Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  8 Jumada II 1443 Na: 1443 H / 08
M.  Jumanne, 11 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ili kuwakomboa Waislamu wa Rohingya kutokana na Udhalimu wa Usekula, njia pekee ni kuwaweka chini ya Kivuli cha Khilafah

 (Imetafsiriwa)

Mamlaka za serikali ya Hasina hivi majuzi zimebomoa zaidi ya maduka 3000 ya Waislamu wa Rohingya katika kambi ya wakimbizi ya Kutupalong wilayani Cox's Bazar, na kuwaacha wakimbizi hao wasio na uwezo bila vyanzo vya mapato na mahitaji ya kila siku. Na ubomoaji huu ulitekelezwa ndani ya siku chache baada ya moto mkubwa uliozuka katika kambi hiyo ya wakimbizi na kuwaacha maelfu bila makaazi. Hata, kabla ya ubomoaji huu, mnamo Disemba 13, 2021, Kamishna wa Serikali wa Kutoa Msaada kwa Wakimbizi na Kuregesha Makwao alifunga maelfu ya shule za kijamii na za nyumbani kwa watoto wakimbizi wa Rohingya ndani ya kambi za wakimbizi ambapo takriban watoto 30,000 walikosa kupata elimu. Ni dhahiri kwamba utawala wa kihalifu hautawaruhusu Waislamu wa Rohingya kujitegemea. Wanataka wakimbizi wategemee misaada ya kigeni ili kuishi. Huku usaidizi wa kifedha wa kimataifa ukipungua kwa wakimbizi wa Rohingya, serikali hii ya kihalifu inazidisha mateso yao yaliyopo. Mgogoro wa Rohingya tayari umeiletea serikali faida kubwa ya kifedha katika suala la misaada na ruzuku, ambayo nyingi haziendi kwa wakimbizi masikini. Kwa watawala hawa wa kirasilimali wa kisekula, mgogoro zaidi hunamaanisha pesa zaidi. Watawala hawa kamwe hawabebi jukumu lolote, kwa kuwa hawaoni wajibu wa kulinda uhai na mali ya wanadamu - wakitazama kila kitu kwa msingi wa manufaa.

Na kulaaniwa kwa janga la kibinadamu la Rohingya na dola za Kimagharibi hakuna maana yoyote. Katika ardhi zao, wanatumia pia masaibu ya wakimbizi Waislamu ili kutimiza maslahi yao ya kiuchumi. Kwa nchi nyingine, kwa kweli, wanaruhusu mgogoro huu kuendelea kwa kimya kwani unatoa kisingizio cha kuingilia mambo yao. Vinginevyo, vipi utawala wetu kibaraka wa Magharibi utathubutu kuharibu riziki na fursa za kielimu za Waislamu wa Rohingya mara baada ya ziara ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu nchini Myanmar Tom Andrews ambaye aliiomba serikali ya Hasina kuhakikisha usalama na fursa za kujikimu kimaisha katika safari yake hiyo.

Enyi Watu wa Bangladesh! Hatuwezi kamwe kuondoa mateso ya Waislamu wa Rohingya isipokuwa tuondoe mfumo wa utawala wa kisekula pamoja na watawala katili zaidi unaowazalisha. Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal alifanya hili kuwa wajibu ili kuwasaidia Waislamu wenye shida:

 (وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ) “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia...” [Al-Anfal: 72]. Lakini serikali ya Hasina haijali kukiuka amri ya Mwenyezi Mungu (swt) kwani haiwakilishi Uislamu na Ummah. Wahalifu hao wanayafanya maisha ya Warohingya kuwa mabaya na mabaya kila siku badala ya kuwapa afueni kutokana na masaibu yao.

Enyi Watu Wenye Hekima na Muono! Tazameni nyuma kwenye historia ya mataifa na muone kama mtakuta chombo kingine chochote isipokuwa Khilafah ambacho kinasimamia kwa dhati mambo ya wanadamu? Hata Mayahudi wanaochukiwa sana walitafuta na kupata kimbilio la amani chini ya Khilafah Uthmani wakati Sultan Bayezid II alipowaokoa na jeshi lake la maji walipokuwa wakikimbia Amri ya Alhambra ya Uhispania mwaka 1492. Kwa hiyo, jitahidini sana kuiregesha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hakuna suluhisho jengine zaidi ya kusimamisha tena Khilafah ili kuwaokoa wanadamu kutokana na dhulma ya usekula.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu