Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  22 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 / 26
M.  Jumanne, 21 Juni 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Mheshimiwa Al-Ustadh Ahmed Muhammad Al-Faqir Al-Ajarmah (Abu Asim)
Mmoja wa Mashababu wa Kizazi cha Kwanza cha Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Kwa nyoyo zenye subira na kuridhia, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Jordan inamuomboleza kwa familia nchini Jordan na Ummah wa Kiislamu, mbebaji da’wah, mmoja wa mashababu wake wema, wasafi na wachamungu, wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, kutoka kizazi cha kwanza cha Hizb ut Tahrir, Ustadh mheshimiwa:

Ahmed Muhammad Al-Faqir Al-Ajarmah

Aliyefariki kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 21 Dhul Qa'adah 1443 H sawia na 20/6/2022, akiwa na umri wa miaka tisini na tatu, na ambaye alitumia maisha yake yote kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa bidii na subira akishikilia ahadi na kubeba da’wah licha ya ukongwe wake, na licha ya madhara na ugumu aliokabiliana nao, baadhi yake ikiwa ni katika magereza ya madhalimu, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu mheshimiwa ndugu Abu Asim. Alikuwa mpole, mwepesi, mwenye kuipenda da’wah na mashababu wake, akifanya kazi kwa bidii, mwenye msimamo katika haki, na akifurahia ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amghufirie na amrehemu na amkusanye pamoja na Manabii, wakweli, mashahidi na watu wema katika Pepo za neema, na hao ndio marafiki bora, na twamuomba Mwenyezi Mungu aitulize familia yake kwa subira, afueni na faraja njema.

Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu ndugu yetu Abu Asim, yakirimu makaazi yake, panua mlango wake, na umbadilishie mahali pazuri zaidi pa kuishi kuliko makaazi aliyokuwa nayo, na familia bora zaidi kuliko familia aliyokuwa nayo, na utukusanyie sisi na yeye chini ya bendera ya Mtume wako Siku ya Kiyama.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu