Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Sha'aban 1443 Na: 1443 H / 028
M.  Ijumaa, 01 Aprili 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangazo la Natija ya Kuutafuta Mwandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wa Mwaka 1443 Hijri


(Imetafsiriwa)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi  Kurehemu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliyeteremsha Qur'an na akatuchagulia Uislamu kuwa ndio Dini yetu, na rehma na amani zimshukie yule aliye anzisha Umma wa Kiislamu, bwana wa viumbe, bwana wetu Muhammad na juu ya familia yake na maswahaba zake wote.

Imepokewa kutoka kwa Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad bin Ziyad kwamba amesema: “Nilimsikia Abu Hurairah (radhi za Allah ziwe juu yake) akisema: Amesema Mtume (saw) au amesema Abu Al-Qasim (saw): «صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ»  "Fungeni kwa kuonekana kwake (mwandamo wa mwezi wa Ramadhan), na fungueni kwa kuonekana kwake (mwandamo wa mwezi wa Shawwal), ni ikiwa mawingu yatawaziba (kutouona mwezi), basi kamilisheni idadi ya siku thalathini za Sha'aban."

Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi wa Ramadhan iliyobarikiwa usiku huu, mkesha wa kuamkia Jumamosi, kuonekana kwa mwezi mwandamo kumethubutu kulingana na masharti ya muandamo wa Kishariah, katika baadhi ya nchi za Waislamu, kwa hiyo kesho, Jumamosi, ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhan wa mwaka 1443 Hijria.

Kwaa mnasaba huu, nafikisha salamu na pongezi zangu za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wote wanaofanya kazi ndani yake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, nikimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie na aharakishe ushindi kwetu na tamkini kupitia mikono yake.

Ramadhan mwaka huu inakuja katika wakati ambapo nchi za Magharibi zinajaribu kugeuza mashambulizi yake ya kimaadili, ambayo zimeyaendesha katika karne nzima ya maisha ya kibinafsi ya Waislamu, kuwa mashambulizi ya moja kwa moja dhidi yake. Baada ya kushindwa kwa kampeni ya "vita dhidi ya ugaidi" kuunda roho ya kusalimu amri katika Umma wa Kiislamu, na baada ya mshtuko wa mapinduzi ya Kiarabu ambayo watawala wa Magharibi walisibiwa nayo, yaliyogeuza meza dhidi ya vibaraka wao na kukaribia kuufukuza ushawishi wa Magharibi nje ya ardhi yetu, kwa kiwango ambacho mkuu wao alisema kwamba yalikigeuza kichwa chake kuwa na mvi! Baada ya mishtuko hii Magharibi ilitambua kwamba maumbile ya Uislamu na Waislamu yanaamuru kwamba kasi ya uasi wa Waislamu dhidi ya hali ya kikoloni itaongezeka mfululizo, na itaendelea kuongezeka hadi Waislamu pasi na budi waregeshe tena mamlaka yao.

Lakini suala la kutia shinikizo dhidi ya Urusi na kuzingirwa kwa China limekuwa suala la dharura kwa maslahi ya Magharibi inayoongozwa na Marekani. Hili lilihitaji kuondolewa kwa sehemu kubwa za vikosi vya kijeshi na vifaa vya Magharibi kutoka kwa nchi za Kiislamu. Lakini Magharibi haitaki kuuacha Umma wa Kiislamu upate pumzi yake wasije wakarudia tena vile vitendo dhidi ya vibaraka wao. Kwa ajili hiyo, wakaanza kuchukua hatua za kuwashughulisha Waislamu wenyewe kwa wenyewe, kwa kuyachezea maisha yao ya kibinafsi kote duniani; na kwa hili, wakahamasisha vibaraka na zana zote kuyabadilisha hadi watakaporegea. Walizidisha maradufu usawazishaji mahusiano kati ya watawala katika nchi za Waislamu na umbile la Kiyahudi, na wakaingiza makundi ya Mayahudi kwenye dola za Ghuba ya Kiarabu, na wakaanza kuishambulia ghariza ya dini katika ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu. Wakawafunga wanachuoni na wakaibadilisha Kamati ya Kuamrisha Mema kwa Kamati ya Burudani iliyozingira Al-Madina Al-Munawwarah na Makka Al-Mukarramah kwa machafu na maovu.

Aya za Qur’an ziliondolewa kwenye mitaala ya elimu nchini Jordan, wakaanzisha jambo hilo hilo katika mitaala ya Misri, na wakaingiza mitaala ya elimu hiyo katika maeneo yaliyokombolewa nchini Syria. Watawala wa Nyumba ya Saud waliondoa katika mitaala ya elimu yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alikuwa amewalaani Mayahudi kwayo. Mtawala wa Misri alianza kufufua ustaarabu wa kifirauni katika sherehe ya kimataifa ya miili ya mafirauni wa kifalme. Amerika iliwaachilia Mabaniani wenye chuki kuwatesa Waislamu katika Bara dogo la India, hivyo wakaichuna Kashmir na kuwafukuza Waislamu kutoka Assam na kuwanyima haki za kiraia idadi kubwa ya Waislamu nchini India, na kuanza kuwazuia wanawake wa Kiislamu kuvaa Khimar (hijab) kupitia nguvu ya idara ya mahakama na sheria.

Vile vile barani Ulaya, Ufaransa iliishambulia jamii yake ya Kiislamu, hivyo ilianza kwa kufunga misikiti na kutunga sheria za kuingilia jinsi Waislamu wanavyowalea watoto wao ndani ya nyumba zao. Ama nchi za Skandinavia zikiongozwa na Sweden zilizidisha mashambulizi dhidi ya familia za Kiislamu na kuanza kuwachukua watoto wa Kiislamu na kuwaficha kutoka kwa familia zao kwa visingizio vya uongo. Hili liliambatana, katika nchi za Kiislamu, na kuanza kwa mchakato wa kuanzisha vifungu vya CEDAW vya kuisambaratisha familia ya Kiislamu, hasa katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa kuharamisha ulezi wa baba juu ya familia yake na kuifanya familia na mkuu wa familia kuwa chini ya huruma ya wasio na maadili. Hatusahau madhihirisho ya kuwapokea wauaji wa Waislamu na wanyakuzi wa ardhi yao na heshima yao katika wiki za hivi karibuni; dhihirisho la kujifanyisha lililofurahiwa na rais wa umbile la Kiyahudi nchini Uturuki, hadi dhihirisho la urafiki aliopewa Bashar Assad nchini UAE, ambayo yalikuwa kama kumwaga chumvi kwenye kidonda cha Ummah mzima wa Kiislamu.

Enyi Waislamu… Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi:

Kafiri Magharibi isingeweza kufanya mashambulizi haya kama si watawala wa Kiislamu kufungua milango ya ardhi wazi kwa ajili ya kuwachezea wapendavyo. Kwa hiyo, upotovu huu wa maisha ya kibinafsi ya Umma wa Kiislamu hautasitishwa, isipokuwa uwe na Khalifa atakayewakusanya watu wake na kuwasaidia dhidi ya maadui zao, hivyo kuwasahaulisha minong'ono ya Shetani. Wamagharibi hawakutumia hatua hizi isipokuwa kwa sababu walitambua masuala mawili muhimu: La kwanza ni kwamba Umma wa Kiislamu bado unafanya uasi juu ya masharti yake na unataka kuregesha mamlaka yake na kuufukuza ushawishi wa Magharibi kutoka katika ardhi yake. Pili ni kwamba masuala ya Urusi na China yatawavuruga Wamagharibi kutoka katika nchi za Kiislamu, na kwa hiyo wakawakabidhi jukumu hilo watawala vibaraka. Hivyo basi, fursa imeiva kwa Ummah kujiondoa wenyewe kutoka kwa vibaraka wa Magharibi na khiana zao, kuachwa huru kutokana na ushawishi wao na kuichukua ardhi yake mikononi mwake. Jambo hili liko kwa watu wenye nguvu na ulinzi ndani yake, na msaada wa rai jumla miongoni mwao. Basi fanyeni hima, enyi Waislamu, katika mwezi huu uliobarikiwa, na muwasukume wenye nguvu na ulinzi miongoni mwenu kutoa Nusra (msaada wa kimada) kwa Uislamu, waweke mikono yao mikononi mwa Hizb ut Tahrir, kwa kutaraji kwamba Mwenyezi Mungu (swt) itatoa ushindi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

Ima hili, au mtazongwa na fedheha duniani na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) kesho Akhera! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً   فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»  "Hakuna mtu yeyote (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mwengine katika sehemu ambayo heshima yake inachafuliwa na utu wake kukiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika sehemu ambayo angependa kupata Nusra yake, na hakuna mtu yeyote (Muislamu) atakayemnusuru Muislamu mwengine katika sehemu ambayo heshima yake inachafuliwa na utu wake kukiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru katika sehemu ambayo angependa kupata Nusra yake." [Imesimuliwa na Abu Dawood]. Hili ni kwa mtu mmoja, basi, enyi watu wenye nguvu na ulinzi, vipi kuhusu yule aliyefelisha Umma mzima wa bilioni mbili?! Mcheni Mwenyezi Mungu katika matukufu ya Waislamu, mcheni Mwenyezi Mungu kabla hamjachelewa.

Kwa kutamatisha, tunaulingania Umma wa Kiislamu katika mwezi huu mtukufu uufanye mwezi wa Ramadhan mwaka huu kuwa ni mwanzo mpya wa ahadi kwa Mwenyezi Mungu (swt), katika kufuata haki, hata kama Magharibi na vibaraka wake wanachukia, na wafurahie ushindi wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Naomba mwezi wenu uwe wa baraka, Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh.

Mkesha wa Jumamosi siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhan wa mwaka 1443 H.

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu