa rambirambi zake kwa wale waliokufa na inawaombea waliojeruhiwa kupona kwa haraka na kwa ukamilifu, ikiomba uvumilivu na thawabu kwa familia na wahanga wa matukio ya hivi karibuni, na inaangazia nyukta zifuatazo:

Kwanza, wimbi la mauaji mfululizo na kuenea kwa hofu inaashiria awamu mpya ya mradi ambao kwao pande zinazohusika katika mchakato wa amani wa Afghanistan zinafanya mashambulizi ya kijasusi kwa gharama ya damu ya Waislamu wa ardhi hii kupata hisa ya windo la simba kupitia mchakato wa amani na kugeuza rai jumla dhidi ya vikundi vya wapinzani wao. Wakati huo huo, bahati mbaya ni kwamba Amerika imepata faida kubwa kutoka kwa mchakato wa amani kwa kulinda vikosi vyake na kambi zake huku ikiimarisha mandhari ya mauaji ya halaiki ya Afghanistan.

Pili, jukumu la serikali ya Afghanistan limekuwa zaidi ya kulaani visa na kuchapisha matangazo kuhusu maiti. Watawala hawa wanakaa nyuma ya kuta za kinga na wanasafiri kupitia magari ya kivita, wakiwa mbali kabisa na watu kuhisi maumivu ambayo wamekuwa wakipata hadi sasa. Watawala hawa, kwa upande mmoja, wanajitambulisha kama mlinzi wa maadili ya kibinadamu na mlezi wa jamhuri, wakipaza sauti kubwa juu ya 'dhana ya jamhuri' kupitia vyombo vya habari; lakini, wakati nguvu na maslahi yao ya kibinafsi yanapokuwa hatarini, hubadilika kuwa wauaji hatari. Hivi majuzi, wale ambao walikuwa wakiikashifu serikali wanatishiwa kwa kifungo na / au kifo. Hakika, mauaji haya yote na hofu ni mayowe ya amani na jamhuri ambayo yanasumbua kila kona ya jamii hadi leo. Kwa kweli, hawauheshimu Uislamu wala haitii jamhuri. Wanachotambua ni kuendelea kudumisha nguvu zao na kupata maslahi.

Kwa hivyo, Waislamu wa Afghanistan lazima watambue kuwa njia ya kutoka katika janga hili hatari sio kubadilisha nyuso, bali kuutokomeza mfumo fisidifu uliopo kwa kuleta mabadiliko ya kimsingi. Mabadiliko ambayo yanaitupa mifumo hii na viongozi wenye kiu ya mamlaka iliyoingizwa kutoka nje hadi makaburini, na badala yake kuasisi mfumo kwa mujibu wa imani na maadili ya Kiislamu ya watu wa ardhi hii. Kwa upande mwingine, mfumo huo utalea viongozi wa kweli ambao wangekuwepo ili kulinda imani, uhai, mali na hadhi ya watu - wakizingatia haya kama jukumu lao la msingi. Mfumo huu si mwingine, bali ni Uislamu na Dola ya Kiislamu (Khilafah).

«إنَّما الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن ورَائِهِ ويُتَّقَى به»

“Hakika, Imam (Khalifa) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na kujilinda kwake.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu