Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 024
M.  Jumatatu, 12 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kumbukumbu ya Kugawanya Pakistan na Bangladesh ni Kumbukumbu Chungu Waislamu lazima Waziunganishe tena kama Dola Moja
(Imetafsiriwa)

Wakati wa siku hizi, mnamo 1971, Pakistan iligawanywa katika sehemu mbili, ya kwanza iliitwa Pakistan, na nyingine, Bangladesh, baada ya kuwa wameunganishwa kama umbile moja kwa karne nyingi. Mgawanyiko huu ulitekelezwa kulingana na mpango chungu wa Waingereza, ambao ulitaka kugawanywa kwa Bara Hindi Dogo katika dola nyingi, ili Uingereza iweze kuyadhibiti kwa urahisi, kwa gharama ya chini, kutoka mbali, kupitia watawala ambao ni vibaraka wa London, walioteuliwa juu ya dola hizi. Hii ilikuwa baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kijeshi katika eneo hilo mwaka wa 1947. Kwa hiyo Uingereza yenye nia mbaya ilichochea vita na mizozo kati ya makabila na dini, ambazo zilikuwa zimeishi pamoja kwa amani kwa karne nyingi, bila migogoro au mifarakano. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kulazimisha mradi wa Uingereza wa mgawanyiko, kwa watu hao, wa dini na makabila mbalimbali. Mpango wa kugawanya ulitekelezwa kindani na watawala na viongozi, ambao walinadiwa kwa watu wa Bara hilo dogo kama viongozi mashujaa. Lakini, kiuhalisia walikuwa ubunifu wa wakoloni Waingereza, katika moyo na roho. Wengi wao walikuwa ni wale waliosoma na kukulia katika shule na vyuo vikuu vyake. Wafadhili wa mchakato wa mgawanyo wa dola walikuwa Uingereza, Amerika na China, nchi tatu ambazo zimekuwa zikihofia Umma wa Kiislamu na umoja wake.

Enyi Waislamu wa Bara Hindi Dogo, India, Pakistan na Bangladesh! Mwenyezi Mungu (swt) amesema, (إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ)  “Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Surah Al-Anbiyya 21:92]. Mwenyezi Mungu (swt) amesema, (إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ) “Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Surah Al-Hujraat 49:10]. Nyinyi mnatokana na Umma mtukufu nao ni Ummah wa Kheri, kama ulivyosifiwa na Muumba wake, Mwenyezi Mungu (swt), (كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ) “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu.” [Surah Aali Imran 3:110]. Uislamu mtukufu umekuunganisheni, ukiyeyusha vizingiti vya kikabila na kitaifa baina yenu, ukiwafinyanga ndani ya kinu chake, kama wamoja. Hakuna mbora kwenu, juu ya wengine, isipokuwa kwa Taqwa (uchaMungu), ikithibitishwa na hadith ya Mtume (saw),

«يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَلَا إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ وَإِنَّ أَبَاكُمْ وَاحِدٌ أَلَا لَا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ عَلَى أَعْجَمِيٍّ وَلَا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ وَلَا لِأَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ وَلَا أَسْوَدَ عَلَى أَحْمَرَ إِلَّا بِالتَّقْوَى»

Enyi wanadamu. Jueni hakika Mola wenu Mlezi ni mmoja tu, na hakika baba yenu ni mmoja. Jueni hakuna ubora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala asiyekuwa Mwarabu juu ya Mwarabu, wala kwa mwekundu juu ya mweusi, wala mweusi juu ya mwekundu, isipokuwa kwa uchamungu.” [Ahmed]

Enyi Waislamu katika Bara Hindi Dogo! Mwenyezi Mungu (swt) amewabariki kwa Uislamu, hivyo mulipata kitambulisho chake na kuunganishwa chini ya utawala wake, kwa karne nyingi. Msidanganywe na Magharibi na vibaraka wake leo, ambao wanatia minong'ono ya mifarakano kati yenu, wakichochea fitina za ujinga baina yenu. Imepokewa kutoka kwa Abu Dawud kwamba Mtume (saw) alisema:

«لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ»

“Sio katika sisi yule anayelingania asabiyya, na si katika sisi anayepigana kwa ajili ya asabiyya, na si katika sisi anayekufa kwa ajili ya asabiyya.” Na yeye (saw) pia ametuonya kuhusiana na utaifa, «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Uacheni hakika huo ni uvundo.” [Bukhari na Muslim]. Na yeye (saw) amesema, «مَنْ تَعَزَّى بِعَزَاءِ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَعِضُّوهُ وَلَا تَكْنُوا» “Yeyote mwenye kujipamba na ujahiliya, basi mwambieni aing’ate tupu ya babake. Wala msizungumze kwa mafumbo.”

