Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  7 Rajab 1445 Na: 09 / 1445 H
M.  Ijumaa, 19 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Marufuku ya Uingereza juu ya Hizb ut Tahrir:
Udhibiti wa Kutapatapa na Unafiki wa Hali ya Juu

(Imetafsiriwa)

Leo, Januari 19, 2024, Hizb ut Tahrir imepigwa marufuku nchini Uingereza kwa uamuzi wa kisiasa pasi na kivuli cha mchakato wa kisheria. Marufuku hiyo ilianzishwa siku nne tu baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, James Cleverly, kutangaza kwamba angeiongeza Hizb ut Tahrir kwenye orodha ya magaidi ya Uingereza. Hii, licha ya ukweli kwamba Hizb ut Tahrir inafanya kazi kisiasa na kifikra pekee, na imefanya hivyo kwa zaidi ya miaka 70.

Uongo kwamba Hizb ut Tahrir ina chuki dhidi ya Mayahudi na inakuza ugaidi ni wa wazi sana kiasi kwamba hauitaji kukanushwa. Unawasilishwa bila aibu, nchini Uingereza na hapa nchini Denmark, na wanasiasa na vyombo vya habari vinavyounga mkono ugaidi wa serikali ya Kizayuni na mauaji ya halaiki ya raia wa Palestina. Hizb ut Tahrir, kwa upande mwingine, inafanya kazi kwa ajili ya kusimamishwa upya kwa utaratibu wa kijamii wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu, ambao kwa karne nyingi ulihakikisha kwamba Waislamu, Mayahudi, Wakristo na dini nyenginezo wanaweza kuishi bega kwa bega kwa usalama.

Dola za Magharibi, ikiwemo Uingereza na Denmark, katika miezi ya hivi karibuni, zaidi ya hapo awali, zimeonyesha ukosefu wao kamili wa maadili au ubinadamu. Madai yote ya haki za binadamu na uhuru - kuishi, kuamini, kufikiri na kuzungumza - yamezikwa ndani ya magofu ya Gaza.

Kwa zaidi ya miaka 70, Hizb ut Tahrir imefanya kazi kisiasa na bila kutumia nguvu ili kuzibadilisha tawala za mateso zinazoungwa mkono na Magharibi katika ulimwengu wa Kiislamu kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah ambayo inaafikiana na imani za Waislamu. Uingereza sasa inajiunga na safu za tawala hizi za kidikteta, ambazo kwa muda mrefu zimejaribu kudhibiti ulinganizi wa Hizb ut Tahrir, kwa nguvu na adhabu. Katika kuhujumu waziwazi madai ya uhuru wa kujieleza na utenganishaji mamlaka, serikali ya Uingereza sasa inaanzisha marufuku hii ya kisiasa. Waziri wa Sheria wa Denmark, Peter Hummelgaard, mara kadhaa ameelezea nia yake kubwa ya kufanya hivyo, lakini hadi sasa hajapata njia ya kuizunguka katiba. Unafiki ni wa hali ya juu.

Hizb ut Tahrir / Denmark inalaani hatua za kutapatapa za serikali ya Uingereza, ambazo hazitasimamisha ulinganizi wa ukombozi kamili wa Palestina wala mapambano ya kisiasa ya kusimamisha tena mfumo wa adilifu wa Uislamu na kukomesha ajenda ya wakoloni wa Magharibi katika ardhi za Waislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu