Matukio ya umwagikaji damu yanayojiri Mashariki mwa Ghouta na Idlib; Mtandao wa Kutetea Haki za Kibinadamu wa Syria umesema kwamba raia wapatao 370 wameuwawa Mashariki mwa Ghouta tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ukitaja kuwa miongoni mwa wafu ni watoto 63 na wanawake 72. Katika eneo la Idlib, hususan mji wa Sarakib, ambao ndio uliolengwa kwa dhoruba hii tangu mnamo 25 Disemba, Warusi na serikali ya kihalifu ya Syria zimemwaga chuki zake dhidi yake, ikitangazwa na baraza lake la mji kuwa eneo lililo kabiliwa na janga, ambapo idadi ya vifo mwezi Januari ilikuwa ni watu wapatao 30 na zaidi ya raia 60 kujeruhiwa. Hii ni ikiongezewa na kulengwa kwa mashule na mahospitali, ambazo idadi yake kubwa haziendeshi tena shughuli zake.