Alhamisi, 02 Rajab 1446 | 2025/01/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  14 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 065
M.  Jumatatu, 16 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mabadiliko ya Kweli Yanaweza Tu Kuja Kutokana na Mradi Unaotokana na Aqidah ya Ummah. Ni nani Aliye Nao?
(Imetafsiriwa)

Umma wa Kiislamu umeishi kwa karne moja katika unyonge na udhalilishwaji, mfarakano na mgawanyiko, na utegemezi kwa nchi kubwa. Hii inatokana na matendo ya watawala Ruwabidha (wajinga watepetevu) ambao hawaheshimu udugu au ahadi yoyote, wanachojali tu ni kubakia kwenye viti vyao vibovu (vya utawala), kutekeleza mipango ya nchi za Kikafiri katika ardhi zetu ili kukazanisha udhibiti wao juu yetu na kupora mali zetu. Wamesimama dhidi ya kila mtu anayewapinga au kutokubaliana nao, au kujaribu kuwabadilisha, na kuwaweka chini ya kifungo, mateso, mauaji, na ukiukaji wa matukufu. Bashar al-Assad na utawala wake wa kihalifu sio wa mwisho wao, ambaye uhalifu dhidi ya watu wake ulifichuliwa na matukio ya hivi majuzi nchini Syria, uhalifu ambao ni wa aibu na kuwafukuza wale wenye maumbile yaliyo sawa.

Ummah umefanya mapinduzi mengi kwa ajili ya mabadiliko, lakini hakuna hata moja yao yaliyofaulu. Mapinduzi ya Kiarabu, ambayo yalilipuka kwa nguvu katika idadi kadhaa ya nchi za Waislamu, yalidhibitiwa kwa mafanikio na nchi za makafiri na kugeuzwa kutoka kwenye mkondo wao. Sasa mapinduzi ya Ash-Sham yamefanikiwa kumuondoa Bashar al-Assad na familia yake, lakini swali ni: Je, watu wa Ash-Sham wameuondoa utawala wake? Na wameweka mradi wa kweli wa mabadiliko?

Mabadiliko ya kweli katika nchi zenu, enyi Waislamu, yanaweza tu kutokea kupitia mradi unaotokana na Aqidah (itikadi) yenu ya Kiislamu. Kupitia kwayo munasimamisha sheria ya Mola wenu Mlezi na kubeba ujumbe wake kwa watu. Mutamridhia Mola wenu Mlezi, na kupitia kwayo mtapata tena mamlaka yenu, mtarudisha mali zenu, mtahifadhi maisha yenu na heshima yenu, na mtapata heshima na hadhi mliyoipoteza tangu kuvunjwa kwa Khilafah. Mtakomboa kile kilichokaliwa kimabavu katika nchi zenu, mtawafukuza maadui zenu, na kuwazuia wasiwadhibiti. Mradi huu unahitaji masharti mawili kwa yeyote anayeubeba na anayetaka kuutekeleza: ikhlasi na mwamko wa kisiasa. Ni lazima awe mkweli kwa Mwenyezi Mungu (swt) Mtume wake (saw) na Ummah. Asitafute kumridhisha yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt), na wala asiiuze Dini yake au Ummah wake kwa pato dogo linalopita. Na kuwa na mwamko wa kisiasa unaomzuia kuburuzwa nyuma ya mipango na vitimbi vya nchi kubwa, na kutodanganyika na hila na michezo yao ya kisiasa, na kutokubali chochote isipokuwa kutekeleza mradi unaotokana na Aqida ya Ummah, hata iweje magumu anayokabiliana nayo, na bila kujali njama kiasi gani wanazopanga dhidi yake.

Hizb ut Tahrir ni kiongozi asiyewadanganya watu wake, na yeye ndiyo yenye mradi huu unaotokana na Aqidah yenu; mradi wa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Inatambulika kikamilifu kwa ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu (swt) Mtume Wake (saw) na kwa Ummah. Imejitolea na inaendelea kujitolea ili kuweka mradi wake kivitendo na utekelezaji. Ina ufahamu wa kisiasa ambao kwao inafichua njama za nchi kubwa na mashirika yao ya kijasusi, na njama zao haziihadai. Haikubali kuacha hata sehemu ndogo ya mradi huu, hata kama ulimwengu wote utasimama dhidi yake.

Mradi wa Hizb ut Tahrir ni mradi wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara yake njema. Umechapishwa kwenye tovuti zetu mbalimbali na maelezo yake na ufafanuzi wake. Unajumuisha nyanja zote za maisha, kuanzia rasimu ya katiba na mifumo mbalimbali ya maisha: kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu... Tunatoa wito kwa Umma kuutabanni, na tunatoa wito kwake kusalimisha uongozi wake kwa mmiliki wa mradi wa kweli wa mabadiliko; Hizb ut Tahrir.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu