Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  23 Rabi' I 1445 Na: 1445 / 02
M.  Jumapili, 08 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je! Wakati Haujafika kwa Maafisa Waheshimiwa wa Jordan Kunyanyuka ili Kuikomboa Palestina, wakati wakiona Kundi la Mujahidina Wametikisa Nguzo za Umbile Katili la Kiyahudi?
(Imetafsiriwa)

Katika dakika chache mnamo asubuhi ya Jumamosi, Oktoba 7, 2023, nguzo za umbile katili la Kiyahudi zilitikiswa, na jeshi lake la kioga likakimbia licha ya vifaa vyake, ala na nyumba za chuma, mbele ya kundi la Mujahidina ambao walivamia maeneo yake yaliyo nyakuliwa ardhini, baharini, na hewani, na vifaa vya kawaida, wakimtegemea Mwenyezi Mungu na kuwa na imani katika Nasr yake (ushindi). Ushindi wao uliungana na sauti za "Allahu Akbar, Allahu Akbar" ambazo ziliwatisha Mayahudi maadui wa Mwenyezi Mungu na hata kuwaogopesha wale walio nyuma yao, wakiwemo wakoloni dhaifu na wahalalishaji mahusiano.

Ewe Ummah Mtukufu wa Kiislamu, pengine unaweza kugundua kuwa leo zaidi kuliko hapo awali kwamba haijalishi njama za kuhalalisha mahusiano zitaendelea kwa muda gani, na haijalishi jinsi gani watawala wenu wanalitambua umbile oga la Kiyahudi, kulilinda kwa usalama na nguvu za kijeshi kando ya mipaka kwa miongo kadhaa, na kulipa vifaa vya kisasa vya kijeshi kutoka kwa makafiri maadui wa Waislamu, sio chochote zaidi ya udanganyifu na mingati yaliyofichuliwa na ushujaa wa kufa shahidi na operesheni za jihad zilizofanywa na watoto wenu kutoka kwa watu wa Palestina katika miaka yote ya uvamizi. Na njama kutoka kwa serikali ya kimataifa ni mtetezi wa Mayahudi, ambaye kwaye watawala waovu hutafuta msaada na kulalamikia mambo yao. Hawatazuia Ummah wa Kiislamu, ambao unangojea siku ambayo unashinda juu ya umbile linalotetemeka mbele ya sauti za Allahu Akbar.

Enyi Jeshi la Jordan, Enyi Mashujaa wa Karamah, Enyi Wana wa Khalid, Shurahbil, na Abu Ubaidah (Mwenyezi Mungu awawie radhi), tunajua kwamba damu inachemka kwenye mishipa yenu na hamu ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na nyinyi mumejiandaa kuruka kama simba kuwanusuru Mujahidina huko Palestina, ambao wamethibitisha utayari wao wa kuungana nanyi katika vita vya muda mfupi kwa ukombozi wa al-Aqsa na Palestina yote. Historia itarekodi ushindi wenu kama ilivyo kwa Salah al-Din. Je! Mtasimama na Ummah wenu ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu, au mtainama ardhini ili kuwafurahisha watawala wenu na kupata ghadhabu za Mwenyezi Mungu?!

Enyi Majeshi Msioogopa, Enyi Nashamah, Maafisa Waheshimiwa: vifanyeni vyeo hivi kuwa heshima inayostahili kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake, Ummah wa Kiislamu, na watoto wenu kwa kunusuru watu wenu huko Palestina. Ima iwe ni ushindi au kufa shahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lisageni umbile hili oga na wale wanaosimama nyuma yake, malizeni mchezo huu wa ulaji njama, udanganyifu, na usaliti ambao umedumu kwa miongo kadhaa, na mufanye kazi pamoja na wale wanaojitahidi kusimamisha Khilafah ili kutabikisha Sharia ya Mwenyezi Mungu. Itasimama hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, na itatawala juu ya maadui wake wote kwani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw).

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia. [Al-Anfal:72].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu