Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445 / 041
M.  Jumapili, 16 Juni 2024

Pongezi za Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1445 H

(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd

Bismillahi Ar-Rahman Ar-Raheem. Sifa njema zote zamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu, na rehma na amani zimshukie mbora wa mitume, bwana wetu Muhammad, na jamaa zake na maswahaba zake.

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao... utulivu unaowastaajabisha makafiri wenye chuki, unaoeleweka tu na Waislamu ambao nyoyo zao zimeshikamana na radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Vile vile ninafuraha kutoa pongezi zangu na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, nikimwomba Mola Mtukufu aukirimu Ummah wa Kiislamu kwa ushindi na tamkini mikononi mwake.

Idd al-Adha ya mwaka huu inafika wakati Umma wa Kiislamu unahisi uzito wa ukoloni juu ya mabega yake katika kila kona ya dunia hii. Kuanzia jinai zinazoendelea dhidi ya watu wa Gaza na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, hadi kuteswa kwa Waislamu nchini India na Kashmir, vita vya wakala vinavyoteketeza miji na watu wa Sudan, sera ya udhalilishaji ya kimfumo inayotekelezwa dhidi ya watu wa Syria popote walipo, hadi kwenye sera ya kuvua utukufu wa Uislamu kutoka kwenye Rasi ya Uislamu, hadi kwenye ukandamizaji wa kila anayeiunga mkono au kuihurumia Gaza katika nchi zinazoizunguka na Magharibi; katika dhurufu hizi za ukoloni, Waislamu wanakaribisha Idd yao mwaka huu.

Enyi Waislamu, Umma Bora ulioletwa kwa Wanadamu:

Vita vinavyoendelea katika ardhi ya Gaza ni onyo kwenu juu ya uovu na hila anazoziweka mkoloni kafiri wa Kimagharibi kwa ajili ya ardhi zenu zote. Nchi za Magharibi hazitazuiliwa kuingilia kati maisha yenu hadi mtakapokata mkono wake kutoka katika ardhi, na hamtaweza kufanya hivyo isipokuwa mregeshe mamlaka yenu kutoka kwa watawala vibaraka. Mamlaka yenu hayataregeshwa isipokuwa kwa wana wenu kutoka kwa watu wenye uwezo na nguvu katika majeshi yenu, kwani hakuna hadhi kwa Umma ulioacha mamlaka yake. Msidanganywe na uongo wa watawala na vinywa vyao kuwa hali hiyo haimkiniki; haya ni maneno ya kila dhalimu anayewadanganya watu wake ili kuwafanya watumwa milele. Jueni kwamba Ummah una uwezo na rasilimali za kuchukua cheo cha dola inayoongoza, ambayo haiwezi kuchezewa kuhusiana na maslahi yake, na ina uwezo na rasilimali za kutosha kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Mujahidina wa Gaza wametoa ushahidi kwa Ummah mzima, hasa kwa majeshi yake, kwamba Mayahudi na umbile lao si lolote mbele ya wale waliojitayarisha. Hata Marekani na silaha zake hazitoshi kushinda kundi dogo la wapiganaji wa Umma wa Kiislamu, basi vipi kuhusu majeshi ya nchi zinazoizunguka ambayo idadi yao ni mamilioni?!

Enyi Waislamu, Enyi Watu Wenye Majukwaa, Vyeo na Vyombo vya Habari:

Kuna ukweli mmoja, nao ni kwamba ardhi za Waislamu bado zinateseka chini ya ukoloni, hivyo musisite kuuweka wazi ukweli huu. Hiki ndicho kiini cha ukosefu wa usalama katika ardhi zenu. Msiwaache watu wa Ummah wa Kiislamu wapotee kwenye ukweli huu. Badala yake, uchocheeni Ummah kuwata watu wenye madaraka na nguvu kuwaondolea hali hizi za kikoloni kwa kuwaondoa watawala vibaraka. Umma wa Kiislamu lazima uwe na dola moja inayoukusanya pamoja na uwezo wake wote na kuziunganisha nyoyo zake, Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume. Sisi katika Hizb ut Tahrir tunakualikeni mupitie yale ambayo Hizb imetayarisha, kutoka katika Quran na Sunnah, kama mradi wa kusimamisha Khilafah hiyo upya.

Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Kiislamu:

Je, munahifadhia nani silaha, vifaa na mafunzo yenu ikiwa si kwa ajili ya kupigana na maadui wa Umma wa Kiislamu? Je, munangoja amri kutoka kwa watawala wasaliti? Maagizo ya watawala hawa yatakuwa tu kuua watu wenu wenyewe na kuharibu nchi zenu wenyewe, so kupigana na adui yenu na kukomboa ardhi yenu. Tazameni jinsi wanavyokuhamasisha kushambulia miji yenu huku wakikuonya dhidi ya kuhama kupigana na umbile la Kiyahudi na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina! Hakika, munawajua kwa karibu! Jinsi wanavyotii kile ambacho Marekani inakitaka na kile anachokipenda mkoloni kafiri Magharibi, huku wakijilazimisha kwa kiburi juu ya watu na matarajio yao. Hizb ut Tahrir inakuiteni kuwa upande wa Uislamu na Umma wa Kiislamu, kuiondoa nchi hii katika khiyana ya watawala hawa, kukata mkono wa kikoloni, na kutekeleza Shariah ya Mwenyezi Mungu kwa kutangaza Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kisha muendelee kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina chini ya uongozi wa Khalifa wa Waislamu, huku Waislamu wakiwa nyuma yenu wakiunga mkono na kutukuza Nasr (ushindi) wa Mwenyezi Mungu.

Enyi Waislamu:

Ni Idd al-Adha, kwa hivyo muombeni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ifanyeni furaha ya Idd iwe kuamsha upya azma yenu na chanzo cha hasira kwa adui yenu. Kisha unganeni mikono na Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa kazi ya bidii ya kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema, ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴾ “Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. * Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” [Muhammad:7-8].

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah... Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa

lillahi Alhamd.

Eid Mubarak. Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu.

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu