Bangladesh Haipaswi Kuyaangalia Mataifa ya Kibeberu ya Magharibi kwa Mafanikio na Ufanisi wake na Isiwe Mwathiriwa wa Siasa za Jografia za India na Marekani
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mshauri mkuu wa serikali ya mpito ya Bangladesh Dkt. Muhammad Yunus alitoa wito kwa viongozi wa kimataifa kuunga mkono ujenzi wa Bangladesh mpya wakati akizungumza kwenye mapokezi kando ya Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa jijini New York mnamo Jumanne. Mara tu baada ya hotuba hiyo, rais wa Marekani Joe Biden pia alisema ikiwa wanafunzi wa Bangladesh wanaweza kujitolea sana kwa ajili ya nchi yao, Marekani pia inapaswa kufanya zaidi.