Enyi Waislamu wa Pakistan na Bangladesh! Mwenyezi Mungu (swt) amesema Kweli aliposema (swt),

(وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ)

“Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Surah Al-Maida 5:2]. Je, ni Taqwa (uchamungu) ipi iliyo bora zaidi kuliko Muislamu kuungana na ndugu yake Muislamu, chini ya hukmu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt)? Hakika wapo wale walio bora kuliko sisi sote waliotutangulia katika hili. Muhajirina (wahamiaji) waliungana na Ansari (waliowanusuru), baada ya makabila ya Aws na Khazraj kuungana. Hii ilikuwa baada ya uadui na vita kutawala katika hali baina yao, vikiteketeza kila kitu na bila kuacha chochote, huku watu wengi wakiuawa kwa sababu hiyo. Ushirikiano baina ya Waislamu, kwa kuungana baina yao, ni moja ya matakwa ya kumcha Mwenyezi Mungu (swt), taqwa. Kwa hivyo, sisi katika Hizb ut Tahrir tunakulinganieni kuungana chini ya bendera ya Tawhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), لا إله إلا الله محمد رسول الله “Hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Kwa nuru ya Khilafah ya Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, ambayo kurudi kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara njema juu yake, tunakulinganieni muweke mikono yenu katika mikono yetu, na museme kama Ansari (ra) walivyosema waliposikia kutoka kwa Mtume (saw), «وَلَا يَسْبِقَنَّكُمْ إِلَيْهِ...» “Wala asikutangulie yeyote katika hili...” Basi hakikisheni kuwa nyinyi ndio watangulizi katika kusimamisha Khilafah katika nchi yenu, kabla ya wengine kukutangulieni katika kusimamisha Khilafah katika nchi yao. Musisite kufanya kazi nasi, mpaka mupate heshima ya dunia hii na Akhera.

Enyi Vikosi vya Kijeshi vya Pakistan na Bangladesh! Nyinyi ndio watu wa nguvu na ulinzi katika Ummah wenu. Kama vile Ansari (wasaidizi wa kinguvu) walivyoitwa Ansari wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu walimnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), kuanzisha Dola ya Kiislamu mjini Madina, pia ni wajibu wenu kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na wale wanaofanya kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu katika nchi zenu. Waislamu wa Bara Hindi Dogo, nchini India, Pakistan na Bangladesh, wana shauku kubwa ya kuregea katika utawala wa Uislamu, kama vile wanavyotamani umoja baina yao. Kwa umoja wao chini ya utawala wa Uislamu, pamoja na uongozi wa Hizb ut Tahrir, wataunda nukta madhubuti ya kuinusuru Dola ya Khilafah Rashida, ambayo itawaunganisha Waislamu wote katika Bara Hindi Dogo, kwa mara nyingine tena. Hivyo basi, eneo hili litakuwa ni nukta kitegemeo ya kuunganishwa kwa nchi zote za Kiislamu zilizo koloniwa, ambazo kwa sasa zinatawaliwa na watawala waovu, kuanzia Indonesia upande wa Mashariki, hadi Morocco na Andalusia upande wa Magharibi.

Enyi Askari wa Jeshi, Enyi Wajukuu wa Muhammad bin Qasim! Jueni kwamba munao uwezo wa kutoa Nusrah (msaada wa kinguvu) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah. Jueni kwamba munao uwezo wa kukabiliana na changamoto zote anuwai, zinazowezekana, kwani nyinyi munatoka kwenye Ummah wa Jihad na mapambano. Ndani ya Ummah huu, kuna wanaume miongoni mwa wanaume. Ndani ya Ummah huu kuna neema, mali na rasilimali ambazo zitaifanya kuwa dola inayoongoza duniani, ndani ya miaka michache. Msijinyime fursa ya kupata radhi za Mola wenu Mlezi, ili mfike Pepo yake pamoja na Ansar (wasaidizi wa kinguvu) waliopita.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal 8:24]

Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu