Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  15 Muharram 1445 Na: 1445 H / 001
M.  Jumatano, 02 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mapinduzi ya Niger na Upotezaji Endelevu wa Dira wa Majeshi ya Waislamu
(Imetafsiriwa)

Alhamisi iliyopita, Walinzi wa Rais nchini Niger walifanya mapinduzi dhidi ya serikali hiyo, kwani walitangaza katika taarifa iliyopeperushwa na runinga kwamba walikuwa wamemfukuza Rais wa Niger Muhammad Bazoum, na kuunda Baraza la Kitaifa kwa ajili ya Ulinzi wa Nchi linaloongozwa na Jenerali Abd al-Rahman Chiani, na punde tu Jeshi liliwafuata kwa kutangaza uungaji mkono wake kwa viongozi wa mapinduzi. Taarifa ya viongozi wa mapinduzi ni pamoja na ahadi ya "kuheshimu majukumu yote yaliyochukuliwa na Niger" na kutoa uhakikisho kwa jamii ya kitaifa, kimataifa na kieneo "kuheshimu hadhi ya kimwili na kimaadili ya mamlaka iliyobanduliwa."

Inasikitisha kwamba viongozi wa majeshi ya Waislamu bado wanabaki kupoteza dira yao, na kwamba hawajaacha itikadi ya utiifu iliyowekwa juu yao na mataifa ya kikoloni. Sasa, viongozi wa jeshi nchini Niger wanafanya mapinduzi dhidi ya serikali, lakini wanafanya hivyo ndani ya mfumo wa utiifu kwa dola za kikoloni.

Vitendo vya jeshi nchini Sudan ni ushahidi bora wa utegemezi huo. Je! Majenerali wanawezaje kuwa na uwezo na tayari kutoa maagizo kwamba miji ya nchi yao imiminiwe makombora na mizinga, na hivyo kuwaondoa watu wao majumbani mwao kwa mikono yao wenyewe? Lakini hawasubutu kuchukua hatua hata moja nje ya mzunguko wa kisiasa ambao dola ya kikoloni inawachorea?! Je! Viongozi hawa watabaki kuogopa kutoka chini ya kifuniko cha kisiasa cha wakoloni mpaka lini, hadi kivuli cha kifuniko cha kisiasa kinachotokana na Ummah wao?!

Je! Viongozi wa majeshi hawakugundua baada ya kile dola za kikoloni zilizowaamuru kuwa ni usaliti wa Ummah wao na wataadhibiwa na moto wa jahannam? Na kwamba kile Mwenyezi Mungu (swt) alicho nacho ni haki kamili ambayo itasababisha pepo pana kama mbingu na ardhi?!

Je! Makamanda wa majeshi hawakugundua kuwa Ummah wa Kiislamu ni Ummah jasiri, mkarimu na mwaminifu kwa viongozi wake? Badala yake, unajivunia wale ambao ni wenye busara na waadilifu kati yao, na huwaita watoto wake kwa majina yao kwa heshima yao na uaminifu kwa kile walichotoa kwa Uislamu na Waislamu?!

Je! Makamanda wa majeshi hawakugundua kuwa Ummah wa Kiislamu una hamu ya kuregelea mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, na kwamba Khilafah imekuwa rai jumla kwa hilo?!

Je! Viongozi hawa wataanza lini kufikia maslahi ya Waislamu? Je! Watatangaza lini kujitenga kwao na ukoloni na uovu wake, na kuunusuru Uislamu na watu wake? Mwenyezi Mungu (SWT) asema:

[وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj 22:40].

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunatoa wito kwa wote wenye ikhlasi, na haswa watoaji maamuzi kutoka miongoni mwa wamiliki wa majukwaa na tovuti, kutekeleza jukumu la kuunusuru Uislamu na Waislamu kwa viongozi wa majeshi; Kwa sababu wana uwezo wa kurekebisha dira ya majeshi ya Waislamu. Na kuujulisha Ummah juu ya kadhia yake nyeti, ambayo ni kusimamisha Khilafah, na kwamba kusimamishwa kwake ni jukumu la viongozi wa majeshi ya Waislamu, ili Ummah awazunguke katika jukumu hili. Kuonyesha ukweli huu kwa Ummah inatosha kuharakisha kuongezeka kwa utambuzi wa kadhia yake nyeti. Kwa hivyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu harakisheni kwa ajili ya Uislamu na Waislamu, Enyi watoaji maamuzi katika Ummah wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَيَزِيدُ اللهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى]

“Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu.” [Maryam 19:76].

Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu