Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  25 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444 / 22
M.  Jumatano, 14 Juni 2023

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Aqidah ya Kiislamu Imekita mizizi katika Ummah wa Kiislamu na Wanawajua Maadui zao, Hata kama Watawala Wanadai Vyenginevyo
(Imetafsiriwa)

Tovuti ya Taasisi ya Washington inajifafanua kama ifuatavyo: "Taasisi ya Washington inataka kukuza ufahamu wa usawa na wa kweli wa maslahi ya Amerika katika Mashariki ya Kati na kuendeleza sera zinazowalinda." Kulinda maslahi ya Amerika ili kudumisha msimamo wake kama taifa linaloongoza duniani kunahitaji kwao ulazima wa kutawala na kudhibiti kupitia ujanja wa kisiasa na operesheni za vita na ukuu wa kijeshi na kiuchumi na uporaji wa mali, ima moja kwa moja au kupitia kwa vibaraka wake miongoni mwa watawala na wafuasi wao, na pengine hii ni kauli ya malengo ya taasisi hizi na vituo vya fikra na siasa vilivyoenezwa katika nchi kuu za kikoloni kote Magharibi kwa jumla na hasa Amerika.

Uchambuzi mfupi wa matokeo ya kura mpya ya maoni ya umma mnamo tarehe 9/6/2023 iliyofanywa na kampuni huru ya kikanda mwezi Machi na Aprili, iliyoidhinishwa na Taasisi ya Washington nchini Jordan, ilisema kwamba watu wa Jordan walionyesha chuki kubwa dhidi ya umbile la Kiyahudi, na uchambuzi huo uliambatanishwa na baadhi ya data na baadhi yake zikiwa na maoni yaliyopinda yasiyo ya moja kwa moja bila ya kuchapishwa. Data hizo ni kwa ajili ya mwandishi wa uchanganuzi huo kuangazia mwelekeo anaotaka kufikia picha ya maslahi ya kisiasa yanayopotosha, na hakuchapisha matokeo kamili ya kura hiyo.

Kura hizi, hasa katika nchi za kilafi za kikoloni ambazo zina nia ya kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia mwelekeo wa kifikra na kihisia wa watu katika nchi za Kiislamu, ikiwemo Jordan, zimeundwa ili kupata matokeo maalum na ya kuhitajika mapema. Lengo lake halisi si kujua maoni ya watu kuhusu suala fulani, bali ni kuchapisha matokeo ambayo yanaathiri mtoa maamuzi. Ni kwa ajili ya kuunga mkono na kupotosha, si kwa ajili ya kuelimika. Inafichuliwa na maswali yaliyoundwa kwa njia ya kupendekeza au kupendelea, na machaguo ya majibu yameundwa ili kusaidia kuhakikisha jibu mahususi linalotafutwa na kura hizi za maoni zinazodaiwa. Inashangaza kwamba hufanywa chini ya macho ya serikali na vyombo vyake mara kwa mara, kukiuka kinachojulikana kama uhuru wa serikali, kwa kuzingatia kwamba ukusanyaji wa habari za takwimu ni marufuku ndani ya nchi, bila ruhusa rasmi.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura ya maoni kwenye tovuti ya Taasisi ya Washington, asilimia kubwa (asilimia 84) ya Wajordan wa marika yote wanapinga kuingia katika mikataba ya kibiashara na makampuni yenye uhusiano na umbile la Kiyahudi, hata kama ingesaidia uchumi wao, ikiwa ni pamoja na kupokea misaada ya kibinadamu kutoka kwa umbile la Kiyahudi hata kama iko chini ya mazingira magumu. Pendekezo hili linaonekana kuwa na umuhimu kwa utawala wa Marekani kuhusu mawasiliano ambayo serikali ya utawala wa Jordan na umbile la Kiyahudi zinafanya, kwa lengo la kufikia mkataba wa mwisho wa "Umeme kwa Maji” kabla ya mwisho wa mwaka huu, kama John Kerry, afisa wa masuala ya hali ya hewa katika utawala wa Joe Biden, na sogora wa makubaliano, walivyofanya. Mwanzoni mwa mwezi huu, mazungumzo yalifanyika na Waziri wa Nishati na Miundombinu, Israel Katz, ili kufikia muafaka, mbele ya balozi wa Marekani wa umbile la Kiyahudi, Thomas Nides. Kwa kukiri kwamba kulikuwa na kukataa kwa watu wengi kutia saini makubaliano hayo katika hali yake ya awali (tamko la dhamira), kwa kanuni ya kulichukulia umbile la Kiyahudi kuwa ni adui na kwa sababu ni mhasirika wa kiuchumi.

Ama kuhusu uhusiano wa Jordan na nchi kubwa, haswa Amerika na Urusi, kura ya maoni ilichagua swali hili. Amerika na Urusi kila mmoja ilimpiku mwengine kwa karibu, na 24% walisema kwamba Washington ni nchi ya kirafiki, huku 22% wakisema jambo lile lile kuhusu Moscow, na usomaji huu uliochaguliwa na mchambuzi ulibadilishwa, kwani ungeweza kuwa ulisema kwamba 76% ya Wananchi wa Jordan hawaichukulii Marekani kama rafiki au adui, kwa vile hatujui maneno ya swali, kama ilivyoonyeshwa na kura nyingine za awali za kimataifa. Kuonyesha ni nchi gani adui zinazoathiri utulivu wa amani katika eneo hilo, na hii inaonyesha kuwa maoni ya umma nchini Jordan yanachukulia Amerika kama nchi adui tofauti na msimamo wa serikali ya Jordan na utawala wa Amerika, ambao unaelezea uhusiano wao kama urafiki na ushirikiano wa kimkakati.

Ama Uislamu, suala ambalo linazitia wasiwasi nchi kubwa ambazo vituo vyake vya kijasusi na kiusalama vya kistratijia vinautazama kwa bidii, hususan ufuatiliaji wa wafanyikazi waaminifu na wenye ufahamu wa kisiasa juu ya hatma yake, na wale walio macho na njama za Kafiri mkikoloni za kuhujumu muelekeo wa Umma wa Kiislamu, na kuuweka mbali na mradi wa mwamko wake wa kusimamisha dola ya Kiislamu, kwa kupotosha fikra zinazohusiana na Aqidah ya Kiislamu na hukmu za Shariah, na kuiweka mbali fikra hii na fikra za vijana wake na kuwavunja moyo kwa njia mbalimbali kutokana nayo. Kwa hakika walivunjwa moyo na matokeo ya utafiti huu katika suala hili na swali halisi kuhusiana nalo.

Kwa hiyo watu wa Jordan walipoulizwa kama “tunapaswa kuwasikiliza wale wanaotaka tufasiri Uislamu kwa njia ya wastani zaidi, yenye uvumilivu, na ya kisasa,” ni thuluthi moja pekee kati yao waliokubaliana na wazo hili, na hii ndiyo nukta ya chini kabisa iliyorekodiwa kwa kuwa swali hili liliulizwa kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 2017, na 63% hawakukubaliana nalo angalau kwa kiasi fulani, kutokana na uhalali wa matokeo.

Amerika na dola za Kimagharibi zimefanya kazi kwa miongo kadhaa kupotosha sura ya Uislamu, na hata kuangamiza ardhi za Waislamu moja kwa moja, kuua watu wake na mamilioni ya watu kuyahama makaazi yao, na kutumia mabilioni ili kuanzisha kile kinachoitwa Uislamu wa wastani wa Amerika, ambao unaufanya Uislamu kuwa ibada ya mtu binafsi ulio mbali na utekelezwaji wa kisiasa wa kivitendo kwa mujibu wa kile Uislamu unachotaka kutoka kwa Ummah, na kufanyia kazi kile kinachoitwa usasa na uhuru, na kueneza ushoga unaogongana na ghariza. Kutafuta msaada wa watawala wa Waislamu na wasaidizi wao na wafuasi wao miongoni mwa wanazuoni wa masultani, waandishi waliofadhiliwa na kupitia yale yanayoitwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), na sasa inageuza uso wake na kuunga mkono kisigino chake, hasa pale Taasisi ya Washington inapoonyesha kuwa ni asilimia 12 pekee ya Wajordan wanaotazama vyema kile kinachoitwa Makubaliano ya Abraham.

Enyi watu wa Jordan, enyi Waislamu!

Hamuhitaji kura ya maoni ili kuonyesha unyoofu wenu kwa Dini yenu na ufahamu wenu juu ya maadui zenu ni nani, kwani wao ni Amerika, Kafiri Magharibi na umbile la Kiyahudi, kama vile munavyoijua imani yenu na uchafu wake unaojaribu kuzidhuru fahamu zenu sahihi juu yake, lakini kuweni waangalifu na udanganyifu mpya wao baada ya kujua kile munachokichukia. Na kuonesha ni kwa kiasi gani wanafanya kazi ya kukuvunjeni moyo na dini yenu na njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha dola yenu, dola ya Khilafah. Basi mwonyesheni Mola wenu Mlezi yale yanayompendeza kwa niaba yenu, na atavuruga njama za maadui zenu na kukupeni ushindi juu yao. Na hiyo ni kwa kuharakisha kuunusuru Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha dola yake, kuwashinda maadui zenu na kukomboa ardhi zenu, na kulifanya neno lenu kuwa juu kabisa na neno la makafiri kuwa chini kabisa.

[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ]

Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam. [Al-Anfal:36]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu