Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  26 Rabi' II 1443 Na: 1443 / 08
M.  Jumatano, 01 Disemba 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

Al-Hajj Yussuf Al-Awadhi (Abu Ayman)

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ

وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Jordan inamuomboleza mbebaji Da`wah, Hajj Yussuf Muhammad Al-Awadhi (Abu Ayman), aliyekwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu jana, Jumanne 30/11/2021 akiwa na umri wa miaka 80 ambayo aliitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu na kubeba ulinganizi wa kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Hajj Abu Ayman hakika alikuwa na shauku kubwa ya kubeba da'wah tangu ujana wake, akiwa jasiri na mkakamavu katika haki bila kuogopa lawama yoyote mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hivyo alikabiliwa na ukatili wa tawala mara nyingi, ambapo serikali ya Jordan ulimfunga gerezani mara tano na kwa miaka mingi, na alibakia thabiti katika daawah yake kwa dhamira isiyoyumba na azma isiyoteteleka, akitaraji kwa Mwenyezi Mungu kuishuhudia Khilafah, mpaka ikaja amri ya Mwenyezi Mungu na ilhali yuko juu ya hilo, roho yake ikatoka kwenda kwa Muumba wake.

Twamuomba Mwenyezi Mungu amfinike kwa upana wa rehema zake na amuingize katika mabustani yake makubwa na amlipe malipo mema kwa niaba yetu na kwa niaba ya Uislamu na Waislamu.

Ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na cha Mwenyezi Mungu alichokichukua, na hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi (swt).

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea." [Al-Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah ya Jordan

- Kalima katika Mazishi ya Al-Hajj Yussuf Al-Awadhi (Abu Ayman) -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu