Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  23 Safar 1444 Na: 1444 H / 06
M.  Jumatatu, 19 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

‘Kujizuilia’ dhidi ya Ujasiri wa Mashambulizi ya Makombora na Mauaji ya Mwezi Mzima kwenye Mpaka wa Bangladesh Yanayofanywa na Dola Dhaifu kama Myanmar Kunathibitisha Udhaifu wa Serikali ya Hasina katika Kulinda Ubwana wa Ummah kutokana na Utiifu kwa Mwalimu wake Mkoloni Uingereza

(Imetafsiriwa)

Usiku wa Septemba 9, kombora lililorushwa na jeshi la Myanmar lilimuua kijana wa Rohingya aitwaye Iqbal (17). Mapema siku hiyo hiyo saa sita mchana, mguu wa kijana wa Bangladesh ulilipuliwa na mlipuko wa mgodi katika eneo ‘Lisilo la nchi yoyote’ linalopakana na Tumbru. Lakini ni jambo la kusikitisha sana kwamba ingawa mamlaka ya nchi hiyo inatishiwa na uchokozi wa mwezi mzima na kurushwa risasi na Myanmar ndani ya Bangladesh, utawala huo wa kihaini haujaonyesha hisia kali kwao, achilia mbali kukabiliana na serikali hiyo dhaifu iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Jambo hili limewashangaza na kuwakasirisha watu wa nchi nzima. Serikali ya makhaini ya Hasina imeutaja kama mzozo wa ndani wa Myanmar ndani ya mpaka wao na kutaka Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kuingilia kati. Serikali ya Hasina imeonyesha sura yake mbaya huko nyuma kwa kuwatelekeza Waislamu wa Rohingya na kuunga mkono jeshi la Myanmar linalochinja kinyama. Waislamu wa Rohingya walipokimbia moto wa Myanmar na kukimbilia Bangladesh, serikali haini ya Hasina "iliwafunga" wakimbizi wa Rohingya na kutoa 'usalama' kwa jeshi la Myanmar ili wasiwe tishio lolote kwa Myanmar! Si hivyo tu, walivunjia heshima jeshi letu la Kiislamu kwa kuwapeleka kupanga paredi na jeshi ya kafiri la mauaji ya halaiki huko Myanmar. Kwa hivyo hata Jeshi la Myanmar livamie mpaka wa Bangladesh kiasi gani, Sheikh Hasina kamwe hatakuwa na misimamo mikali dhidi yao kwa sababu wote wawili Hasina na utawala wa kijeshi wa Myanmar wanadumisha utiifu wao kwa bwana wao wa kikoloni Uingereza. Kwa hivyo, serikali ya Hasina haitumikii chochote isipokuwa maslahi ya kijiografia ya bwana wake ambayo daima imekuwa ikiunga mkono utawala wa kijeshi wa Myanmar dhidi ya uingiliaji wa Marekani kupitia Aung San Suu Kyi. Hivyo basi Hasina ametoa ushahidi mbele ya Mkuu wa Chama cha Labour Keir Starmer jijini London mnamo Jumamosi kwamba anatumikia maslahi ya kikanda ya bwana wake kwa kuilinda serikali ya Myanmar. Alimwambia kwamba Bangladesh inatekeleza ‘kujizuia kukubwa zaidi’ licha ya athari za kuenea kwa mizozo ndani ya eneo lake (“PM Hasina: Bangladesh inajizuia kutokana na mvutano wa mpakani na Myanmar”, Dhaka Tribune, 17 Septemba 2022).

Kwa upande mwingine, kile kinachoitwa maslahi ya wakoloni wa Amerika katika mauaji ya halaiki ya Rohingya na kuwarejesha makwao hakiko nje ya maslahi yake ya kijiografia na kisiasa. Vikwazo dhidi ya jeshi la Myanmar na Marekani kamwe havikutokana na chembe chembe za huruma kwa wakimbizi wa Rohingya, bali kama njama ya kutumia masaibu ya Waislamu wa Rohingya kutoa shinikizo kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony J. Blinken hivi karibuni alisema kuwa serikali yake inajitahidi kuongeza kwa kiasi kikubwa makaazi mapya ya wakimbizi wa Rohingya kutoka Bangladesh. Kwa hivyo Marekani inajaribu kuweka hai suala la wakimbizi wa Rohingya ili iweze kuweka shinikizo kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar unaoungwa mkono na Uingereza. Cha kusikitisha ni kwamba Waislamu wa Rohingya wanaoteswa wamekuwa wahanga wanaochukiwa wa mzozo wa kijiografia wa mkoloni kafiri Uingereza-Marekani. Hata BNP haina ujasiri wa kuchukua msimamo mkali dhidi ya mauaji ya halaiki ya Rohingya huko Myanmar au uingiliaji wa kijeshi wa jeshi la Myanmar kwenye mpaka wa Bangladesh kwa sababu mithili ya sheikh Hasina, pia wanafanya siasa za chinichini. Kwa hivyo, kama chama tawala, BNP pia inataka uingiliaji kati wa Umoja wa Mataifa na ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa kutatua mgogoro wa Rohingya kwa kuzingatia maslahi ya Marekani. Hii ni kama kumuomba mbwa mwitu kuwalinda kondoo! Tutarajie nini zaidi kutoka kwa watawala hawa wa kisekula wasaliti ambao daima wamejitolea kulinda maslahi ya kijiografia ya wakoloni wao Marekani-Uingereza kwa gharama ya Waislamu wa Rohingya wanaodhulumiwa na maslahi ya nchi!

Enyi Watu, Waislamu wa Rohingya ni kaka na dada zetu, na hatuwezi kuwaangusha kutokana na kutokuwa na utasa wa watawala wa watumwa wa kisekula. Mtume (saw) amesema, «الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Mwislamu mwengine, hamdhulumu, wala hamsalimishi (kwa adui)” (Bukhari na Muslim). Kuvunjwa kwa Khilafah na kulazimishwa kwa mfumo bandia wa utawala wa dola ya kitaifa juu yetu ndio sababu ya kimsingi iliyoisukuma sehemu hii adhimu ya Ummah wetu kwenye dimbwi la kutisha na giza. Jueni kwamba, Waislamu waliishi Arakan tangu karne ya 8 M na walikuwa wa kwanza kusilimu katika bara hili; na kuanzia 1430 hadi 1784 Waislamu wa Rohingya walitawala jimbo la Arakan kwa msaada wa Sultan wa Bengal. Wakiwa sehemu ya Ummah huu ulionyooka, walikuwa mstari wa mbele wakati wa mapinduzi dhidi ya Waingereza katika bara hili. Mabudha walikubaliana na mabeberu wa Uingereza ilhali Waislamu wa Rohingya hawakufanya hivyo. Hivyo kabla ya kuondoka katika bara hili, Uingereza iliwatenga Waislamu wa Rohingya na kuwaacha chini ya huruma za jeshi la Myanmar. Kwa hivyo, hatuwezi kuwatelekeza enyi Waislamu! Ni fard (wajibu) juu yetu kusimama kando ya ndugu zetu wanaoteswa. Tunahitaji kuukataa uongozi huu wa kisekula wa utumwa na kujitahidi kuiregesha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itatabanni maslahi ya kweli ya Waislamu wa Rohingya na kuwapa ulinzi na hifadhi. Khilafah inayokaribia itawakomboa kutoka kwenye tundu la mfumo huu wa kinyama wa kisekula-kitaifa na kuwaoanisha ndani ya jamii yetu kama ndugu zetu. Khilafah pia haitasita kulikusanya jeshi lake kuwalinda na kuwaokoa Waislamu wanaodhulumiwa hata ndani ya Myanmar kwa kuipigisha magoti bi idhnillah.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Qur’an,

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal: 72].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu