Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 5 Rabi' II 1445 | Na: 1445 / 03 |
M. Ijumaa, 20 Oktoba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan Yaandaa Maandamano Makubwa jijini Amman Kuyaamsha Majeshi ya Ummah na Kuyataka Kuhamasika Kuinusuru Gaza na Kuwaokoa Watu Wake
(Imetafsiriwa)
[Sehemu ya Kisimamo cha Hizb mbele ya Msikiti wa Chuo Kikuu cha Jordan jijini Amman - 20/10/2023 M]
Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan iliandaa maandamano makubwa ambayo ilikuwa imeyaitisha kupitia afisi yake ya habari. Yalifanyika baada ya swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Chuo Kikuu cha Jordan leo. Iliyahutubia majeshi ya Ummah kwa ujumla na jeshi la Jordan na jeshi la Misri hasa. Iliamsha azma yao ya kuchukua hatua ya kuinusuru Gaza na kuwaokoa watu wake katika mateso yao makubwa. Haya, kwa kuzingatia kufeli kwa watawala wao na kukimbilia kwao kwenye ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa, ambayo viwango vyao vya uwongo vimeanguka, kwa kuzingatia mienendo ya watawala hawa na mawasiliano yao baina yao na maadui wa Umma barani Ulaya na Marekani, na uungaji mkono wao kwa watu wa Gaza kwa kauli zisizo na maana, kuhusu kutoa misaada, kuruhusu maandamano, na kila kitu ambacho kinapunguza mzigo wa hasira ya Ummah dhidi yao. Isipokuwa kwa kupeleka majeshi yake na kushiriki katika kupigana na Mayahudi, na kuegemea kwao kwa wakoloni makafiri, wakiongozwa na Marekani, adui wa Uislamu na Waislamu, muungaji mkono mkubwa wa umbile la Kiyahudi kwa idadi na vifaa, kwa uwazi na hadharani, na kwa bora zaidi ya kile mashine ya kijeshi ya uharibifu imezalisha.
Idadi kubwa kutoka kwa wana wa Jordan, pamoja na wanachama wa Hizb, walijiunga na maandamano hayo. Takbira na nyimbo zao zilidhihirisha wajibu aliouweka Mwenyezi Mungu (swt) juu ya Umma wa Kiislamu, watoto, na majeshi yake, ambao damu yao inachemka kwenye mishipa yao kutokana na utayari wao wa jihad na kupigana na Mayahudi, kuwanusuru watu wa Gaza, na hata kuunusuru Ummah na kuregesha mamlaka yake yaliyo nyakuliwa, ili kusimamisha Khilafah, kadhia nyeti ya Ummah.
Ustadh Salim Abu Sbitan, mmoja wa wanachama wa Hizb ut Tahrir, alitoa hotuba akinukuu kutoka kwenye toleo la hivi karibu zaidi la Hizb ut Tahrir: [هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ] “Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye” [Ibrahim: 52]
Alionyesha ushindi wa kikundi cha waumini juu ya Mayahudi waoga, ambao uliwashtua Mayahudi, na kuonyesha kiwango cha uoga wao na ombi lao la msaada kutoka Marekani. Na ziara ya Rais wake Biden kuwaunga mkono Mayahudi na kunyanyua motisha yao. Alisema wakati akimhutubia Netanyahu katika mkutano wake, "Marekani [tutaendelea] kuisaidia Israel wakati unafanya kazi kutete watu wako."
Mzungumzaji alisema kwamba watu wa Palestina hawahitaji dawa au chakula, lakini badala yake wanahitaji mtu atakayewasaidia, kummaliza adui yao, na kurudisha fahari yao. Wanahitaji jeshi la Jordan, na la Ibn al-Walid, na Abu Ubaida, ambao waliwafukuza Warumi kutoka katika ardhi ya Ash-Sham. Wanahitaji jeshi la Misri na Salahuddin, mshindi wa Makruseda. Aliongeza kuwa vita ya Karamah sio mbali na sisi wakati Jeshi la Mayahudi liliposhindwa katika nchi ya hadhi na fahari.
Aliyahutubia majeshi ya Waislamu, akisema: Ardhi ya Isra na Mi'raj inakuiteni, kwa hivyo jibu wito huo. Watu wa Ukanda wa Gaza wanaomba nusra yenu, kwa hivyo wanusuruni. Msiwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) alisema,
[أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawba:38-39]
Ustadh Abu Salim Al-Sakhri Pia alitoa hotuba nyingine ya kugusa moyo ambayo aliwahutubia watu waliokusanyika, na akaamsha shauku, na akatoa wito kwa majeshi ya Ummah kusonga ilikutoa Nusrah kwa ndugu zao huko Gaza, al-Aqsa, na Palestina, wakati ambao walipiga takbira, "Allahu Akbar" wakisimama, wakilaani kushindwa kwa watawala kuwanusuru Waislamu.
Zifuatazo ni baadhi ya kauli zilizoandikwa juu ya mabango yaliyo nyanyuliwa na waandamanaji katika maandamano haya, ambayo yalizungukwa na uwepo mkubwa wa polisi, na vikosi vya usalama katika ua wa Msikiti wa Chuo Kikuu cha Jordan na malango yanayouzunguka:
- Palestina iko chini ya mzingiro na uharibifu. Hivyo yako wapi majeshi ya Pakistan, Uturuki, Misri na Jordan?!
- Ewe Jeshi la kishujaa la Jordan ... lini mtaswali katika Msikiti wa Al-Aqsa?!
- Kamba ya Marekani ni dhaifu ... lakini kamba ya Mwenyezi Mungu iko imara!
[إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلاَ تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawba: 39]
- Enyi wapanda farasi wa Mwenyezi Mungu Songeni mbele.
- Enyi Majeshi ya Waislamu, lini hamu ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, itachochea nafsi zenu?!
- Kuwaondoa Mayahudi ndio jibu.
- Enyi Jeshi la kishujaa la Jordani ... Mayahudi ni viumbe waoga zaidi wa Mwenyezi Mungu.
- Enyi Jeshi la kishujaa la Jordan, kuweni kama Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wenye kukaribia na sio kurudi nyumba.
- Enyi Majeshi ya Waislamu, heshima yenu inakiukwa.
- Ewe Mwenyezi Mungu hatuna mwengine isipokuwa wewe.
- Ewe Jeshi la kishujaa la Jordan, vita vyenu ni kwa Mayahudi. Muko mashariki mwa mto na wao wako magharibi mwake.
- Gaza anaomba msaada wenu.
- Gaza, kihakika Palestina yote, inalilia majeshi.
- Hatutaki kufungua vivuko, tunataka kusogesha majeshi.
- Allahu Akbar ... Allahu Akbar, na izza ni ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
- Click to open image! Click to open image!

https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/jordan/3527.html#sigProIdca32f4323c
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: |