Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  25 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 02 / 1441 H
M.  Jumamosi, 15 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wabunge wa Denmark Watangaza Kufilisika Kwao Kithaqafa

Wabunge kutoka pande zote za Bunge la Denmark jana Ijumaa, 14 Agosti 2020, walijibu amali zilizo fanywa na Hizb ut Tahrir katika mji wa Aarhus, kama sehemu ya kufichua sera ya ubaguzi wa rangi ya getto na kulinda kitambulisho cha Kiislamu. Amali hizo zilizofanywa na wanachama wa Hizb ut Tahrir mjini Aarhus zilikuwa kwa muundo wa mazungumzo pamoja na watu katika mitaa na ugawanyaji toleo linalowazungumzia watu wa Aarhus.

Licha ya kuwa, amali hizi zote ni za amani na halali kisheria, wanasiasa wamezikabili kwa mashambulizi ya cheche za maneno, huku wengi wao wakitoa wito wa kupigwa marufuku Hizb ut Tahrir, na hata wametaka wafuasi wa chama hiki kupelekwa uhamishoni!

Lakini kwa matokeo haya duni, wabunge hao wamethibitisha waziwazi kuwa ule unaoitwa uhuru wa kujieleza hauwahusu Waislamu na hususan sauti za kukosoa. Unafiki ulikuwa wazi pindi wanasiasa katika Kasri la Christiansborg (kiti cha Bunge la Denmark) katika matukio kadhaa wametetea maneno ya chuki ya Rasmus Paludan na uteketezaji Quran kwa kisingizio cha "uhuru wa kujieleza".

Na pamoja na hivyo, hakuna yeyote katika Bunge la Denmark aliye hubiri kuhusu "uhuru wa kujieleza" pindi Waislamu wanapojieleza wenyewe kwa namna inayofichua sera zinazofuatwa na kupambana na mtazamo wa kisekula ulioko katika jamii

Kanuni za kiubaguzi, marufuku na kuzidhibiti akili zinafafanua majibu ya siasa za Denmark ya kushikamana kwa Waislamu na maadili yao ya Kiislamu, huku hatua za kisheria kama vile kifurushi cha getto, kanuni ya imam na marufuku ya niqab, pamoja na kukazanisha kanuni ya shule huru ni mifano wazi ya hili. Huku wanasiasa wakitaka utiifu wa Waislamu kwa katiba na maadili ya Kimagharibi ya uhuru, kanuni moja baada ya nyengine inaletwa ambazo zinagongana na haya na kuwabagua Waislamu waziwazi.

Unafiki wa Bunge la Denmark kamwe hautakwisha. Hakika hujma za kitapeli na duni juu ya Hizb ut Tahrir kutoka kwa wanasiasa wa mirengo yote zinajaalia udhaifu mkubwa kwa thaqafa huru ya Kimagharibi kuwa dhahiri kwa kila mmoja.

Ndio, kwa mara nyengine tena tunashuhudia udhaifu kamili wa kifikra wa wanasiasa wa nchi hii, ukosefu wa usalama wa kithaqafa na ufukara wa kiroho, katika majaribio yao ya kutafuta njia zitakazo wawezesha kuushinda ulinganizi wa Uislamu.

Hakika majibu ya kiadui kwa amali za Hizb ut Tahrir ni alama ya mfadhaiko wao mkubwa kwa Waislamu kutoachana na maadili yao ya Kiislamu na kwamba bado kungali na Waislamu wengi ambao ni wachangamfu katika ubebaji ulinganizi wa Kiislamu.

Marufuku, kukataza na vitisho vya uhamisho haya hufuatwa pekee pindi mtu anaposhindwa vita vya kifikra na kutoweza kujibu hoja za upande wa pili. Hivyo basi inaweza kusemwa kwamba wanasiasa wa Christiansborg wamefichua nafsi zao na kuachana na kukabiliana na fikra na maadili ya Uislamu zisizo zuilika kwa njia madhubuti na inayofaa.

Fikra za Kiislamu haziwezi kuzuiwa, na Hizb ut Tahrir itaendelea bila ya kuchoka na kazi yake ya kisiasa ya Kiislamu. Na kufilisika kithaqafa kwa Kasri la Christiansborg hakutasaidia isipokuwa kuongezea zaidi motisha yetu ya kubeba ulinganizi kwa nguvu na msukumu mkubwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu