Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: 23:23:42 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  24 Safar 1443 Na: 1443 H / 008
M.  Ijumaa, 01 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Enyi Waislamu wa India! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ وَمَنْ قُتِلَ دُونَ دِينِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ دَمِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ أَهْلِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ»

“Yeyote anayeuwawa kwa kutetea mali yake ni shahidi, na yeyote anayeuwawa kwa kutetea Dini ni shahidi, na yeyote anayeuwawa kwa kutetea damu yake ni shahidi na yeyote anayeuwawa kwa kutetea familia yake ni shahidi.” [Tirmidhi]
(Imetafsiriwa)

Ulimwengu ulishuhudia, kwenye mitandao ya kijamii, kipande cha video cha kutisha kinachoonyesha polisi wa India wakiwafyatulia risasi wakaazi wa kitongoji cha Waislamu, katika jimbo la Assam kaskazini mashariki mwa India, kuwaondoa kwa nguvu kutoka katika nyumba zao. Video hiyo ilionyesha ufyatuaji risasi wa kinyama kwa mkulima mmoja, ambaye jina lake lilikuwa Moinul Haque. Alipigwa kifuani na kuanguka chini, akikata roho, baada ya hapo maafisa wa polisi waliohamaki walimpiga kwa fimbo, wakati alipokuwa anafariki. Mwanahabari mmoja mpiga picha, aliyeandamana na vikosi hivyo vya polisi, Bijay Shankar Baniya, aliukanyaga mwili uliojeruhiwa, uliotulia tulii wa Moinul Haque, Mwenyezi Mungu amrehemu na amsamehe. Hili lilitokea wakati wa mchakato wa kuwahamisha maelfu ya Waislamu katika jimbo la Assam, kaskazini mashariki mwa India. Waziri wa Assam, anayehusika na Jimbo la Assam, Himanta Sarma, aliandika nukuu ya tweet juu ya kufurushwa kwa watu kulikofanywa na Polisi wa Assam, akielezea furaha yake, "Kuendelea na harakati zetu dhidi ya uvamizi haramu, ninafurahi na napongeza usimamizi wa wilaya ya Darrang na @assampolice kwa kuweza kusafisha karibu bigha 4500, kwa kuzifurusha familia 800, kubomoa majengo 4 haramu ya kidini na taasisi moja ya kibinafsi huko Sipajhar, Darrang." Wakati huo huo, vyanzo vya habari viliripoti kwamba karibu Waislamu 20,000 walifurushwa majumbani mwao, baada ya uamuzi wa mamlaka wa kutokomeza vitongoji vya makaazi ya Waislamu, kwa kisingizio kwamba yalikuwa yamejengwa kwenye ardhi inayomilikiwa na serikali.

Kuuawa na kuteswa kwa Waislamu nchini India kwa jumla, na huko Kashmir na haswa Assam, sio jambo geni. Kumeendelea tangu ukoloni wa Uingereza ulipokiuka Bara Dogo la Waislamu la India, kwa kuchukua hatua kadhaa za kihalifu dhidi ya Waislamu huko. Sera ya Uingereza ilijengwa juu ya msingi wa mauwaji ya kikabila ya Waislamu katika Bara hilo dogo, na kuwagawanya katika vijidola vinne, India, Pakistan, Bangladesh na Myanmar (Burma), ili kuvunja nguvu, mshikamano na umoja wa watu hao, kudhoofisha utawala wa Uislamu na Waislamu juu ya Bara Hindi.  

Serikali ya BJP, ikiongozwa na mchinjaji wa Gujrat na mvunjaji Msikiti wa Babri, Modi, na serikali ya mitaa huko Assam, ni upanuzi tu wa enzi hiyo ya ukoloni ya Uingereza,  ingawa kwa mshtuko mpya wa Amerika, kwa kuwa chama cha Modi kinaegemea upande wa ukoloni wa Amerika. Kwa hivyo, haikushangaza kuona ukimya wa jiwe wa kafiri Magharibi, ukiongozwa na wakoloni wapya na wa zamani, kwa uhalifu uliofanywa na mtoto wa ukoloni wa Kimagharibi, India, dhidi ya Uislamu na Waislamu ndani ya eneo lake. Wala haishangazi kuona ukimya wa jiwe wa watawala waovu katika Ulimwengu wa Kiislamu, wa karibu zaidi na wa mbali, kwani wao ni vibaraka wa ukoloni. Hakika, hawana mamlaka, isipokuwa yale wanayoamrishwa na mabwana zao huko Magharibi. Lakini, lau kama wangekusudia kuwasaidia Waislamu wa India wanaodhulumiwa, isingekuwa vigumu kwao kuwasaidia.

Kwa mfano, uwekezaji wa India nchini Imarati (UAE) ni mkubwa zaidi kati ya mataifa mengine yote ulimwenguni. Maslahi ya kiuchumi ya India nchini Imarati ni muhimu mno, haiwezi kusubutu kuyapoteza. Fauka ya hayo, wafanyikazi wa India katika Dola za Ghuba wanachukuliwa kama mshipa wa uhai katika kutuma pesa kwa hazina ya serikali ya India. Tishio dogo tu la kuwafukuza Mabaniani kutoka dola kama hizi lingeilazimisha India kupiga magoti, kwani Imarati inashika nafasi ya kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu na ya 11 ulimwenguni, katika orodha ya Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini India, kwa thamani ya karibu dolari bilioni 17.2. Imarati ni mshirika wa tatu mkubwa zaidi wa kibiashara wa India baada ya Amerika na China, na ujazo wa biashara unakadiriwa kuwa $ 60 bilioni. Imarati inasafirisha bidhaa kama bidhaa za petroli, madini ya thamani, kemikali na bidhaa za mbao kwenda India. Imarati iliuza nje mafuta ghafi yenye thamani ya dolari bilioni 10.9 mnamo 2019-2020 na ilikuwa kituo cha pili kikubwa zaidi cha uagizaji bidhaa za India. Imarati inahesabu karibu asilimia 50 ya jumla ya biashara ya India na dola za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) na asilimia 71 ya usafirishaji bidhaa jumla wa India kwa GCC. Kwa upande wa uwekezaji, Imarati ndio mwekezaji mkubwa zaidi wa Kiarabu, kwani uwekezaji wake unawakilisha karibu asilimia 82 ya jumla ya uwekezaji wa Kiarabu nchini India, ikiwa na thamani jumla ya uwekezaji ya dolari 15 bilioni. Kwa hivyo, Imarati peke yake inaweza kuitishia India na kuwasaidia Waislamu huko, lakini hilo lingali ni ndoto!

Kusaidia Waislamu nchini India na kulinda matukufu yao ni wajibu kwa Waislamu wote, haswa dola zenye nguvu zilizo jirani kama Bangladesh, Pakistan na Taliban nchini Afghanistan. Sehemu yoyote kati ya hizi tatu inaweza kumzuia Modi na serikali yake ya kibaguzi. Lakini, hii inahitaji watu wanaomiliki nguvu na mamlaka nchini Pakistan na Bangladesh kuzing'oa serikali zao vibaraka, zinazoshirikiana na Modi. Hapo tu ndipo wataweza kuyahamasisha majeshi kuwasaidia Waislamu nchini India na kubomoa ngome ya Dola ya Kibaniani, sio tu kuikomboa Kashmir na Assam pekee, bali pia kulirudisha Bara zima la India kwenye zizi la Uislamu, chini ya bendera ya Khilafah Rashidah ya Pili, ambayo wakati wake umewadia.

Ni wajibu kwa Waislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na wale walioko Imarati, Pakistan, na Bangladesh, sio tu kutaka kususiwa kwa bidhaa za India, lakini pia kudai kukatwa kwa mafungamano yote na serikali ya India, yakiwemo mahusiano ya kiuchumi. Ni wajibu kwa Waislamu kuyataka majeshi ya Waislamu, haswa majeshi ya Pakistan, Bangladesh, Hijaz na Imarati kuwapindua watawala wao wasaliti na kutoa Nussrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah na kumteua Khalifah Muongofu, atakayeyaongoza majeshi hayo kunusuru Uislamu na Waislamu, akirudia historia ya kamanda wa jeshi, Muhammed bin Qasim Al-Thaqafi, aliyelifungua Bara Hindi kwa Uislamu.

Sera ya ubaguzi wa rangi ya Modi dhidi ya Waislamu nchini India inaweza kusababisha nchi hiyo kuharibika na kugawanyika zaidi kuliko hata ilivyo sasa. Sera kama hiyo haitamtumikia yeyote nchini, bila kujali dini yao au kabila. Zaidi ya hayo, yote haya ni mwendelezo tu wa sera ya wakoloni wa Uingereza na sera ya Amerika ya vita dhidi ya Uislamu. Sera hiyo inatumikia tu maslahi ya Magharibi na Amerika, huku watu wote wa India watalipia gharama yake kubwa

Idadi ya Waislamu nchini India ni takriban watu milioni 400, ikiwa ni asilimia 40 ya idadi ya watu wa India. Idadi hiyo sio kama inavyodaiwa na serikali, ambayo ni nusu ya hiyo. Kwa hivyo, sio sahihi kuwachukulia Waislamu kama wachache walioshindwa. Badala yake, Waislamu wa India wana uhusiano wa asili na Waislamu wote katika Bara la India na Asia ya Kati, ambao inawafanya kuwa watu wa ardhi hizo.

Kwa Waislamu wa India ambao wamelengwa na kudhulumiwa, tunawakumbusha kwamba udhaifu hukaribisha udhalilishaji, huku kujitayari na kifo huleta heshima. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ دِينِهِ، فَهُوَ شَهِيدٌ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ دَمِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ أَهْلِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ»

“Yeyote anayeuwawa kwa kutetea mali yake ni shahidi, na yeyote anayeuwawa kwa kutetea Dini ni shahidi, na yeyote anayeuwawa kwa kutetea damu yake ni shahidi na yeyote anayeuwawa kwa kutetea familia yake ni shahidi.” (Tirmidhi). Kwa hivyo, tunawaambieni, simameni kwa ajili haki zenu kama vile ndugu yenu Moinul Haque alivyosimama. Alikuwa jasiri katika kukabiliana na wale waliotaka kumpora nyumba yake. Na kwa watu wa India kwa ujumla na haswa wasomi, tumewahutubia mara kwa mara kukomesha wazimu wa Modi na wafuasi wake miongoni mwa watu wa India. Kumbukeni kwamba mnaishi pamoja na Waislamu, huku majeshi yao yameizunguka India. Kumbukeni kwamba Waislamu ni Umma mmoja na hivi karibuni hali itageuka, wakati ardhi zao zitakapounganishwa na mipaka kati yao kufutwa. Huenda mkajuta wakati huo.

Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu