Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  23 Muharram 1443 Na: Afg. 1443 H / 04
M.  Jumanne, 31 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan Yawapa Hongera Watu wa Afghanistan na Ummah Wote wa Kiislamu kwa Kutamatisha Uvamizi wa Amerika na NATO!
(Imetafsiriwa)

Hatimaye, baada ya miaka 20 ya uvamizi wa Afghanistan na Waamerika na washirika wao, vikosi hivyo vya uvamizi baada ya kushindwa kwa udhalilifu, viliondoka Afghanistan kwa huzuni saa sita usiku mnamo 30 Agosti 2021.

اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ اللَّهُ أَكْبَرُ!

Allahu Akbar! Allahu Akbar!

حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ، نِعْمَ الْمَوْلَى وَنِعْمَ النَّصِيرُ!

Mwenyezi Mungu anatutosha, na [Yeye] ni Wakili bora. Mlinzi na Msaidizi bora alioje!

Amerika iliivamia Afghanistan chini ya kaulimbiu za udanganyifu za 'vita dhidi ya ugaidi', ujenzi upya na usaidizi kwa nchi hii. Lakini, chini ya miito hii ya uwongo, Amerika iliua mamia ya maelfu ya watoto, wanawake na raia; iliharibu Misikiti na vijiji; ikapandikiza watawala wafisadi zaidi mno, fikra chafu na mikakati ya kijeshi iliyofeli pamoja na ajenda mbaya za kisiasa kwa watu wa Afghanistan. Amerika iliondoka Afghanistan huku uwekezaji wake wote ukipotea na serikali yake kibaraka ikivunjwa mithili ya nyumba ya buibui.

 [إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

“Hakika uwongo lazima utoweke!” [Al-Israa 17: 81].

Baada ya Uingereza na uliokuwa Muungano wa USSR, Amerika ni dola kuu ya tatu kutoroka kwa aibu kutoka Afghanistan kutokana na mapambano ya kijeshi, kimfumo na kisiasa ya watu na Mujahidina wa ardhi hii ambao wamejitolea muhanga uhai, na mali zao katika njia hii. Mwenyezi Mungu (swt) akubali kujitolea muhanga kwao!

Njia waliyoingilia Waamerika kwenye mazungumzo na Mujahidina na njia waliyoondokea Kambi ya Anga ya Bagram na Uwanja wa ndege wa Kabul katikati ya usiku inaonyesha wazi kufeli kwao kusiko na kifani na / au kushindwa nchini Afghanistan. Kushindwa huku kutabaki kama doa katika historia ya sera yao ya kigeni, ikidhoofisha sifa na hadhi yake ya kimataifa kama dola kuu nambari moja duniani. Sawa na kadhia ya Syria iliyomtoa mvi Obama, ugumu na mienendo ya Afghanistan iliwaweka marais 4 wa Amerika katika wasiwasi mkubwa kufikia hadi kumfanya Joe Biden kulia hadharani.

Sasa uvamizi umemalizwa, tungependa kuwakumbusha Waislamu wa Afghanistan kwa nukta mbili:

Kwanza: Historia imethibitisha kuwa watu wa Afghanistan daima wamefanikiwa kushinda uvamizi wa aina yoyote, lakini wameshindwa katika mchakato wa ujenzi wa dola na utawala. Hitaji msingi la watu wa Afghanistan na Umma wote ni kusimamisha Dola ya Kiislamu na Utawala wa Uislamu. Lakini, serikali za hapo awali hazikuwa zikitawala watu kwa mujibu wa Uislamu kwani zilikuwa zimeunda utawala dhaifu na mipango mibovu ya kiuchumi na hazikutabikisha Uislamu. Ndiyo sababu, baada ya muda, zilipoteza uaminifu wao na kufeli. Hivyo basi, Mujahidina na viongozi wa jeshi na wa kisiasa nchini Afghanistan wanapaswa kutambua kwamba ushindi wao unapaswa kutafsiriwa kuwa mfano wa kuigwa na matarajio kwa kundi jengine la Jihad miongoni mwa Ummah, na wanapaswa pia kuelewa kuwa kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu nchini Afghanistan kunaweza kufanya mabadiliko chanya muhimu katika eneo hili na Ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Pili: Uvamizi wa kijeshi ilishindwa kwa sababu ya kujitolea muhanga pasi na masharti yoyote kwa Mujahidina wa Afghanistan; lakini, Jihad na mapambano hayapaswi kuishia hapo. Hii ni kwa sababu Fitna haijatokomezwa kikamilifu na mabaki ya uvamizi yangalipo katika fikra, kisiasa, kiuchumi, ujasusi, sheria na miundo ya kiserikali na mifumo ya taasisi mbalimbali. Vipengee hivi vya uvamizi vyahitaji mapambano na juhudi za kina za kutokomeza mabaki haya ya uvamizi kutoka katika nyanja zote za maisha.

Kutokana na hay, sisi kwa mara nyengine tena tunapenda kupongeza ushindi wa Jihad kwa watu wa Afghanistan na tunapenda kutaja kwamba kuanzia leo na kuendelea bila shaka historia itaandikwa tofauti: Afghanistan isiyo vamika na ulimwengu bila uaminifu wa Amerika! Ingawa, Magharibi itaendelea kujaribu kula njama dhidi ya matakwa ya watu wa Afghanistan, lakini viongozi wa Mujahidina wanapaswa kutambua kwamba kuwa imara katika uwanja wa vita kulisababisha ushindi wa kijeshi juu ya uvamizi; vivyo hivyo, kuwa thabiti katika siasa kutasababisha kuzishinda njama zao na kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 30:4-5]

#أفغانستان             #Afganistan       #Afghanistan

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu