Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  11 Jumada II 1442 Na: 05 / 1442 H
M.  Jumapili, 24 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri wa Uwiano kwa Mara Nyengine Tena Atoa Wito wa Vita vya Kifikra dhidi ya Uislamu!

(Imetafsiriwa)

Waziri wa Uwiano, Mattias Tesfaye, alisema katika mahojiano huko Jyllands Posten mnamo 22/01/2021 kwamba "nusu ya pili" katika mvutano wa maadili dhidi ya Uislamu linaendelea! Nusu ya kwanza, kulingana na Waziri, ilikuwa kupunguza kasi ya uhamiaji kutoka nchi za Kiislamu, huku "nusu ya pili" lazima iwanyime Waislamu kitambulisho chao cha Kiislamu kupitia sheria, ikiwemo pamoja na marufuku ijayo ya shule za Waislamu.

Kwa mujibu wa serikali, taasisi zote za serikali lazima zihamasishwe katika vita hivi vya kifikra. "Ikiwa si hivyo, serikali ya Kidemokrasia ya Kijamaa itawafanyia," Tesfaye alionya.

Aliongeza: "Mtu anaweza kusema kwamba sehemu kubwa ya Uislamu leo inawakilishwa na wenye msimamo mkali. Ninachoona kuwa ni maoni ya kupindukia ni maoni ya kawaida katika duru zengine za Waislamu. Kwa mfano, maoni ya ushoga, kwamba Quran iko juu ya katiba, na kwamba wanawake lazima wafunikwe nje ya kuta nne za nyumba. "

Waziri hakuficha kile ambacho katika Uisilamu alikichukulia kutishia hali ya ustawi yenyewe: swala ya Kiislamu, marufuku ya pombe, mavazi ya wanawake na kutenganisha jinsia katika uogeleaji ilikuwa miongoni mwa mifano ya mambo "yaliyo vuka mipaka" na "hatari" ya Uislamu. Yote ni sheria za Kiislamu ambazo zimefanywa kuwa za lazima katika maandiko ya Kiislamu, na ambayo huleta tu usalama, maelewano na ustawi kwa watu na jamii endapo yanatekelezwa.

Hapo zamani, Waziri wa Uoanishaji alikuwa na matakwa ya kikashfa kwamba mashirika ya Kiislamu yahalalishe uasherati kabla ya ndoa na kuiita adhana ya swala ya Kiislamu kuwa ni "kilio cha vita." Aina pekee ya Uislamu ambayo wanasiasa wataikubali ni ile inayoitwa "Uislamu wa Kidenmark", kama Waziri alivyosema: "Lazima kuwe na Uislamu wa Kidenmark nchini Denmark. Na lazima kuwe na Uislamu mchache wa Mashariki ya Kati nchini Denmark ”.

Serikali inawataka Waislamu kwamba lazima wabuni "Uislamu wa Kidenmark" ambao unaendana na jamii na ambao Qur'an haiko juu ya katiba. Uislamu bila Sharia, mavazi ya Kiislamu, utengaji wa kijinsia, marufuku ya pombe na marufuku ya uasherati. Ambapo watoto hawalelewi na maadili kama vile tabia njema na adabu, kwani hili, kulingana na Waziri wa Uoanishaji, ni kielelezo cha "udhibiti hasi wa kijamii".

Matakwa haya ya kubadilishwa Quran kutoka kwa wajinga wa kiimla sio mpya. yalikuwa pia ni matakwa ambayo kipote cha mabwenyenye wa jamii ya Makka kwa kukosa nguvu walikabiliana nayo kwa Mtume Muhammad (saw) kwani hawangeweza kumpinga kiakili.

]وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ لاَ يَرْجُونَ لِقَاءنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـذَا أَوْ بَدِّلْهُ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاء نَفْسِي إِنْ أَتَّبِعُ إِلاَّ مَا يُوحَى إِلَيَّ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ]

“Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio taraji kukutana na Sisi husema: Lete Qur'ani isiyo kuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuati ila ninayo funuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.” [Yunus 10:15]

Tunataka kutuma ujumbe ufuatao kwa Waziri wa Uoanishaji na serikali ya Denmark:

Uislamu umejengwa juu ya mtazamo wa busara wa maisha ambao Waislamu wamekinaika nao kiakili. Hoja ambazo zinathibitisha ukweli wa Uislamu hazipingiki. Kwa hivyo, hamtaweza kufanikiwa kutuoanisha kwa nguvu sisi Waislamu ndani ya mtazamo wenu wa kisekula wa maisha kupitia udhibiti wa akili na sheria za kibaguzi.

Ikiwa mnaota kwamba lazima tuachane na maadili yetu ya Kiislamu, basi jengeni hoja kwamba mtazamo wenu wa kisekula wa maisha ni wa kweli zaidi kuliko wetu. Au kwamba muondoko wa maisha yenu ya kibinafsi na ya kimada unawiana vizuri na maumbile ya mwanadamu kuliko Sharia. Lakini, kamwe hamtaweza kufanya hivyo, na kwa hivyo mnapaswa tayari kukabili ukweli kwamba "nusu ya pili" ya vita vyenu dhidi ya Uislamu tayari vimeshindwa hata kabla ya kipenga kupulizwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu