Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  10 Muharram 1443 Na: 1443 H / 01
M.  Jumatano, 18 Agosti 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kuamua Kuzuia Haki Msingi ikiwemo Elimu, za Waislamu wa Rohingya Hasina Msekula Afichua Sura Yake Ovu ya Unyama

(Imetafsiriwa)

Mnamo Agosti 12, 2021, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bangladesh ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ilitangaza kwamba Sheikh Hasina ameidhinisha sera ya kutoruhusu kuboresha viwango vya maisha vya kambi za wakimbizi wa Rohingya, achilia mbali kuwa na hifadhi zilizofungamanishwa na Bangladesh kufuatia ombi kutoka kwa Benki ya Dunia (WB) na mashirika mengine ya UN (The Daily Star, Agosti 13, 2021). Inajulikana vyema kuwa taasisi kama WB ambazo hujibu maslahi ya kijiografia ya haswa Amerika zina ajenda yao kinyama juu ya wakimbizi wa Rohingya. Lakini Hasina mkatili ameagiza kuweka hali ya maisha na huduma za kambi hizo za wakimbizi katika kiwango 'kilichodhibitiwa' na cha 'kimantiki'. Kwa maana nyengine, hali ya sasa ya maisha ya kutisha katika kambi hizi ambazo hazina maji safi na haki za kimsingi zote ni za 'kimantiki' kulingana na Hasina. Kwa upande mmoja, serikali imefunga kila njia ya wao kujitegemea, lakini kwa upande mwingine, serikali inasema hawawezi kubeba "mzigo" wao, huku wakipora mabilioni ya dolari za fedha za kigeni zilizopelekwa kwa ajili ya Waislamu wa Rohingya. Juu ya hayo, utawala wa Hasina haukusita kufichua sura yao mbaya kwa kunyima haki za kimsingi za kibinadamu katika kambi hizo duni na kukataa kuwapa Waislamu wa Rohingya elimu rasmi, mafunzo ya ufundi, na kuunda nafasi za kazi, wakitoa kisingizio kilemavu kwamba hii ingewashajiisha kukaa kwa kudumu nchini Bangladesh! Huku Waislamu kote ulimwenguni, na haswa watu wa Bangladesh, walijitokeza kwa hamu kuwasaidia Waislamu wa Rohingya, serikali ya kisekula ya Hasina iliwatenga kwa kisingizio kwamba wanaeneza ugaidi, na kuwazuia kujumuishwa katika jamii yetu kwa kuwafanya wahalifu na kujenga hisia za utaifa kwa watu kupitia vyombo vya habari vya kisekula. Mwezi Machi mwaka jana, watu 15 waliuawa na karibu 400 wakisalia kupotea katika moto mkali katika kambi ya Balukhali wilayani Cox's Bazar kwani wao, wengi wao wakiwa ni watoto na wazee, hawakuweza kukimbia nje ya kambi hizo kutokana na uzio. Sera ya Hasina ya 'kuwachukua' Waislamu wa Rohingya kwa kweli ni kifungo badala ya hifadhi, na maagizo haya ya hivi karibuni kutoka kwake yanaonyesha wazi wazi nia ya kishetani ya utawala wake kwa watu hawa wa Ummah wanaoteswa. Kwa hivyo, haishangazi kwa nini wakimbizi wengi ambao wamewekwa kizuizini katika Bhasan Char, 'kisiwa cha gereza' katikati ya bahari, wangali wanahatarisha maisha yao kutoroka kutoka huko. Kwa uchache wakimbizi 27 wa Rohingya walipotea baada ya mashua yao kuzama Jumamosi iliyopita, Agosti 15, wakati wa jaribio la kutoroka jela hili la kisiwa hiki.

Enyi Waislamu, lazima mupinge kampeni ya kueneza hofu ya serikali ya Hasina dhidi ya kaka na dada zetu wa Rohingya yenye lengo la kugeuza mshikamano wetu kuwa uadui kwao. Lazima musisahau,

[إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ]

“Hakika mimi ni katika Waislamu” [Surah Fussilat: 33].

Watawala hawa wa kisekula daima watacheza karata duni ya dola ya kitaifa ili kuhalalisha ukandamizaji wao kwa Waislamu wenzetu wa Rohingya. Chini ya uamuzi huu, Waislamu kama hao wanaoteswa watatumiwa kama biashara na mbuzi wa kafara kwa maslahi na mazungumzo kadhaa ya kinyama ya kisiasa ya kieneo. Ni kwa kusimamishwa tena Khilafah Rashidah wa pili pekee, ndipo tunaweza kuhakikisha haki kwao kwa kuwaruhusu kuishi mahali wanapotaka ndani ya dola ya Khilafah. Hapo zamani, Dola ya Khilafah haikuwahi kuamiliana na hata wasiokuwa Waislamu kwa mtindo huo wa kinyama. Sultan Bayazid II wa Khilafah Uthmani aliwakaribisha mara moja Mayahudi wa Sephardi waliofukuzwa kutoka Uhispania mnamo Julai 31, 1492. Sio tu kwamba aliwaokoa kwa vikosi vyake vya wanamaji chini ya amri ya Kemal Reis na kuwakaribisha, lakini pia alituma matangazo maeneo yake yote kwamba wakimbizi hao wapewe idhini ya kukaa ndani Dola ya Uthmani na kuwa raia. Umma mtukufu wa Muhammad (saw) unasubiri kwa hamu kurudi kwa Khilafah iliyoahidiwa ili kuleta afueni kwa wale wanaodhulumiwa na mateso yao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu