Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 29 Ramadan 1445 | Na: 031 / 1445 H |
M. Jumatatu, 08 Aprili 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangazo la Matokeo ya Kuutafuta Mwandamo wa Mwezi wa Shawwal 1445 H
Pongezi za Idd Al-Fitr Al-Mubarak
(Imetafsiriwa)
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Alhamd
Bismillahi Ar-Rahman Ar-Raheem. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu, na rehma na amani zimshukie bora wa mitume, bwana wetu Muhammad, na jamaa zake na maswahaba zake…
Amepokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba yeye amesema, nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema: kwamba Mtume (saw) amesema, au alisema: Abu Al-Qasim (saw) amesema:
«صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ» “Fungeni kwa kuuona mwezi (mwandamo) na fungueni kwa kuuona mwezi. Na ikiwa (kutokana na kutanda mawingu), mwezi utafichika kwenu, basi hesabuni siku thalathini.”
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi wa Shawwal katika mkesha huu uliobarikiwa wa Jumanne, mwandamo wa mwezi mpya haujathibitishwa kulingana na mahitaji ya Shariah. Kwa hivyo, kesho Jumanne ni kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Mwenyezi Mungu akipenda, na siku inayofuata kesho Jumatano, itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd al-Fitr iliyobarikiwa.
Kwa mnasaba huu, Hizb ut Tahrir inawapa Umma wa Kiislamu pongezi zake za dhati kwa sikukuu ya Idd al-Fitr iliyobarikiwa, na kumuomba Mwenyezi Mungu airegeshe mwakani, ilhali dola yake ikiwa tayari imeshasimama, ambapo Mwenyezi Mungu ameipa nguvu dini yake, na kueneza neno lake. Vile vile, natoa pongezi maalum, kwa niaba yangu na kwa niaba ya Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, nikimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amjaalie mafanikio katika kutekeleza wito huu wa kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ya kuasisiwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Idd al-Fitr inakuja mwaka huu, huku mapambano ya dhamira kati ya Umma wa Kiislamu na wakoloni makafiri wa Magharibi yakionekana tofauti na miongo mingi. Umma wa Kiislamu umeuthibitishia ulimwengu kwamba bado umedhamiria kuwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni ardhi ya Kiislamu na hautaiacha hata kama mkoloni kafiri Magharibi atajaribu kuikandamiza. Kwa hakika, Magharibi leo inaogopa kwamba tukio la Oktoba 7, 2023, lirudiwe tena na kutishia uwepo kwa umbile la Kiyahudi, ambalo limeonekana kuwa dhaifu, kwani lingekuwa karibu kuangamizwa lau upinzani wa pili ungefunguliwa dhidi yake kwa kuhamasisha majeshi ya Kiislamu kuinusuru Gaza, watu wake, na Palestina yote... Hii ndiyo sababu Magharibi ina ukali sana katika kampeni yake isiyo na aibu ya kuunga mkono umbile la Kiyahudi kwa silaha na usaidizi wa kimaadili na vikwazo kwa Waislamu wa Magharibi na katika nchi za Kiislamu mikononi mwa watawala wasaliti.
Ama mujahidina mashujaa wa Gaza na watu wao waliokuwa na subira kama majabali, walikanyaga pua za jeshi la Kiyahudi katika mchanga wa Ardhi Iliyobarikiwa. Waliuthibitishia ulimwengu kwamba endapo Uislamu utamiliki moyo wa watu, huwainua watu hao kwenye nafasi ya juu katika historia ya Uislamu na Waislamu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye uwezo, ayakubali matendo yao na ayaweke kesho Akhera katika viwango vya juu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Anasema (swt):
[قَالَ اللهُ هَذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً رَّضِيَ اللهُ عَنْهُمْ وَرَضُواْ عَنْهُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * لِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Naye ni Muweza wa kila kitu.” [Al-Ma’idah 5:119 – 120].
Ama kwa watu wengine wa Umma wa Kiislamu, walihisi gereza linaloitwa "mpaka wa Sykes-Picot" kama ambavyo hawajawahi kuhisi hapo awali. Waislamu ni Ummah mmoja, damu yao ni moja, na hisia zao ni moja. Vilio vya wanawake huru, vilio vya watoto, na nusra kwa wazee viliwasha moto wa udugu wao. Lakini wanabaki kuwa watu waliofungwa nyuma ya gereza linaloitwa mpaka wa Sykes-Picot.
Gereza la Sykes-Picot liliundwa kwa madhumuni haya haya, ambayo ni kuwatenga Waislamu na kuwazuia kusaidiana wao kwa wao. Leo Palestina, jana Syria, kabla ya hapo Kashmir, kabla ya hapo Iraq, kabla ya hapo Afghanistan, na kabla ya hapo Palestina... Kila wakati watu miongoni mwa Waislamu wanauawa, huku mamilioni waliosalia wakitazama tu na hawawezi kusonga, na hiyo ni kwa sababu tu ya mipaka ya Sykes-Picot!
Enyi Askari katika Majeshi ya Kiislamu: Mumeona usaliti wa watawala, uaminifu wao wa kipofu kwa kafiri mkoloni Magharibi, jinsi wanavyokulazimisheni kuratibu usalama na maadui wa Umma wa Kiislamu, na jinsi wasivyokupeni amri ya kusonga isipokuwa kuiangamiza miji ya nchi yenu na kuwaua watu wenu ndani yake. Kwa hiyo, lazima muache kutoa uaminifu wenu kwa kundi hili la wasaliti, na muende mara moja kuinusuru Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na ikiwa watawala watapinga, ni sababu ya nyinyi kukabiliana nao kwa kila njia. Umma utakuwa pamoja nanyi kwa ajili ya kukunusuruni kwa pesa na maisha, na Hizb ut Tahrir pia inakunyoosheeni mkono, kwani imetayarisha mambo muhimu kwa ajili ya kurejesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hili halitapatikana isipokuwa kwa kuwaunga mkono watu wa Nusra, kama walivyofanya Ansari, Mwenyezi Mungu awe radhi nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) walipompa bayah (ahadi) ya kusimamisha utawala wa Uislamu miongoni mwao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُوْلَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]
“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal 8:74].
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La illaha illa Allah… Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahil Hamd
Idd Mubarak Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu
Mkesha wa Jumanne ndio kukamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka wa 1445 Hijria sawia na Aprili 9, 2024 M.
Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |