Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  7 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 17
M.  Jumatano, 15 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kadhia ya Palestina na Vita vya Gaza Zilianza Siku ambayo Khilafah Ilisitishwa Suluhisho Lake, Pamoja na Masuala Yote Yanayowakabili Waislamu, Yanaweza Kupatikana Tu kwa Kusimamishwa kwake tena
(Imetafsiriwa)

Leo, hakuna haja ya maelezo ya kina kuhusu jinsi kadhia ya Palestina ilivyoanza na kuasisiwa kwa umbile la Kiyahudi mnamo siku mwaka wa 1948. Vita vya uharibifu huko Gaza, ambako wanadamu, mawe, na miti vinaangamizwa, vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miezi saba, ikishuhudiwa na ulimwengu kwa jumla. Majadiliano rasmi na yasiyo rasmi ya vyombo vya habari, pamoja na majukwaa ya mtandaoni, yanayohusisha viwango vyote vya makundi ya binadamu, jamii, mataifa, mashirika ya kimataifa na vyama, yamefanya usomaji wa vitabu vya historia ya kisasa vya karne iliyopita kuwa usio wa lazima, pamoja na kusimulia usuli kuhusiana na kadhia hii kila upande.

Kwa hakika, vita vya Gaza kwa miezi na masiku, kufuatia upinzani wa kishujaa wa mujahidina mnamo Oktoba 7, 2023, vimefichua ukweli unaojulikana kwa watu wa kawaida na kufichuliwa kwa ummah wao wenye ufahamu wa kisiasa na wenye ikhlasi kuhusu jinsi Ummah ulifikia hili udhalilishaji, unyonge, na kushindwa kuwaunga mkono ndugu zao Waislamu huko Gaza na kwengineko duniani. Pia imefichua nani aliye nyuma yake na sababu zake ni zipi. Imekuwa muhimu na yenye umuhimu wa kivitendo kuishinda kabisa hali hii, kama ifuatavyo:

- Tawala zilizopo katika nchi za Waislamu, zote bila ya ubaguzi, zimekuwa ni vibaraka wa Magharibi tangu kuasisiwa dola zao za kitaifa katika Makubaliano ya Sykes-Picot ili kuendeleza utengano, mfarakano, na kutotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Zinasimama kama kizuizi kikubwa dhidi ya umoja na kuwanusuru ndugu na dada zao Waislamu, kwa hivyo kuwaondoa watawala na serikali hizi na kuziunganisha nchi za Waislamu imekuwa kipaumbele kuelekea kwenye suluhisho la kudumu.

- Kafiri mkikoloni Magharibi, ikiongozwa na Amerika na Ulaya, ndiye adui mkuu wa Umma wa Kiislamu. Wanashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Uislamu na Waislamu na katika vita vya Gaza. Ni hali ya kivita pekee ndiyo inayoweza kuchukuliwa dhidi yao. Watawala wasaliti hawapaswi kuwaundia kambi za kijeshi, wala kusaini makubaliano ya ulinzi au harakati za pamoja kama ile inayoitwa ‘Eager Lion’, wala kutekeleza masuluhisho yao ya kusalim amri kwa kadhia zetu, iwe ni suluhisho la dola mbili au suluhisho jengine lolote la kimataifa.

- Umbile halifu la Kiyahudi ni zao la dola hizi za kikoloni, ambazo zililipanda na kulidumisha kama uvimbe mbaya wa saratani katika mwili wa Ummah ili kuzuia mradi wake wa mwamko kwa kurudisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Duara za kijasusi za Magharibi na usalama wa taifa zinazuia kwa uangalifu kusimamishwa kwake na kusaidiwa na duara za kijasusi katika nchi zetu, ambazo watawala wake hufanya kazi ya kulilinda umbile hili na kulilinda dhidi ya hatari ya kutoweka, haswa baada ya udhaifu na uoga wake kufichuliwa baada ya Oktoba 7, 2023.

- Mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, matawi yake, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, na sheria za kimataifa zote ni zana za kikoloni za Magharibi zinazofanya kazi kwa ajili ya maslahi ya dola kubwa na chini ya shinikizo lao. Hawawezi kuwa upande wa Waislamu na hazifanyi kazi kwa manufaa ya watu wa Palestina. Kutafuta hifadhi kwao ni kama kutafuta kivuli kutokana na joto kali kwenye moto. Ikiwa mtu ana matumaini, vyenginevyo ni usaliti wa wazi.

- Nchi za kibepari za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, zinaweka sheria ya kishenzi na ya kifisadi kwa wanadamu, kupora mali za watu kwa nguvu na udanganyifu. Wanateka nyara ulimwengu kwa jina la demokrasia bandia na nguvu ya kikatili. Watu wamechukizwa na vitendo vyao, vikiwemo kukamatwa, ukandamizaji na kunyamazishwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopinga mauaji ya halaiki huko Gaza, ambayo ni ushahidi wa wazi wa kile kinachoitwa demokrasia na kufeli kwake kama mfumo wa utawala, na uthibitisho wa haja ya binadamu ya mfumo adilifu wa Mwenyezi Mungu, ambao ni Uislamu.

- Wale wanaosimama kati ya kuanguka kwa watawala hawa walioweka ahadi na mabwana zao wa Magharibi na mwamko wa Ummah leo, na hata kuwanusuru watu wetu wa Gaza, ni kundi la wasaidizi wa madhalimu hawa kutoka kwa wanasiasa wa Ummah, wanazuoni, na wanafiki ndani ya serikali. Watakabiliana tu na fedheha na aibu pekee na watatupwa katika shimo refu, watalaaniwa na watu ikiwa hawatarejea kwenye safu za Umma na Dini yake.

- Umma bado unatumai kwamba wenye nguvu miongoni mwao, askari na maafisa wao, watavua vazi la udhaifu na fedheha, watamuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuwanusuru ndugu zao katika imani huko Gaza kwa kuyapeleka majeshi yao kabla hawachelewa, kabla hajashuka ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote. Mwenyezi Mungu amewapa silaha na zana na amewafanya kuwa majeshi ya kulinda Umma na watu wake pekee, sio kuhami tawala za vibaraka zinazoegemea kwa Mayahudi na Marekani.

Enyi Watu, Enyi Waislamu!

Imetosha kwa masuluhisho tasa na ya kujisalimisha yanayosambazwa na watawala watiifu na kukimbilia kile kinachoitwa sheria ya kimataifa iliyowekwa na adui mkoloni kafiri, kama vile yale wanayopendekeza baada ya uharibifu na uhamishaji huko Gaza. Nyinyi hamna suluhisho zaidi ya yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambayo ni utabikishaji wa Uislamu ndani ya chombo kimoja: Khilafah Rashida iliyojitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ikiulinda Umma wa Kiislamu na kuwaangamiza kikamilifu maadui zake. Hairuhusiwi kuwepo dola ya Mayahudi, hata kama kando yake kuna dola ya Palestina. Ni Haramu kishariah kwa Waislamu kuwa na mahusiano na umbile la Kiyahudi isipokuwa kwa vita vya kijeshi. Hakuna mikataba au makubaliano ya khiyana yanayoruhusiwa. Wale wanaotafuta suluhisho la halali ni lazima wasitabanni masuluhisho kutoka kwa uhalisia ambao unawaweka katika mtanziko wa kuamiliana na kujadiliana na zana za wakoloni makafiri.

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلَالاً بَعِيداً]

Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali. [Surat Al-Nisa:60]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu