Alhamisi, 26 Rajab 1447 | 2026/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Enyi Waislamu: Maisha Yenu Yanawezaje Kuwa Mazuri Wakati Wanawake Walio Huru Wako Katika Magereza ya Mayahudi, Wakiteswa na Heshima Zao Zikivunjwa?!

Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Palestina kilifichua, kulingana na ushuhuda mpya uliokusanywa na mawakili na watafiti wa kituo hicho kutoka kwa wafungwa kadhaa walioachiliwa huru kutoka Ukanda wa Gaza kutoka magereza na vituo vya uzuizi vya umbile la Kiyahudi, utaratibu na mpangilio wa mateso ya kingono, ikiwemo ubakaji, kuvua nguo, kulazimishwa kurekodi filamu, na unyanyasaji wa kingono kwa kutumia zana na mbwa, pamoja na udhalilishaji wa kisaikolojia wa makusudi unaolenga kuponda utu wa binadamu na kufuta kabisa kitambulisho cha mtu binafsi.

Soma zaidi...

Rais wa Slovenia Hajui Historia, au Anaipuuza!

Hii ilikuwa katika mahojiano na Kituo cha Al Jazeera mnamo 9/11/2025, ambayo kituo kilitangaza kikamilifu asubuhi ya 10/11/2025. Kutoka ardhi ya Waislamu huko Qatar, Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar, anasema: “Israel ina haki ya kuwa na dola.” Swali linaloelekezwa kwa rais ni: Ni nani aliyelipa umbile hili haramu la Kiyahudi haki hii? Na je, kuna mtu yeyote anayesoma historia na hajui jinsi umbile hili lemavu lilivyoanzishwa katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina? Je, mauaji ya Mayahudi dhidi ya Waislamu, watu wa Palestina, yanaondoka akilini mwa msomaji yeyote adilifu wa historia? Umbile hili lemavu lilisimamishwaje juu ya mafuvu na maiti za watu wengi wa Palestina?

Soma zaidi...

Ukumbusho kwa Waislamu kuhusu Utakatifu wa Muislamu: Damu Yake, Mali Yake, na Heshima Yake

Vyombo vya habari vilisambaza habari za uhalifu wa kutisha uliotokea katika mji wa Al-Fashir nchini Sudan, wa mauaji, ubakaji, na uhamishaji uliosababisha maelfu ya familia kuhama. Na swali linalojitokeza ni: je, inawezaje kuwa rahisi kwa Muislamu anayeshuhudia kwamba hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na anaamini Siku ya Mwisho—inawezaje kuwa rahisi kwake damu ya ndugu yake Muislamu, mali yake, na heshima yake?!

Soma zaidi...

Dharau ya Amerika kwa Raia Wake Yenyewe Yawaacha Wanawake na Watoto na Njaa

SNAP (Programu ya Usaidizi wa Lishe ya Ziada) ni mpango wa shirikisho unaowasaidia watu binafsi, familia, na wale wenye ulemavu kupata manufaa ya kielektroniki ambayo hutumika kwa chakula, vinywaji visivyo na kileo, na mimea kukuza chakula chao wenyewe. Inaripotiwa kuwa kuna Wamarekani milioni 42 ambao hutegemea manufaa ya SNAP kujilisha wao wenyewe na familia zao. 54% ya watu wazima wanaopokea manufaa ya chakula ni wanawake, hasa kina mama wasio na waume, na 39% ni watoto, ambayo ina maana kwamba takriban mtoto 1 kati ya 5 hutegemea manufaa haya ili kuhakikisha hawalali njaa.

Soma zaidi...

Je, Kukamatwa kwa El Fasher Ndio Mwisho wa Mpango, Au Bado Kuna Mishale Zaidi Yenye Sumu Kwenye Ala?

Sudan imeshuhudia mabadiliko makubwa katika vita vyake, ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya miaka miwili, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikichukua udhibiti wa El Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan. Hii imeimarisha udhibiti wao katika eneo hilo. Mapigano sasa yamejikita katika eneo jirani la Kordofan.

Soma zaidi...

Wewe Ndiye Uliyewaletea Waislamu Njaa, Masoud Pezeshkian!

Iran ilitangaza kufilisika kwa benki yake kubwa zaidi ya kibinafsi, Benki ya Ayandeh, ambayo ina matawi 270 nchini Iran, baada ya madeni yake kupanda zaidi ya dolari bilioni tano, na kinachoshangaza ni ukosoaji wa rais wa Iran Masoud Pezeshkian kuhusu kushindwa kwa utawala akisema: “Tuna mafuta na gesi lakini tuna njaa”!

Soma zaidi...

Watawala wa Waislamu Hawana Sifa za Kulinda Heshima ya Waislamu!

Vyombo vya habari viliripoti kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alicheza densi kwenye zulia jekundu kwenye uwanja wa ndege nchini Malaysia mnamo Jumapili, 26/10/2025, alipopokewa na Waziri Mkuu wa Malaysia. Idadi ya Wamalaysia, wanaume na wanawake, walipunga bendera za Marekani na kucheza muziki wa kienyeji ili kumkaribisha mhalifu huyo muuaji ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza.

Soma zaidi...

“Vita vya Burqa” vya Wananchi Ni Mwangwi wa Kisasa wa Ukoloni wa Ulaya, Uliotumika Kupuuza Mauaji ya Halaiki mjini Gaza na Kumvua Mwanamke wa Kiislamu Kitambulisho Chake cha Kiislamu

Vita vya hivi karibuni vya watu wengi kutoka kwa vyama vya kidemokrasia na serikali za mrengo wa kulia vinavyotaka kupigwa marufuku kwa burqa sasa vinajumuisha Australia, Italia na Ureno. Mataifa haya ni sehemu ya kundi kubwa la nchi adui za Ulaya ambazo tayari zimepiga marufuku burqa. Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, na Uswizi zinatekeleza marufuku ya kitaifa katika maeneo yote ya umma, huku Uholanzi na Ujerumani, zikiwa na marufuku ya sehemu inayolenga muktadha maalum kama vile shule au afisi za serikali. Nchini Uingereza, mjadala unalenga wafanyikazi, ambapo chama cha mrengo wa kulia cha Mageuzi cha Uingereza kinasema kwamba burqa kama hizo zinazuia uoanishwaji, mawasiliano, na usalama, zikiziita “nembo za mgawanyiko.”

Soma zaidi...

Mayahudi Hawaheshimu Maagano Wala Hawawezi Kuaminiwa, Na Wapatanishi Si Waaminifu

Umbile la Kiyahudi limekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano dhidi ya Gaza zaidi ya mara 80, na kusababisha mashahidi wengi na majeraha, pamoja na kubomolewa kwa nyumba na uharibifu wa mali. Waziri mkuu wa umbile la Kiyahudi hata alijisifu kwamba aliangusha tani 153 za mabomu kwenye Ukanda wa Gaza kwa siku moja.

Soma zaidi...

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chahitimisha Kampeni yake ya Kimataifa: “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimeendesha kampeni ya kimataifa ya kuinua ufahamu wa kimataifa na kuleta muanga wa kimataifa kuhusu mgogoro wa kutisha wa kibinadamu uliosababishwa na mzozo nchini Sudan ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mitatu na nusu sasa. Mzozo huu usio na maana, kati ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) vinavyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (“Hemedti”), umesifiwa kama “Vita Vilivyosahaulika” kutokana na kutopokea uangaziaji wa vyombo vya habari na uangalizi wa kimataifa unaostahili.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu