Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 28 Shawwal 1444 | Na: 1444 / 21 |
M. Alhamisi, 18 Mei 2023 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)
Kwa imani na kujisalimisha kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Jordan inaomboleza kwa Waislamu kwa jumla, na watu wa Jordan na Waislamu hasa wa Australia, mmoja wa wanachama wanyoofu, wenye subira na waheshimika wa hizb, mwenye misimamo imara yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), na sisi hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Mwanafikra wa kisiasa kutoka kizazi cha zamani cha wanachama wa Hizb ut Tahrir
Mhandisi Ismail Al-Wahwah (Abu Anas)
Ambaye alifariki dunia kwa rehema za Mwenyezi Mungu (swt) mnamo siku ya Jumatano, 27 Shawwal 1444 H sawia na 17/5/2023 M, nchini Australia, baada ya maisha yake aliyoishi katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) akibeba ulinganizi wa haki na kheri pamoja na Hizb ut Tahrir, ikifanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, kwa subira licha ya mashtaka mengi na kukamatwa kwake, vifungo vya jela mara kadhaa, na hukmu za kidhalimu ambazo ubatili wake umethibitika, kama ilivyo katika ile kesi iliyozuliwa inayoitwa “Mu’ta”, alitafuta malipo yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, akitegemea nusra Yake (swt), licha ya yale aliyokumbana nayo na kuteseka wakati wa maradhi yake.
Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alibaki imara juu ya haki aliyoibeba, mkaidi na muwazi. Alikuwa akiendelea, azma yake haikupungua, alitangaza haki kwa hotuba zake za kijasiri na mahojiano ya kisiasa ya vyombo vya habari. Alionyesha imani juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa Ummah wa Uislamu ya ushindi na tamkini na kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo daima imekuwa ndio lengo la wito wake na uhamasishaji wa Ummah.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu, maiti wa Ummah, kwa rehema zake, na amkubalie kwa mapokezi mema, na ayajaalie makaazi yake kuwa Firdaus ya juu kabisa Peponi pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, watu wema, kwani wao ndio wandani bora, na kumlipa kwa niaba yetu na Uislamu na Waislamu malipo bora zaidi. Na tunamuomba (swt) kwa ajili yetu na jamaa zake, subira, faraja, na rambirambi njema.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |