Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
H. 5 Safar 1444 | Na: 1444 / 04 |
M. Alhamisi, 01 Septemba 2022 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Mashababu wa Hizb ut Tahrir
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 23]
(Imetafsiriwa)
Kwa nyoyo zenye subira na uthabiti, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Iraq inamuomboleza mbebaji da’wah, mmoja wa Mashababu wake wema, safi na mchamungu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), ndugu mheshimiwa:
Tahseen Al-Hayyani (Abu Ali)
ambaye aliregea kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Alhamisi usiku; Tarehe 5 Safar 1444 H, sawia na 1/9/2022 M, ambaye alitumia maisha yake akiwalingania rafiki zake, majirani, ukoo na watu wa mji wake kubadilisha uhalisia fisidifu na kufanya kazi ya kuunusuru Uislamu, kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, hasa baada ya uvamizi wa Iraq, alitumia juhudi na mali yake katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu (swt), na hakusita kufanya amali iliyomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu (swt), iwe ni ibada, da’wah, au kutafuta nusra kwa ajili Yake, (swt). Na yeyote aliyeishi na marehemu, alimjua kuwa ni mwalimu mwenye kupenda watu na mwenye urafiki, akitaka kukidhi mahitaji yao, alihangaika na maradhi na alikuwa na subira na kutafuta malipo, mpaka alipofariki.
Jicho linabubujikwa na machozi, moyo unahuzunika, na tumehuzunishwa na kutengana nawe, Ndugu yetu Hazem, na hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi:
[إنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Iraq |
Address & Website Tel: |