Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari yenye kichwa: Makubaliano ya Nchi Nne (Quartet) ya Kusitisha Mapigano na Hatari ya Mazungumzo kwa Msingi wa Hadhara ya Kimagharibi
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tangu Quartet—ambayo inajumuisha sambamba na Amerika, Saudi Arabia na Misri na Imarati, ilipotangaza taarifa yake mnamo 12/9/2025 kuhusu mgogoro wa Sudan, watu wengi nchini Sudan wamegawanywa katika mikondo miwili: mkondo unaounga mkono taarifa ya Quartet inayotaka mazungumzo na suluhisho la kisiasa, kwa kisingizio kwamba inaleta amani, na mkondo mwengine unaosema unakataa kile kilichokuja katika taarifa ya Quartet, na kutaka kuendelea kwa vita. Na ijapokuwa pande zote mbili ni Waislamu, hawakuufanya Uislamu kuwa ndio msingi wa kutoka kwao katika kubainisha misimamo yao, wakati ilitakiwa hapo awali jambo hili litokee



