Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  11 Sha'aban 1444 Na: Afg. 1444 H / 06
M.  Ijumaa, 03 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bila ya Khilafah, Wanachama wa ‘Ummah Teule’ Watazama Baharini!
(Imetafsiriwa)

Shirika la Habari la ANSA, chombo cha habari cha Italia, limeripoti kuwa wakimbizi 60 ambao wengi wao ni raia wa Afghanistan, Pakistan na Iran wamepoteza maisha kufuatia kuzama kwa meli katika bahari ya Italia. Meli hiyo ilikuwa imebeba wakimbizi 250 waliozama katika bahari ya Crotone, Italia baada ya kugongana na mwamba. Wakati huo huo, polisi wa Bulgaria walitangaza Jumapili iliyopita, Februari 19, 2023, kwamba miili ya raia 18 wa Afghanistan ilipatikana ndani ya lori la mizigo. Iliaminika kuwa wakimbizi walipoteza maisha kutokana na ukosefu wa oksijeni.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Afghanistan huku ikionyesha masikitiko yake makubwa inakumbusha kwamba hii ni mifano midogo tu ya masaibu na uchungu unaoupata Ummah mteule - taifa ambalo limekabidhiwa na Mwenyezi Mungu (swt) jukumu la kutumikia. watu kote duniani:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aali Imran: 110].

Maadamu Ummah huu mteule ulitimiza jukumu na wajibu wake kwa kuasisi mfumo na dola ya Kiislamu, walikuwa wakienda Ulaya kama wakombozi, wakafikia milango ya Vienna na Moscow. Lakini pindi walipopoteza dola na mfumo wa Kiislamu pamoja na kusahau jukumu lao la kiulimwengu, sasa wanakimbilia kutafuta hifadhi katika nchi za Magharibi; ingawa, Mwenyezi Mungu (swt) amewaumba wanadamu ili wamuamini, waishi kwa mujibu wa ujumbe Wake na wasimamishe Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) duniani kupitia dola ya Kiislamu (Khilafah) kwa njia ya Utume.

Ilikuwa ni kwa kuanguka kwa Khilafah ambapo ardhi zetu ziligawanywa, kisha kukaliwa kimabavu na kukoloniwa; watawala waovu na/au mifumo fisadi ya kikafiri iliwekwa juu yetu; na hatimaye rasilimali zetu zikaporwa. Hapakuwa tena na Dar-ul-Islam, mahali ambapo raia wake wangeweza kuhisi hali ya usalama na ustawi. Ilikuwa ni kwa sababu ya uvamizi na ukoloni uliotufanya tupitie vita vya muda mrefu, umaskini wa bandia, na migawanyiko mibaya kwa msingi wa mipaka ya kitaifa. Mbele ya matukio hayo yote, wapo waliohangaika kutimiza jukumu lao huku wengine wakiachana. Badala ya kujitahidi kwa ajili ya mwamko wa Umma wa Kiislamu, kupata uhuru kutoka kwa ukoloni, kukomesha ukaliaji kimabavu, na kusimamisha Khilafah, kwa bahati mbaya waliichukulia thaqafa na hadhara ya Kimagharibi kuwa ndio njia bora ya maisha. Waliiona faraja na urahisi huo kuwa ni baraka ambayo iliwafanya kukimbilia Magharibi wakijua kwamba kwenda Magharibi na kuishi miongoni mwa makafiri kungewaletea madhara ya hatari duniani na Akhera.

Kwa upande mmoja, watawala wa Kiislamu katika ardhi za Kiislamu wanaamiliana na wakimbizi huku wakikusudia kupata fadhila kutoka kwa mabwana zao wa Magharibi; kwa upande mwingine, serikali na mashirika ya Magharibi yana tabia ya kishenzi na wahamiaji. Ingawa, wanajifanya kutetea haki za binadamu na ubinadamu, wanaonekana kutumia wakimbizi kama zana za kisiasa - wakitumia tu vipaji na nguvu kazi ya vijana kama chanzo cha kazi kwa ukuaji wao wa kiuchumi na uzalishaji.

Kwa hivyo, ni jukumu la watawala wa sasa wa Afghanistan kutilia maanani sana elimu ya kifikra ya Waislamu kwa upande mmoja, na kuwapa watu makaazi, chakula, mavazi na hali bora zaidi kwa usalama, elimu na afya katika jamii kwa upande mwingine. Ili raia wasije wakaingia katika vishawishi na kusiwe na fursa kwa adui na dola za kikafiri kujipenyeza na kuwahadaa watu kwa ahadi za kidunia zinazoimbwa na Wamagharibi. Kwa hivyo, kwa kweli tunahitaji mno mfumo muongofu na ajenda pana ya kuanzisha jamii thabiti na yenye uaminifu ambayo chini ya mwavuli wake tutaibuka tena kama taifa la ushindi kuelekea ulimwengu wa makafiri sio kama wakimbizi, lakini kama wakombozi na wabebaji wa kheri. (ulinganizi wa Uislamu).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu