Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 2 Jumada II 1446 | Na: H 1446 / 060 |
M. Jumatano, 04 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala wa Bara Arabu Wanashindana katika Ufisadi na Utiifu kwa Maadui wa Ummah!
(Imetafsiriwa)
Siku chache zilizopita, watawala wa Imarati walijigamba juu ya uhamasishaji wao mkubwa wa kuwafikia wauaji wa Rabbi wa Kiyahudi, Zvi Kogan, kwenye ardhi zao, na kupongeza umakini wa vyombo vya usalama na kasi ya taratibu zao zilizochangia kufichua tukio hilo, baada ya huduma hizi zote kufanya kwa muda wote, kulingana na yale yaliyoelezwa katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati huo huo, Imarati na Wizara yake ya Ulinzi haikujitolea kuwanusuru zaidi ya mashahidi elfu 44 na elfu 104 waliojeruhiwa huko Gaza, ingawa muuaji wao anajulikana na haihitaji uchunguzi au umakini wa vyombo vya usalama kumfikia.
Haikupita hata siku chache tangu jinai ya watawala wa Al Saud dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa na ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu, pale walipoleta waimbaji na wanamitindo kama sehemu ya matukio ya Msimu wa Riyadh 2024 kujitokeza jukwaani wakiwa uchi, bila aibu au fedheha hata kidogo mbele ya Mwenyezi Mungu au watu wa Gaza na Lebanon, na bila kujali hata mayowe ya waliofiwa, kuugua kwa watoto, makumi ya maelfu ya mashahidi na mirundo ya vifusi.
Matukio haya mawili ni ncha tu ya upotovu wa watawala wa Bara Arabu, ambao umekuwa ukiendelea kwa miongo kadhaa na umeshika kasi katika miaka ya hivi karibuni kwa namna ya kushangaza na isiyo na adabu.
Kwa miaka mingi, watawala wa Imirati wamefungua mlango wazi wazi wa kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na kufungua nchi hii kwa ajili ya Mayahudi wanyakuzi na kuwajengea mahali pa ibada katika Bara Arabu. Walikuwa miongoni mwa watia saini mashuhuri wa Makubaliano ya Abraham, ambayo yanalenga kuhujumu Uislamu na kufisidi dini ya Waislamu. Wanaendelea kutoa huduma zao kwa Amerika na Mayahudi kutekeleza mpango wa baada ya vita mjini Gaza, ambao unalenga kuhakikisha kuwa Waislamu hawainuki huko.
Ndivyo ilivyo pia kwa watawala wa Al Saud ambao wanakimbizana na wakati ili kuingiza ufisadi na uovu katika ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu, kwa kuandaa mambo machafu na maovu. Wameazimia sana kueneza uchafu kiasi kwamba wameunda shirika zima ambalo linatumia mabilioni ya riyal kila mwaka, ambalo wanaliita Mamlaka ya Burudani. Shirika hili huwa mwenyeji wa waimbaji wa kiume na wa kike kuimba nyimbo za kashfa na uchafu katika tafrija zenye kelele, densi mchanganyiko, na kuandaa hafla mbalimbali kwa jina la mashindano, ambayo lengo lake ni wanawake kuonekana uchi, na wanaume kuchanganyika na wanawake. Hivi majuzi, tumeona jinsi watawala wa Al Saud wanavyotangaza kwa uwazi utayari wao wa kusawazisha kikamilifu mahusiano na umbile la Kiyahudi kwa badali ya idhini yake ya kuanzishwa dola dhaifu ya Palestina chini ya robo ya eneo la Palestina.
Kuwa Umma wa Kiislamu umechoshwa na watawala hawa Ruwaybidha (wazembe wajinga) na khiyana na jinai zao, ni lazima uharakishe kujiondolea wao uovu wao na ufisadi wao. Tunawakhasisisha watu wenye ikhlasi wenye nguvu na ulinzi, ili waharakishe kutimiza matumaini ya Ummah wao katika kuukomboa kutokana na adhabu, ufisadi na dhiki ambayo watawala wameuletea. Anasema Mwenyezi Mungu (swt):
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |