Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  21 Rabi' I 1444 Na: Afg. 1444 H / 05
M.  Jumatatu, 17 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Dola za Kigaidi au wale Wanaoitwa Wanachama wa SCO Wazungumza kuhusu 'Vita dhidi ya Ugaidi' nchini Afghanistan!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, Oktoba 14, 2022, New Delhi iliandaa mkutano wa baraza la Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) chini ya kichwa cha Muundo wa Kikanda wa Kupambana na Ugaidi (RAT). Baada ya mkutano huu, baadhi ya nchi wanachama ziliapa kutekeleza hatua za pamoja ili kukabiliana na vitisho vinavyotokana na makundi ya kimataifa ya kigaidi yanayoendesha operesheni zao kutoka Afghanistan.

Tangu mwaka wa 2001, hata hivyo, kile kinachoitwa mandhari ya Kimagharibi ya 'Vita dhidi ya Ugaidi', ambayo kwa hakika ilikuwa ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu, imeonyesha kufeli kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa, kila dola inafafanua neno ‘ugaidi’ kulingana na maslahi yake yenyewe, ikiwataja maadui zake kuwa magaidi na/au wafuasi wa ugaidi. Hata hivyo, ikiwa mtu atatafuta maana ya neno hili katika Kamusi ya Oxford, atapata: "matumizi ya vitendo vya vurugu kufikia malengo ya kisiasa". Kulingana na Kamusi ya Oxford, nchi wanachama wa SCO ndio dola halisi za kigaidi.

Mapambano ya kigaidi ya China dhidi ya Waislamu wa Turkistan Mashariki - kwa vile ardhi zao zinakaliwa kimabavu na wao wenyewe wanateswa kwa sababu tu wao ni Waislamu. Harakati ya Hindutva na dola ya Kibaniani ya Modi ambayo sio tu imeikalia kwa mabavu Kashmir bali pia inaendelea kuwakandamiza Waislamu wa India. Serikali ya Pakistan, ambayo inawakandamiza Waislamu katika maeneo ya Baloch na Pashtun, inashirikiana vikali na dola za kikoloni, hasa Marekani katika kuwaua Waislamu ili kudumisha maslahi yake, imefungua njia zake za anga wazi kwa droni za Marekani - ikitoa usaidizi kwa dola kuu zenye nguvu kufanya mashambulizi ya kijasusi ndani ya Afghanistan. Kadhalika, Iran, ambayo imeunga mkono mauaji ya Waislamu nchini Syria, Iraq na Yemen, ilishirikiana na Marekani na NATO katika kueneza ugaidi katika nchi za Afghanistan na Iraq - bado ina nia ya kuwatia hofu raia wake kwa njia na mbinu mbalimbali ili tu kuhakikisha uhai wake wa kisiasa. Dola ya Urusi pia iliwauwa mashahidi mamia kwa maelfu ya Waislamu nchini Syria huku Waislamu wa Chechnya na Asia ya Kati wangali wakipumua vibaya chini ya ukandamizaji wake. Mbali na hilo, dola za Asia ya Kati zimeshirikiana mkono na Bwana wao katika kuwatesa na kuwakandamiza Waislamu na harakati za Kiislamu.

Hata hivyo, mipango, maamuzi na njama za dola hizi yataangamia kwani uhalisi unaonyesha kwamba wao [nchi wanachama wa SCO] sio tu kwamba wamefarikiana bali wanabeba uhasimu mkubwa dhidi ya mwengine. Ushirikiano huo wa dola za kigaidi unaashiria kuwa wana wasi wasi mkubwa kuhusiana na kuibuka dola yenye nguvu ya Kiislamu katika eneo hilo; hivyo, wanajaribu kuzuia kuinuka kwa Uislamu kwa njama hizo. Hata hivyo, wanapaswa kujifunza kutokana na historia kwamba katika vita kati ya Haki na Batili, daima ni Haki inayoshinda na kuitowesha Batili.

Tunaamini kwamba mwamko wa Kiislamu, fursa ya umoja wa Waislamu na kusimamisha tena Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume inawezekana zaidi nchini Afghanistan, Pakistan, na Asia ya Kati kuliko katika sehemu nyingine yoyote duniani - hili ndilo lililoongeza wasiwasi wa dola hizi. Dola hizi zinajaribu kusimama dhidi ya wimbi kubwa la mwamko kwa hatua zao tasa wakati wimbi hili ni kubwa kwani limepunguza ubwana wa dola hizi za wauaji kuwa kiwango cha chini. Inshaallah, hivi karibuni Waislamu wa eneo hili watalindwa kutokana na udhalimu wa dola hizi na watafurahi kwa kusimama Khilafah ya Kiislamu.

(لِلَّهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu