Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  6 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 1443 / 28
M.  Jumanne, 05 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tukio la Aqaba na Kupotea kwa Maisha ya Wasio na Hatia ni jukumu la serikali inayoongoza kwanza
(Imetafsiriwa)

Juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jordan alitangaza matokeo ya uchunguzi wa tukio la Aqaba, ambapo watu 13 walikufa, Jumatatu iliyopita, Juni 27, 2022, kutokana na kuvuja kwa gesi yenye sumu ya chlorine baada ya meli ya mafuta kuanguka katika moja ya bandari za Akaba na kulipuka, na makumi kadhaa kujeruhiwa, na akasema kwamba ripoti ilithibitisha kwamba tahadhari muhimu kwa usalama wa umma hazikuchukuliwa katika kushughulikia nyenzo hizo za hatari, na akasema: “Uchunguzi ulithibitisha uwajibikaji ni kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Usimamizi na Uendeshaji wa Bandari ya Aqaba, mkurugenzi wa idara ya uendeshaji katika kampuni hiyo, mkuu wa idara ya upakuaji na upakiaji, na mkuu wa zamu ya upakuaji na upakiaji, mkuu wa meli wakati wa ajali, na wengine.” Baadaye, Baraza la Mawaziri lilikubali kusitisha huduma za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bahari ya Jordan, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Usimamizi na Uendeshaji wa Bandari ya Aqaba, na maafisa kadhaa katika kampuni hiyo.

Hili sio tukio la kwanza kusababisha vifo vya watu wasio na hatia. Matukio haya na uzembe katika uchungaji wa mambo ya watu yamekuwa yakijirudia mara kwa mara. Tukio la Bahari ya Dead na tukio la Hospitali ya Chumvi sio mifano ya mbali na haikufungika katika mifano hii pekee. Halafu kamati za uchunguzi zinatujia zikitupia jukumu na kuweka adhabu juu ya wale ambao wako kwenye ngazi ya chini kutoka kwa ustawi na wajibu wa kiidara, ingawa hawako huru kutokana na uwajibikaji, na wale ambao wako katika ngazi za juu za utawala na idara, yaani mfumo wa utawala na taasisi zake za moja kwa moja za kuchunga mambo ya watu zimeepushwa na uwajibikaji wa kuhojiwa na adhabu.

Ufisadi wa kiidara katika serikali zote umeenea na kufikia kilele chake kwa utambuzi wa utawala wenyewe pindi unaposema: “Tunataka mageuzi ya kiidara ambayo athari zake zinaweza kuhisiwa na raia” na Waziri Mkuu akathibitisha “haja ya mapinduzi ya kiidara katika ndani ya mageuzi ya kiidara”, lakini hatafuti kiini na sababu za ufisadi huu kwa sababu unagusa moja kwa moja nidhamu na mfumo wa serikali, ambapo mfumo fisadi wa kirasilimali unatekelezwa katika utawala na idara nchini humu, iwe katika sheria za sasa au zilizochakachuliwa za kidemokrasia, juu ya ufisadi wake kwa ukamilifu wa kanuni na ulinzi wake dhidi ya dhima zote, jukumu na uwajibikaji. Maraisi wa serikali na mawaziri wao na wakurugenzi wao wa idara, vitengo na taasisi za serikali wanazunguka katika mzunguko wa mfumo huu kwanza kabisa, na kipaumbele chao sio kushughulikia mambo ya watu na kuhakikisha haki zao za kibinadamu za kuishi kwa upande wa chakula, mavazi, makaazi, afya, elimu na usalama, juu ya hayo ni hifadhi wa maisha ya binadamu, usalama na amani. Ni vipi basi uchunguzi wowote usio na upendeleo unaweza kuwafikia kwa uwajibikaji na adhabu? na ni wajibu.

Ulegevu wa kiidara uliokithiri kimsingi ni wa kisiasa, na uko mbali na hata dhana kidogo ya kuchunga mambo ya watu katika idara. Kwa mujibu wa naibu mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Aqaba, Bandari ya Aqaba ina wafanyikazi 2,370, wakati haihitaji zaidi ya wafanyakazi 700-800 kwa mtazamo wa kibiashara. Na hii ni kwa taasisi nyingi za serikali, na uteuzi huu uliokithiri ni njia inayochukuliwa na serikali mtawalia kunyamazisha sauti pinzani, badala ya kutekeleza dori yao inayodaiwa kwa kupunguza ukosefu wa ajira katika kazi halisi, au kutoa ruzuku kwa wasio nazo na kuwawezesha kuishi. Ama kuhusu vyeo vya juu katika nafasi za uwajibikaji, haswa zile zenye hila na hatari zaidi kati yazo, utoshelezi sio kigezo cha kwanza, bali ni utiifu, kwa hivyo kilichokatazwa na kilichoharamishwa kinatokea, na hakuna ubaya kwa hawa kulaumiwa kunapotokea maafa.

Sera ya kusimamia maslahi katika dola ya Kiislamu imeegemezwa kwenye usahali katika mfumo, ukamilishaji kazi kwa haraka, na utoshelevu wa wale wanaochukua idara. Hili linachukuliwa kutoka katika uhalisia wa kufikia maslahi, hivyo mtu mwenye maslahi anataka kuyafikia kwa haraka na kuyafikia kwa ukamilifu zaidi, na Mtume (saw) asema:

«إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ»

 “Hakika Mwenyezi Mungu amepitisha ihsani (ustadi, ubora) juu ya kila kitu. Basi mnapouwa uweni kwa uzuri; na mnapochinja chinjeni kwa uzuri.” Ustadi katika uendeshaji wa maslahi umefaradhishwa na Sharia, na ili kufikia ustadi huu katika kukamilisha maslahi, ni lazima kuwe na sifa tatu katika idara: Mojawapo: usahali katika mpangilio; kwa sababu husababisha urahisi, na utata huleta ugumu. Ya pili: kuongeza kasi ya kukamilisha miamala; kwa sababu humrahisishia yule mwenye maslahi. Na ya tatu: uwezo na utoshelevu wa yule aliyekabidhiwa kazi, na hii hulazimu kufanya kazi nzuri, kwani huhitaji kuifanya kazi yenyewe.

Pindi Abu Bakr al-Siddiq, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alipochukua Khilafah, yaliyojiri katika hotuba yake ni: "أيها الناس، قد وليت عليكم ولست بخيركم، أطيعوني ما أطعت الله فيكم فإن عصيته فلا طاعة لي عليكم. القوي فيكم ضعيف عندي حتى آخذ الحق منه، والضعيف فيكم قوي عندي حتى آخذ الحق له"" “Enyi watu, nimetawalishwa kwenu na mimi sio mbora wenu, ni tiini maadamu namtii Mwenyezi Mungu kwenu, pindi nikimuasi basi hakuna utiifu kwangu juu yenu. Mwenye nguvu kwenu kwangu mimi ni dhaifu mpaka niichukue haki kutoka kwake, na dhaifu kwenu kwangu mimi ni mwenye nguvu mpaka niichukue haki kwa ajili yake.” Na imeelezwa katika riwaya kwamba Khalifa Omar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: "لو ماتت شاة على شط الفرات ضائعة لظننت أن الله تعالى سائلي عنها يوم القيامة" “Lao kondoo atakufa katika kingo za Furat na kupotea, nadhani kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku moja ataniuliza kumhusu.” Ama Amiri wa Waumini, Omar bin Abdul Aziz, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: ""انثروا القمح على قمم الجبال حتى لا يُقال جاع طير في بلاد المسلمين “Tawanyeni ngano juu ya vilele vya milima mpaka isisemwe kwamba ndege ana njaa katika nchi za Waislamu” Na taswira hizi ni kwa ajili tu ya kutambua maana ya uchungaji na uwajibikaji halisi uliofungamana katika upande wa kivitendo wa hadith ya Mtume (saw), kwa Makhalifa hawa:

«أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ...»

“Hakika! Nyote ni wachungaji na kila mmoja wenu ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake, mtawala (Imam) anayewatawala watu ni mchungaji na yeye ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake …” Kwa sababu walijizingatia kuwa wao ndio kichwa cha wajibu kwa raia wao na kwamba wanahesabiwa kwa hilo, na kwa msingi huo, watawala wanahisabiwa katika Uislamu.

Enyi Waislamu:

Ufisadi wa mfumo wa kirasilimali na mtazamo wake wa idara na utawala umedhihirika kwa kila mtu mwenye utambuzi na macho. Kuasisiwa kwa dola zilizopo katika nchi za Kiislamu juu ya fikra fisidifu ya kirasilimali na ufisadi na ulegevu tunaouona, iwe katika idara au utawala, ni matokeo yasiyoepukika ya ufisadi wa asili ambayo kwayo mifumo hii imejengwa juu yake. Na mageuzi ya nchi za Waislamu, na kwa wanadamu wote, yanaweza kupatikana tu kupitia Uislamu katika imani na sheria yake. Kupitia kutoa utiifu kwa Mwenyezi Mungu pekee, Mtume Wake, waumini, Khalifah ndiye mtawala ambaye macho yake hayalali, na akili yake haitulii, isipokuwa raia wake wawe salama kutokana na tishio au hatari yoyote, na yeye ndiye anayewachunga raia wake, kuwahami, na kuchunga damu zao, wako salama chini ya kivuli chake, na wanamtumainia nafsi zao, mali zao na heshima yao. Na anawaamini na wanamuamini, na yeye ndiye ngao yao ambayo wanakingwa kwayo na kupigana nyuma yake, na anamsukuma mbali kila dhalimu na muovu. Na kwa hilo tunakulinganieni; Khilafah kwa njia ya Utume kama ilivyoahidiwa na bwana wa viumbe, Muhammad, rehema na amani iwe juu yake aliyesema:

«مَا مِنْ عَبْدٍ ‌يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»

Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akisema, “Hakuna mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamtawalishia raia, kisha akafa siku ya kufa ilhali amewahadaa raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu amemuharamishia Pepo.” (Bukhari na Muslim)

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu