Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  4 Safar 1444 Na: 1444 / 03
M.  Jumatano, 31 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Watu wa Iraq: Ni Wakati wa Nyinyi Kujichagulia Wenyewe na Kuachana na Utawala Fisadi na Viongozi wake Vibaraka.

(Imetafsiriwa)

Kiongozi wa vuguvugu la Sadri, Muqtada al-Sadr, alitangaza mnamo Jumanne alasiri, Agosti 30, 2022, katika kongamano lililopeperushwa na idhaa za satelaiti, kumalizika kwa kikao hicho na kujiondoa kikamilifu kutoka Zoni ya Kijani ndani ya saa moja. Tangazo hili lilikuja baada ya siku yenye umwagikaji wa damu, ambapo makumi ya watu waliuawa na kujeruhiwa. Al-Sadr alisema katika hotuba yake wakati wa kongamano hilo, akionekana kukerwa na kufadhaika, "Natoa pole kwa watu wa Iraq, na sasa natembea kwa aibu, damu ya Iraqi ni haramu, na muuaji na aliyeuawa wako motoni bila kujali ni nani aliyeanzisha mapigano, na sasa nayakashifu mapinduzi ya vuguvugu la Sadri baada ya kupotoka kutoka kwa hali ya amani." Aliendelea, "Kuna wanamgambo wa fedheha, na harakati hiyo haipaswi kuona fedheha, badilisheni mawazo yenu, na mujiondoe kikamilifu hata kwenye kikao hiiki ndani ya saa moja," na akamalizia hotuba yake kwa kusema: "Sitaingilia siasa zozote kuanzia sasa, na kustaafu kwangu ni kwa mwisho na halali, na tafadhali msiniulize swali lolote la kisiasa."

Kwa hivyo, Muqtada al-Sadr alifunga pazia la matukio yaliyodumu zaidi ya miezi kumi, ambapo nchi iliishi katika machafuko na ghasia, na ikapigwa muhuri wa damu, ambapo malipo yake ni moto, kulingana na madai yake.

Pia inaonekana, msimamo huu wa Al-Sadr ulikuja kutokana na mashinikizo na vitisho vya ndani, pamoja na mashinikizo ya nje yaliyowakilishwa na Iran na mvamizi Marekani, kuanzia kwa kutelekezwa kwa maregeo yake, Kazem al-Hairi, na kumalizikia na kile alichokiita wanamgambo wakorofi na akigongana na wafuasi wake. Lakini cha kustaajabisha ni vyomvo vya habari kugeuza ukweli, na kumfanya aliyeshindwa kuwa shujaa mshindi. Kutokana na tangazo hili (tangazo la aliyeshindwa) kutoka kwa kiongozi wa vuguvugu la Sadri, kauli za heshima na sifa kutoka kwa vyama vyote vya kisiasa zilimwagika juu yake. Zinatoa wito kwa kila mtu kuonyesha ujasiri na kuyapa maslahi ya nchi kipaumbele.

Ukweli uliodhihirika kwa kila mfuasi ni kwamba Muqtada al-Sadr ni mtu isiyeshikamana na rai moja; Kwa sababu maslahi binafsi yanamtawala yeye pamoja na wengine, hivyo kila anapotangaza kujitoa, au kususia kwake uchaguzi na mchakato wa kisiasa, kisha haraka hugeuka kauli yake, baada ya suluhu kufanywa na dhamana kutolewa, na kauli mbiu za kuondoa ufisadi huondoka, na kukataa mazungumzo na wafisadi na kukosa budi kuwabadilisha kupuuzwa!

Enyi Waislamu:

Kilichotokea na kinachoendelea ni mapambano ya wahalifu juu ya vyeo, ​​mapato na wizi, na wako tayari kuiteketeza nchi kwa ajili ya maslahi na kazi zao; Kwa hiyo, kutafuta wokovu kupitia wao ni kuyakimbilia mazigazi, kwa kuwa wote wana shauku juu ya mfumo huu uliooza wa kidemokrasia, kwa hiyo wanauombea na kutoa wito uhifadhiwe. Hayo yamethibitishwa na Muqtada al-Sadr mwenyewe katika hotuba yake ya mnamo tarehe 3/8/2022, ambapo alisema: “Nina hakika kwamba watu wengi wamechoshwa na tabaka zima la watawala, na kwa hiyo walichukua fursa ya kuwepo kwangu kumaliza ufisadi na nyuso za zamani hazitakuwepo tena kupitia mchakato wa mapinduzi ya amani ya kidemokrasia kwanza, kisha mchakato wa uchaguzi wa kidemokrasia wa mapema." Kwa hotuba hii, wafisadi wanataka kukuwekeni mbali na chanzo cha ugonjwa na sababu ya ugonjwa huo, mushughulishwe na mabadiliko ya nyuso, na kuacha njia ya wokovu wenu.

Umewadia wakati wa kuamka kutoka katika kughafilika kwenu, muondoe pazia machoni mwenu, na mutambue kwa yakini kwamba hakuna wokovu kwenu isipokuwa kwa kuregea kwa Mola wenu Mlezi, na kwamba: “Wa mwisho wa Ummah huu hawatasuluhisha isipokuwa kwa kupitia yale waliyosuluhisha kwayo wa mwanzo wake.” Na hiyo ni kwa kupitia kushikamana na Dini ya Mwenyezi Mungu na Shariah yake, ambayo yamevuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunnah za Mtume wake, rehma na amani zimshukie.

Hakuna izza wala heshima kwenu isipokuwa kwa dini yenu, kama alivyosema Amirul-Muuminin, Khalifah Rashid (Khalifah aliyeongoka) Omar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi katika maneno yake maarufu: “Sisi tulikuwa watu wadhalilifu, basi Mwenyezi Mungu akatutukuza kwa Uislamu, kwa hivyo hata tukitafuta utukufu kiasi gani mwingine usiokuwa ule aliotutukuza nao Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.”

Kwa ajili ya izza ya duniani na Akhera, tunakulinganieni, enyi Waislamu, mufanye kazi ya kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu, na kutekeleza sheria ya Mola wenu Mlezi chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu