Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  27 Shawwal 1445 Na: 10 / 1445 H
M.  Jumatatu, 06 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeuri ya Kifikra Yafikia Viwango Vipya nchini Denmark

(Imetafsiriwa)

Ikiwa umesoma vyema, unajitegemea, unazungumza Kideni barabara na unatii sheria, lakini wakati huo huo ni Muislamu ambaye kiasili unabeba maadili ya Kiislamu pamoja nawe, basi unaweza kuwa hatari kwa jamii ya Denmark.

Huu ndio ujumbe ulioonyeshwa na msemaji wa Chama cha Social Democratic, wa utangamano, Frederik Vad. Taarifa ambayo imepata kuungwa mkono na Waziri Mkuu, Waziri wa Mtangamano, Waziri wa Kanisa na Waziri wa Usawa. Serikali sasa inaitisha kwa uwazi kabisa "uoanishaji uliojengwa juu ya msingi wa vima".

Huu unaoitwa "utambuzi wa tatu katika mjadala wa utangamano" hautokei kwa bahati. Ni sehemu ya sera inayoendelea ya vitisho, ambayo imedumu kwa zaidi ya miongo miwili, na ambayo inalenga kuwatisha wakaazi wa Denmark kukaa mbali na Waislamu.

Kwa vile sasa karata ya "Waislamu wote ni wahalifu" na karata ya "Waislamu wote ni magaidi watarajiwa" zimepoteza athari yake, wanataka Bw. na Bi Jensen wafikirie kwamba mwanafamasia Muislamu nchini, msimamizi wa kesi au daktari wa macho labda anashiriki katika njama ovu za kujipenyeza ndani ya taasisi za nchi.

Kwa maana nyengine, kama Muislamu inabidi uishi kwa kushukiwa mara kwa mara unapohudhuria kazi au masomo yako na kufanya kazi yako ya kitaaluma au ya umma.

Kwa njia hii, serikali ya Denmark ina mtazamo wa chuki kwa Muislamu yeyote ambaye habebi fikra ya kisekula au ya kiliberali, na hutumia unyanyasaji wa kisaikolojia dhidi ya kundi zima la watu, bila kujali ni kiasi gani linafuata sheria na kufanya kazi kwa bidii.

Hata hivyo, Kaare Dybad Bek, Morten Dahlin na Frederik Vad ndio hatari kwa jamii, kwa jeuri yao ya kifikra na maneno ya chuki ya Waislamu kuhusu jamii sambamba na kujipenyeza.

Inashangaza kwamba wanasiasa, ambao vyenginevyo wanadai kuvumiliana na kuegemeza "dira ya vima" yao juu ya uhuru na vima vya kiliberali, wanaweza kuvumilia unafiki wao wenyewe wanapotaka kudhibiti kile Waislamu wanachosema, kufikiri na kuhisi.

Kwa watu wenye uhuru wa kutafakari, kuchukuliwa, au kukataliwa, kwa maadili fulani ni jambo ambalo hufanyika kupitia mijadala ya kifikra na uchunguzi yenye lengo, ambapo hoja hukutana na hoja na kutafuta njia ya kufikia ukinaifu wa watu. Kwa njia ile ile ambapo Wamagharibi wengi hutambulishwa Uislamu kwa njia ya kukinaisha kila siku na hivyo basi kuwa Waislamu.

Nia ya serikali ya kutaka kuwaiga Waislamu kwa msingi wa vima ni ushahidi wa wazi wa kufilisika kwake kwa msingi wa vima. Wanahubiri kuhusu uhuru huku wanataka kudhibiti ni vima gani ambavyo Waislamu wanapaswa kuvibeba, na hivyo kuhujumu msingi wa jamii "iliyo na uhuru", ambayo kwa kweli imekuwa ni udanganyifu.

Hizb ut Tahrir / Denmark inalaani vikali unafiki wa wazi wa serikali, majaribio ya vitisho na ujeuri wa kifikra, ambayo tutafichua, kupambana na kusimama dhidi yake wakati wote, kama ambavyo tunatoa wito kwa watu wote wenye staha nchini Denmark kufanya vivyo hivyo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu