Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  18 Rajab 1441 Na: 1441/10
M.  Ijumaa, 13 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Lini Mujahideen wa Zamani watajifunza kutokamana na wao kudungwa mara kwa mara na Amerika?!

(Imetafsiriwa)

Kwa muda mrefu, Amerika imepuuza kutambua kujitolea na matendo ya kusifika ya Mujahideen wa zamani na kuyakanyaga. Badala yake daima humuweka mtu aliyejitolea zaidi, kidemokrasi na kisekula katika madaraka ambaye kihisia na kiakili hausiani na watu wa Afghanistan kamwe.

Mwenyezi Mungu (swt) aliwabariki Mujahideen hawa na msaada wake na hadhi yao wakati walipoanza kupigana na Umoja wa Kisovieti kwa ikhlasi na kujitolea, ambayo moja ni upendo mkubwa wa umma na msaada walioupokea. Hata hivyo, baada ya kuhudhuria kwao katika kongamano la Bonn [2001], baadhi ya hawa Mujahideen, kwa njia ya kudhalilisha, waliikabidhi hadhi ya kisiasa ya Afghan na uwanja kwa Wavamizi makafiri wa Kiamerika, ili tu watafute hadhi yao katika muungano na msaada wa Wamagharibi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) aliwaacha wao kwa Waamerika [kuamua juu yao]. Ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu (swt) kupeana neema na ushindi kwa makundi yoyote yanayosimama juu ya Uislamu na kumfichua na kumdhalilisha yeyote yule ambaye anaisaliti Dini ya Mwenyezi Mungu (swt)

Katika miaka 19 iliyopita, Waamerika kupitia sera zao zilizokita katika manufaa wamewatumia baadhi ya Mujahieen hawa kama bidhaa za matumizi. Wanawaweka katika kushiriki madaraka, iwapo Waamerika wataona kuna umuhimu wao katika kuhalalisha nidhamu yao bandia na kuwaweka kando wakati mahitaji yao yamekamilika. Kwa hivyo, baadhi ya viongozi wao wa kisiasa aidha huuawa kimwili au sifa zao huchafuliwa kupitia kashfa ambazo zimewagharimu wao msaada wa ummah na kisiasa. Mahusiano yao na Waamerika na NATO hayakuwaweka wao mbali tu na Muumba wao bali pia yaliwafanya wapoteze nafasi zao na mahusiano mazuri katika mujtama.

Leo, wakati baadhi ya hawa Mujahideen wa zamani wanadai kuwa wameanzisha "Serikali ya watu wote" ambayo sio chochote ambacho kimesimama juu ya Uislamu au kutishia ajenda za Amerika nchini. Bali hii ni kurudia makosa ya zamani ambayo yalenga tu kupokea marupurupu ya kibinafsi ambayo hayawezi kuwasaidia wao kurejesha nguvu na hadhi yao iliyopotea.

Hizb ut Tahrir iko kwa mara nyingine tena hapa kuwakumbusha kwa dhati juu ya fursa ambazo bado wanazo za ukombozi kutokamana na uhaini wao wote waliourudia na kuomba msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa kuongezea, wanaweza kurudisha hadhi yao na heshima iliyopotea mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na watu wao iwapo wataanza kunyanyuka dhidi ya uvamizi wa Amerika, jamhuri, imani za kidemokrasia na kujitahidi kufufua maadili ya utawala wa Kiislamu. Hivi ndivyo wanaweza kulipa fidia kwa madhambi yao na uhalifu walioutekeleza. Mwenyezi Mungu (swt) ni mkarimu mno na mrehemevu mno na humuhukumu kila mtu juu ya yale wanayomalizikia nayo maishani mwao.

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَى]

“Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa.” [An-Nazi’at: 26]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu