Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  2 Rabi' I 1443 Na: 03/1443
M.  Jumamosi, 09 Oktoba 2021

Waziri Mkuu Afungua Bunge na Shambulizi Jipya kwa Familia za Kiislamu!

(Imetafsiriwa)

Katika vipindi vya kawaida na vilivyopangwa vizuri, serikali ya Denmark yawasilisha mipango ya sera inayolenga kuwashawishi Waislamu na vilevile kugeuza umakini kutoka kwa maswala muhimu ya jamii. Hivi karibuni, Waziri Mkuu alisema kuwa tume inapaswa kuundwa kuangazia wanawake wa Kiislamu. Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Bunge la Denmark mnamo Jumanne 5 Oktoba, alisema:

"Katika baadhi ya duara za kidini na baadhi ya duara za wahamiaji, wasichana na wanawake wengi wanapigania uhuru wa kuishi maisha wanayotaka kuishi [...] Kama jamii lazima tusisitize kwamba maadili yetu maarufu - usawa, uhuru - lazima yatekelezeke kwa kila mtu nchini Denmark. Pendekezo letu ni kwamba tuunde tume ya kutathmini haki na uhuru wa wasichana na wanawake."

Kwa mara nyingine tena, serikali inaonyesha muonekano hasi wa wanawake wa Kiislamu na kuutia matatani Uislamu chini ya pazia la fahamu zilizo ingizwa siasa kama "udhibiti wa kijamii". Tangazo hili la nia ya madai ya "kuwaokoa" wanawake wa Kiislamu linakuja katika wakati mmoja ambapo mwenyekiti wa zamani wa chama cha Frederiksen na Waziri Mkuu, Helle Thorning-Schmidt, amechapisha kitabu ambacho anaripoti juu ya unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na wanaume kutoka kipote cha wasomi cha jamii.

Waziri wa Frederiksen wa mambo ya nje, Jeppe Kofoed, na mmoja wa marafiki wake wa karibu wa kisiasa, meya wa zamani wa Copenhagen, Frank Jensen, amehusika katika visa kadhaa vya unyanyasaji wa kijinsia. Hata hivyo amejitahidi sana kuficha kashfa hizi na kuwaweka watu hawa madarakani. Bunge lile lile ambalo Waziri Mkuu alilihutubia limekuwa likizama katika visa vya ukiukaji wa kijinsia, ambavyo vimejumuisha karibu vyama vyote vya bunge!

Lakini Waziri Mkuu huyu ana ujasiri wa kudai kwamba ukandamizaji wa wanawake ni tatizo linalokumba "duara za kidini"!

Chaneli kubwa zaidi za runinga na magazeti zimejaa sana visa vya unyanyasaji wa kijinsia. Vivyo hivyo katika vyuo vikuu, ambapo utafiti mpya unaonyesha kuwa ni tatizo lililoenea kwamba maprofesa hutumia vibaya nyadhifa zao kuwanyanyasa kingono wanafunzi wa kike. Katika miaka ya hivi karibuni, imekuwa dhahiri kwa kila mtu kuwa mtazamo wa kudhalilisha wanawake kwa kweli unapenya sehemu zote za jamii nchini Denmark na nchi za magharibi kwa jumla.

Utafiti wa EU kutoka 2014 ulionyesha kuwa kila sekunde mwanamke wa Kideni hupitia udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia. Je! tabia hii potofu ndiyo Waislamu wanapaswa kuiga?

Mette Frederiksen anazungumza juu ya "maadili gani ya pamoja"? Je! Ni mtazamo huu mchafu wa Kimagharibi kuhusu wanawake ambao umemdunisha mwanamke kuwa bidhaa?

Waziri Mkuu anakataa kata kata kuweka nidhamu katika nyumba yake mwenyewe, na hata amepata sifa kama mlinzi wa wahalifu wa kingono. Wakati huo huo, anaendelea na uvamizi wa kimpangilio wa kisaikolojia dhidi ya Waislamu nchini kwa kurudia kuyatia matatani maadili na mfumo wao wa maisha na kuwachagua Waislamu kama watuhumiwa katika takriban tatizo lolote la kisiasa. Yeye anarusha mawe wakati amezungukwa na vigae vikali kutoka kwa nyumba ya vioo ambayo imevunjwa mbele ya macho ya ulimwengu kwa muda mrefu.

Maadili ya Kiislamu ya kumtukuza na kumheshimu mwanamke yaliyoamrishwa na Qur'an na Mtume Muhammad (saw) yanatekelezwa kwa furaha na Waislamu wengi. Visa vya Waislamu ambao hawaamiliani na wanawake kwa heshima haviwezi kuhusishwa na Uislamu, badala ya kuwa ni mielekeo ya Kiislamu, ni mielekeo ya ukandamiza wanawake ambayo imeikumba Magharibi.

Mpango mmoja wa kisiasa hadi mwengine unazinduliwa kulazimisha Umagharibi katika mfumo wa maisha wa Waislamu kwa lengo la kuharibu familia ya Kiislamu, kwa njia ile ile ambayo familia ya Magharibi imesambaratika. Kupitia uhadaifu wa mara kwa mara na matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kutoka kwenye jumba la bunge la Denmark, watu wa Denmark wakati huo huo wananyimwa fursa ya kuuchunguza Uislamu bila ya mapendeleo, ambayo ndiyo njia pekee ya maisha inayoweza inayoweza kuwakomboa wanawake Magharibi kutokana na mtazamo uliooza wa wanawake ambao vuguvugu maarufu la #MeToo limeuangazia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu