Jumapili, 17 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  19 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: Afg. 1445 H / 26
M.  Jumatatu, 27 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kufichua Uhalifu wa Wazayuni na Kupaza sauti ya Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina si ‘Uhalifu’ bali ni Wajibu wa Kiislamu wa Kila Muislamu!

(Imetafsiriwa)

Mnamo Novemba 2023, wabebaji Dawah wawili wa Hizb ut Tahrir walizuiliwa na maafisa wa ujasusi wa mkoa wa Nangarhar walipokuwa wakizungumza katika maandamano yaliyolenga kulaani mashambulizi ya kikatili ya umbile la Kizayuni huko Gaza. Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, wabebaji Dawah hawa wamekuwa katika hali ya isiyokuwa na uhakika katika suala la mamlaka, na wanajulikana kama ‘Wafungwa wa Kadhia ya Palestina’ miongoni mwa wafungwa wa Gereza la Jalalabad.

Inashangaza kuona kwamba tangu lini na kwa kuzingatia hukmu ipi ya Sharia, ujasiri wa kufichua jinai za Wazayuni na kupaza sauti za Waislamu wa Palestina umetajwa kuwa ni kitendo cha ‘uhalifu’? Kiwango cha mauaji ya halaiki na jinai za kivita zinazofanywa na umbile la Kizayuni ni ule usio na kikomo na wa kikatili ambao hata uliwalazimu mamia ya maelfu ya wasiokuwa Waislamu kufanya maandamano makubwa ya kulaani ukatili na jinai hizo za kivita; lakini kwa bahati mbaya, kuwatetea Waislamu waliokandamizwa wa Palestina sio tu kwamba ni marufuku katika ardhi ya Kiislamu bali pia kunatuzwa kwa jela. Ukweli mchungu ni kwamba serikali inayotawala nchini Afghanistan inazuia mikutano ya pamoja kuhusiana na uhalifu wa Gaza. Huku ikiwa ni wajibu wa Majeshi ya Kiislamu na watu wenye mamlaka kukimbilia kuwatetea Wapalestina wanaodhulumiwa. Kwani Waislamu wa Palestina wangali wanataraji kuwaona Mujahidina wa Afghanistan wakija kuwaokoa; ndio maana wamewaita mara nyingi ili wapate msaada.

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal:72]

Hoja kwamba ‘ni faradhi tu kwa tawala za Kiarabu na nchi jirani za Palestina kuwafikia Waislamu wa Gaza’ ni udhuru usio wa Kiislamu na matarajio yasiyo ya kisiasa. Kwa sababu mtu yeyote mwenye ufahamu wa kisiasa angetambua vyema zaidi kwamba tawala hizi hazijafanya lolote kuzuia jinai za Wazayuni, na ni wazi kutokana na vitendo vyao kwamba tawala hizo si lolote ila ni stoo za Marekani na kivuli cha umbile la Kizayuni.

Madai ya kwamba ‘tunapaswa kwanza kujiimarisha na kisha kuwafikia Waislamu wa Palestina’ pia ni madai yasiyo na msingi. Ikiwa dai kama hilo lingekuwa kweli, serikali inayotawala ingekuwa imefanya mradi wa uhamasishaji wa kijeshi na ingefanya juhudi kubwa kujitayarisha kijeshi kwa madhumuni haya makubwa.

La kusikitisha, kinachoonekana miongoni mwa baadhi ya viongozi ni kwamba ruwaza yao kuhusu mafunzo na kuwapa Mujahidina zana yamezidi kuwa finyo kila uchao, na kudogoshwa hadi kwenye mipaka ya kitaifa ya Afghanistan. Wakati Mujahidina wanapaswa kupewa mafunzo na kuwezeshwa na wazo la kukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, Kashmir, Turkestan Mashariki na ardhi nyinginezo, na pia wanapaswa kuwa na mkakati wa kivitendo mezani wa kuiondoa mipaka bandia. Kuzikomboa ardhi za Kiislamu kutokana na kukaliwa kimabavu ni wajibu ambao watu wenye nguvu wanapaswa kuutekeleza haraka iwezekanavyo.

Matukio ya kikatili yanayotokea katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina ni Ibtila (mtihani) mkubwa zaidi wa Umma wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Zaidi ya siku 200 tangu kuanza kwa vita vya kikatili huko Gaza, sura halisi za dola kubwa, taasisi za kimataifa, waangalizi wa haki za binadamu, watawala wa Waislamu na watu wenye nguvu zimefichuliwa huku misimamo yao ya uoga na vyeo vyao vikifichuliwa. Ni kana kwamba Waislamu wa Gaza wanapigana peke yao dhidi ya majeshi ya hali ya juu ya Ukafiri yaliyo na AI na silaha za hali ya juu zinazokimbia kutoka Mashariki kupitia Magharibi ili kuwakandamiza Waislamu.

[وَلِيُمَحِّصَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكافِرِينَ]

“Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie mbali makafiri.” [Aali Imran:141]

Bila shaka watawala wa Kiislamu na watu wenye nguvu watahisabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu (Al-Qahhar) Siku ya Kiyama kwa kitendo chao cha kunyamazia kimya kuhusiana na jinai za Wazayuni nchini Palestina; na wale ambao - kutokana na matamanio yao ya Nafs - wamewafunga wabebaji Dawah kwa sababu tu walikuwa wakipaza sauti za Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina na kufichua jinai za madhalimu watakabiliwa na hesabu kali zaidi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu