Ijumaa, 13 Muharram 1446 | 2024/07/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  10 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 19
M.  Jumapili, 16 Juni 2024

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi miongoni mwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]
Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan Yamuomboleza:

Dkt. Muhsin Muhammad Hilal Al Khalif Al Azamat (Abu Hafs)

Mlezi mtukufu na msimamizi wa elimu na mmoja wa wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambaye alifariki dunia kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu (swt) siku ya Arafah, tarehe tisa Dhul-Hijjah 1445 H sawia na 15/6/2024 M, akimsujudia Mwenyezi Mungu kwa kuitikia wito, juu ya Mlima Arafat, akitekeleza ibada hii tukufu ya Hijja, kwa kufuata amri na kitendo cha Mtume (saw), kama alivyokuwa siku zote, kama tunavyomchukulia yeye na Mwenyezi Mungu ndiye hakimu wake, aliyejitolea katika Uislamu kama akida na hukmu za Shariah, na mbebaji ulinganizi kwa yale yanayomridhia Mwenyezi Mungu (swt).

Dkt. Mohsin alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu, alikuwa msemaji wa ukweli, mwalimu, khatib, na mzungumzaji kwa ajili ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Alipendwa, mfasaha, mwenye tabia njema, na miongoni mwa wachamungu na wasafi. Sisi hatumtakasi kwa Mwenyezi Mungu. Hakuogopa lawama ya mwenye kulaumu katika kusema ukweli na misimamo inayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amsamehe na amteremshie rehema zake kubwa, na amjaalie kuwa miongoni mwa watu wa Pepo ya juu kabisa, pamoja na manabii, wakweli, mashahidi na watu wema, hao ndio wandani bora zaidi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipe rambirambi njema na aitie moyo wa subira na uthabiti familia yake, na awazidishie malipo yao katika msiba wao. Tunasema tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu:

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. [Al Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Kalima ya Ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Dkt. Muhsin Al Azamat

Iliyowasilishwa  kwa niaba ya Ujumbe, na Dkt. Muhammad Malkawi (Abu Talha)

Jumapili, 10 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 16 Juni 2024 M

Kalima ya Ustadh Abu Salim Al-Sakhari

katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Dkt. Muhsin Al Azamat Mwenyezi Mungu Amrehemu

Kalima ya Muadhama Sheikh Said Ridhwan Abu Iwad (Abu Imad)

katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Dkt. Muhsin Al Azamat Mwenyezi Mungu Amrehemu

Kalima ya Ustadh Muhammad Abu Al-Haijaa

katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Dkt. Muhsin Al Azamat Mwenyezi Mungu Amrehemu

Kalima ya Ustadh Muhammad Al-Fuqahaa

katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Dkt. Muhsin Al Azamat Mwenyezi Mungu Amrehemu

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu